Serikali Ikubali Kuufumua Mfumo wa Elimu

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Kumekuwa na mjadala mzito wa kitaifa juu ya mabadiliko katika mfumo wa elimu nchini Tanzania.
Wadau na makundi mbalimbali wanataka mabadiliko ya kina katika mfumo wa elimu ili kuufanya uendane na mfumo wa maisha ya Sasa.
Ingawaje serikali bado inaamini kuwa mfumo wa elimu uliopo sio mbaya sana bali unahitaji mabadiliko madogo ili kuendana na wakati.

Mtazamo wa serikali unakinzana vikali na wadau wa elimu nchini hasa taasisi binafsi zinazosimamia elimu pamoja na wadau wengine.
Machi 2, 2022 Viongozi wa dini walipokutana Rais Samia walisema mfumo wa elimu nchini unahitaji mjadala wa kitaifa ili uweze kufumuliwa upya na kuundwa katika mfumo utakao endana na maisha ya Sasa.

Mawazo haya ya Viongozi wa dini hayatofautiani Sana na wadau wengine kwani hata aliyekuwa Spika wa bunge Job Ndugai aliwahi kumwambia Waziri wa elimu kwa wakati huo, Joyce Ndalichako kuwa sauala la mfumo wa elimu linatakiwa kuamliwa na raia kwa kutoa maoni mfumo gani wanautaka na sio kuicha serikali Pekee iamue.
Elimu yetu imekuwa na mtazamo wa kuajiriwa, kutegemea na sio kujitegemea.
Wakati huo huo elimu yetu haiamui katika uhalisia wa maisha yaliyopo bali yale yatarajiwayo.
Kuna Mwalimu mmoja aliwahi kusema mfumo wa elimu wa sasa unalenga kupima kumbukumbu za watu na sio kukuza maarifa na stadi za watu.
Pia mfumo huu hata mitihani yake imejikita katika kupima kumbukumbu ndio maana si ajabu kuona swali la mtihani likiuliza aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati Magufuli alifariki tarehe ngapi?
Mfumo wetu wa elimu umejaa makolokolo mengi ya kupotezeana muda na sio kukuza maarifa ya stadi za maisha.
Mfumo huu wa elimu ndio unafanya tatizo la ajira liendelee kuwa kubwa nchini kwakuwa hauendani na uhalisia uliopo.
Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete aliwahi kusema mfumo wa elimu yetu unazalisha wahitimu ambao kwa miaka ijayo hawatakuwa na tija yoyote.
Mfumo ambao mwanafunzi anatembea na mkoba mzito wenye daftari kubwa zaidi ya 12 hadi anapata maumivu ya mgongo lakini ndoto yake ipo kwenye daftari 5 au 6 tu alizobeba.

Mtu wa kwanza kupanda mlima Kilimanjaro aliitwa nani? yabaki kuwa maswali kwenye mfumo wetu wa elimu tutegemee kuwa na wahitimu shindani? hapana hawizekani.

Nakumbuka mwalimu wangu wa elimu ya juu Professor Wiketye aliwahi kusema "Leo hii mimi nikikamatwa na kufungwa kwenye mti nikacharazwa viboko nikaambiwaa inawezekana kijana wa kitanzania kujiajiri nitajibu hapana hata nipigwe kiasi gani"

Mwalimu alisema hali ya uchumi wa nchi yetu ndio tatizo la ukosefu wa ajira, kivuli ambacho serikali nayo inajificha katika kutetea jambo hili.
Tukatae, tukubali lakini bado huu mfumo una madhaifu kibao unahitaji mabadiliko makubwa na sio ya kitoto.
Umewahi kujiuliza 7 jumlisha 4 jumlisha 2 jumlisha 3 kuwa ni 16 ukapata jibu lake ni ngapi na kwanini iwe hivyo? hili ni fumbo.

Mfumo wa elimu ambao muhitimu mwenye miaka 25 hana ajira na hajui kushika jembe Wala nyundo amebaki mtaani akisikilizia mchongo wa ajira za Serikali.
Serikali ikubali tu mfumo huu ufumuliwe elimu iwe ufunguo isifunge maisha yetu.

Peter Mwaihola




IMG_16509045018769242.jpg
 
Huo mfumo unaodai hauko hii ni hadaa na mbwembe za wapiga propaganda za kuzima za Waliopita.

Hapa naona ni mundelezo wa propaganda za kiuhasama hasi ili tu watu wajadili hayo mafumbo yako.

Kweli hamchoki na Uhasama wa kuendeleza Ukoloni wa kifikra pamoja na Ukoloni mamboleo!

Aluta Continua.
 
Huo mfumo unaodai hauko hii ni hadaa na mbwembe za wapiga propaganda za kuzima za Waliopita.

Hapa naona ni mundelezo wa propaganda za kiuhasama hasi ili tu watu wajadili hayo mafumbo yako.

Kweli hamchoki na Uhasama wa kuendeleza Ukoloni wa kifikra pamoja na Ukoloni mamboleo!

Aluta Continua.
Mkuu wewe huoni tatizo katika mfumo wetu wa elimu?
Huoni kama taifa tunafail kwenda na kasi ya mabadiliko ya ulimwengu?
 
Nafaka,
Nimesoma vizuri tu kuhusu "mfumo' anaodai mleta vijembe(mada) hususani ya maswali ya mitihani.

Kukujibu:
Hapana na Hapana
Sababu:
Mjadala anaotaka ujadiliwe hapa haulengi mustakhabali wa Nchi
Ni mvurugaji. Anachokoza fikra.
 
Nafaka,
Nimesoma vizuri tu kuhusu "mfumo' anaodai mleta vijembe(mada) hususani ya maswali ya mitihani.

Kukujibu:
Hapana na Hapana
Sababu:
Mjadala anaotaka ujadiliwe hapa haulengi mustakhabali wa Nchi
Ni mvurugaji. Anachokoza fikra.
Unaonekana unaogopa kufikiria nje ya box. Mambo lazima yabadilike kuendana na dunia inavoenda. Kweli kuna umuhim wa kuangalia mfumo. Kuna vitu vipo obsolete kwwnye elim yetu ambavyo havimsaidii mwanafunzi. Thats why tuna large number of graduates ambao wana mawazo mgando.
 
Bangida
Nafikiri nje ya box ndio maana nimemjibu huyo juu yako Hapana na Hapana.

Kweli mambo lazima yabadilike, dunia tuliyokuwemo iwe ya kifikra au ya uasilia bado inagandamiza fikra za mwafrika na kujiamulia yanayomfaa.

Sikubaliani na hoja ya kuwa kuwafundisha watoto nani alikuwa Raisi au mlima uko wapi ni makosa ya kimfumo!

kuondolewa katika 'maswali ya mitihani" ndio suluhisho mbadala.
??
Je ni nchi gani isoyotoa historia ya Maraisi waliopita?

Huo mgando unaodai hauko.Ni propaganda hasi.
 
Kilimo cha mahindi marekani .ha ha ha alafu upo yombo dovya
Sasa unataka kuongelea Kilimo cha Mahindi Yombo Dovya wakati largest producer ni America ?

Sasa usipojifunza na kuangalia the largerst / biggest amefanya nini au ana nini wewe hata unayetaka kuwa top 1000 unawezaje kujifunza ? Yaani ujifunze through mediocres ?

Anyway ni kweli mfumo wa Elimu Duniani / na Sio Tanzania una walakini na huu automatically utabadilika tu as time goes on...., Sababu sasa hivi tumesahau Elimu kazi yake ni kuelewa na kuweza kupambana na mazingira yetu na sio ujifunze nini ili uweze kupata pesa zaidi... (hizo nyingine ni skills na individual struggle baada ya kupata basic knowledge)

Its all about knowledge na hapa tukicheza badala ya kutengeneza tutaharibu..... Na hili kupunguza hili la watu kufundisha / (kujifanya wanafundisha ili tu kutengeneza pesa) Nilishauri hivi....

Kubadilisha Mfumo wa Elimu ili Kupata Shule Zinazojitegemea na Kujiendesha kwa Faida
 
Back
Top Bottom