Serikali ilitazame upya suala la ‘machinga’

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Kila mfanyabiashara ana haki ya kufanya biashara LAKINI kwa utaratibu uliopo sasa wa kuwaruhusu Machinga kuzagaa kila sehemu inaleta simanzi kubwa kwa wafanyabiashara wakubwa.

Mfano hai njoo hapa Mwanza mtaa wa Nyerere panatisha. Mbele ya maduka makubwa yamevamiwa na machinga na kuwanyima wafanyabiashara wanaolipa mapato makubwa, leseni na mapato mengine kupata wateja.

Wafanyabiashara hawa wakubwa hawana pa kusemea lakini wanaumia sana rohoni. Hivi kwa nini Machinga wamepewa uhuru wa kufanya watakalo? Hata sababu kubwa ya Wafanyabiashara wa Kilimanjaro kufunga biashara zao mojawapo ni Machinga.

Nashauri suala hili lifanyiwe utafiti na hata kuwa na kikao cha Wafanyabiashara na Serikali ione tatizo la machinga na kulipatia ufumbuzi.
 
Inabidi mjiongeze maana hawa ndo wapiga kura wetu tunaowategemea hatuwezi kuwasumbua mda huu.
 
Kila mfanyabiashara ana haki ya kufanya biashara LAKINI kwa utaratibu uliopo sasa wa kuwaruhusu Machinga kuzagaa kila sehemu inaleta simanzi kubwa kwa wafanyabiashara wakubwa.

Mfano hai njoo hapa Mwanza mtaa wa Nyerere panatisha. Mbele ya maduka makubwa yamevamiwa na machinga na kuwanyima wafanyabiashara wanaolipa mapato makubwa, leseni na mapato mengine kupata wateja.

Wafanyabiashara hawa wakubwa hawana pa kusemea lakini wanaumia sana rohoni. Hivi kwa nini Machinga wamepewa uhuru wa kufanya watakalo? Hata sababu kubwa ya Wafanyabiashara wa Kilimanjaro kufunga biashara zao mojawapo ni Machinga.

Nashauri suala hili lifanyiwe utafiti na hata kuwa na kikao cha Wafanyabiashara na Serikali ione tatizo la machinga na kulipatia ufumbuzi.
Yaani asubuhi tunaokwenda kazini kwenye Vituo vya Daladala Wanawasha Moto wa Kuni kupika Supu na Chai. Moshi unatanda kituoni Abiria tunanuka Moshi. Utakuta Machinga amesimamisha Mti katundika nyama anaikatakata. Watu wa Afya wako Wapi? Machinga ni Kero penye Mitaro ya Maji taka/mvua wameweka Mbao na juu duka. Kila Kona Siku hizi ni kutambua Tu wapi unataka weka Biashara unaweka bila kizuizi. Na Mwaka huu wa Uchaguzi watavamia kila mahali Kwa Raha zao.
 
Mkuu mwenyewe alipokua Mwz aliwaambia Wamachinga wakiona hata mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa panafaa kwa biashara zao waweke biashara zao hapo.
 
Hii sasa ndio serikali inayowajali wanyonge.

Maendeleo hayana chama
 
Hili suala wa kulaumiwa Wala siyo Rais , ni viongozi wa maeneo husika.

Akili zao zimegota , hakuna ubunifu , waoga wanadhani Rais atawafokea kumbe hapana.

Ni jukumu lao kupanga miji yao huku wakijua suala la Machinga lipo wahudumiwe pia kwa kuwekewa mazingira ya kupata wateja.

Kama hawajatengewa maeneo rafiki ni marufuku kuwagusa.
 
Hahah mkuu naona umepigilia msumari ki 'kweri kweri'.
Hii ni awamu yetu wanyonge, ninampango wa kuongeza meza tatu za kuuzia mitumba kwenye ile barabara ya kuelekea ferry.

Maendeleo hayana chama
 
Ni kweli kabisa awa chinga ni bomu limetegwa na mtegaji kalikali juu ila fuse anayo mtu mwingine.Subiri kidogo muda ni mwamuzi mzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni awamu yetu wanyonge, ninampango wa kuongeza meza tatu za kuuzia mitumba kwenye ile barabara ya kuelekea ferry.

Maendeleo hayana chama
Hahah kupiga honi tu mitaa ile wanazingua siku wakiona meza zako ni balaa hahah,ila ukifanikisha nami ntaleta meza niuze miguu ya kuku,kachori mixer mahindi ya kuchoma.
 
Muhimu uwe tu na kitambulisho cha ujasiriamali, sisi wanyonge tusipoitumia vizuri awamu hii nakuhakikishia tutajuta maisha yetu yote maana hakuna awamu nyingine tena itakayotujali na kututhamini sisi walala hoi.

Maendeleo hayana chama
 
Hili ni bomu baya kabisa na huko mbeleni linaleta matatizo makubwa sana! haya ndio makosa ya maamauzi ya watu wachache ktk mambo mazito. awamu ya 6 itakuwa na wakati mgumu mno mno!
 
Sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007

Sheria ya Mazingira namba 25 ya mwaka 1972

Sheria ya Barabara namba 13 ya mwaka 2007

ZINAPIGA MARUFUKU KUFANYA UCHUUZI WA OVYO OVYO MAENEO YA WAZI NA HIFADHI ZA BARABARA MIJINI NA VIJIJINI

MATAMKO YA RAIS SIO SHERIA
 
Mkuu mwenyewe alipokua Mwz aliwaambia Wamachinga wakiona hata mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa panafaa kwa biashara zao waweke biashara zao hapo.
Hatima ya hii ni Nini? Miji inachafuka kama Bombay India🙉🙉 Kama hawadhibitiki Siku moja tutalia. Kuna wengine wanafanya Biashara ya mnada Barabarani Siku ya Jumanne Boko Chama ni Kero Kwa Magari yote na wasafir wengine. Foleni mpaka Tegeta hakuna wa kuwaondoa.
 
Nilivoona heading ya post hii nilihisi tu unaongelea Mwanza. Kwa kweli Mwanza imechafuka sasa.
Sehem zote wanazopita waenda kwa miguu zimetwaliwa na wamachinga. Sasa hivi waenda kwa miguu wanapita barabarani kwenye magari.
Litazamwe upya hili swala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom