Serikali ilipe madeni ya watumishi

Serikali ilipe madeni ya watumishi

Administer

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
2,633
Reaction score
2,378
Nazungumzia mapunjo ya mishahara kwa watumishi mbalimbali wakiwemo wahudumu wa afya na walimu.

Fomu za kudai mapunjo hayo zilijazwa tangu mwezi January 2020 lakini hadi leo hii hakuna taarifa yoyote juu ya kulipwa.

Hii hali inawakera watumishi waliopunjwa
 
Mapunjo!
Ukiskia mtumishi anatumia Msamiati mapunjo ni kielelezo cha Ukongwe kazini au kukariri vitu. Anyway sikuhizi hakuna kitu kinaitwa MAPUNJO hilo neno lilishatoweka kwenye kamusi za Kikoloni Umepunjwa na nani sasa. Kwa sasa wanaita MALIMBIKIZO...
Mkuuu kuajiriwa ni Utumwa na Utakufa maskini, ukitaka Utajiri njoo Namanyere tulime Mpunga na Mahindi hutajuta.
 
Nimelima mwaka huu mpunga umesombwa na maji mvua kubwa
 
Nazungumzia mapunjo ya mishahara kwa watumishi mbalimbali wakiwemo wahudumu wa afya na walimu.

Fomu za kudai mapunjo hayo zilijazwa tangu mwezi January 2020 lakini hadi leo hii hakuna taarifa yoyote juu ya kulipwa.

Hii hali inawakera watumishi waliopunjwa

Serikali hainaga mpango wa kulipa madeni ya ndani.lakini vitu kama hivi vinaongeza chuki dhidi ya serikali.wangekuwa wanalipa haya malimbikizo jamani.maana kuna vitu walishaacha kabisa .mfano nauli ya likizo na stahiki zingine.

Ndiyo maana ukitaka kuwathibitishia watumishi wa uma kwamba "serikali ina hela".basi walipwe kwanza madai yao ya msingi.

Hiyo moja njoo sasa kwa wastaafu.hadi machozi yanaweza kukutoka.wengine walifanya kazi kwa uaminifu mkubwa sana.sasa hivi wanazungushwa kama wanomba msaada vile.maafisa utumishi wanawaangaliaga kama mavi vile.Neno moja wanatakiwa kukumbuka ni kwamba nao kuna siku utumishi wao utakoma .Laani hiyo haitawaacha salama.

Wengine ni wajane waume zao hawapo tena.njoo sasa kuhusi kufuatilia haki walizoacha marehemu.utafuatilia wewe mpaka mwisho unapata umasikini sababu unaambiwa faili liko utumishi Dodoma.sasa mjane mpaka atoke huko sumbawanga anafikaje huko.
 
Kuna mzee hapa anadai pesa za uhamisho(2017),Malimbikizo ya mshahara(2018) na mafao yake ya kustaafu.(2019)

Unaona muziki huo?
 
Mkuu ww ni mtumishi? una uhakika na kitu unaongea? au awamu ya malipo yako haijafika tu?

Kama haikuhusu, ungepita tu na kwenda zako ili uwaachie wale wanaoguswa na hili....

Kwa sababu na wewe unaweza kuulizwa; una uhakika kuwa kila mtu ameshalipwa?

Mimi mwenyewe nadai mamilioni...!!

Unadhani kwanini wengine tuko very aggressive wakati mwingine na serikali hii??

It's because of these things... denying our basic rights like these....!!
 
Awamu hii haijali shida za watu bali inajali vitu tu.

Ukweli ndio huo, serikali ya Magufuli inajali vitu na sio binadamu. Kuna watu wanadai serikali fedha nyingi mpaka kusababisha makampuni kufilisika kwani nao wameshindwa kulipa madeni waliokopa benki hivyo kufilisiwa; serikali haishituki juu ya shida ya watu hawa kwani inajificha kuwa inahakiki madeni huku miaka inakwenda na watu na nchi vinaathirika!

Serikali haina budi kujadili madeni yao na kuwalipa watu fedha zao halali ili wasaidie kujenga uchumi wetu uliodorola! Magufuli watu wanateseka hebu walipe madeni yao angalau kidogo waendeshe maisha.
 
Wanalipa Mkuu amini nakuambia,ila wanaanza waliokuwa wanadai nyuma kwanza,wenye madai ya hivi karibuni hawalipwi hadi wa nyuma wamalizike,mfanomara ya mwisho walilipa watumishi waliokuwa wanadai wa mwaka 2015,hivyo kama madai yako ni ya 2016 na kuendelea,awamu yao ndio hii
 
Back
Top Bottom