Serikali ifanye udhibiti wa uuzaji wa spare za magari ya Serikali na Mafuta; Tunaomiliki garage tunaumia sana mfanyacho

Madereva nao wamejiongeza. Kama mabosi wao wanakula kwa urefu wa kamba zao, nao pia wanajinafasi katika sehemu zao za kazi.

Kama tatizo ni kubwa kiasi hicho, basi kuna haja ya magari ya serikali kuwekewa vifaa maalumu ili nyendo zake ziweze kufuatiliwa kwa urahisi. Ufuatiliaji kupitia "motor vehicle tracking devices" ni wa kawaida sana ambapo serikali haishindwi kuugharamia na kuutumia.
 
Serikali inapaswa kununua magari ya Ambulance, polisi, Rais, PM, Spika, IGP, CDF na Mkuu wa UT tu, wakurugenzi wa mashirika, mawaziri, Wakuu wa mikoa na watumishi wengine wote wakopeshwe magari na/au wapewe bajeti ya mafuta.
 
Hii nchi ni ngumu sana kuongoza. Yaani unashindwa kuelewa hizitaasisi zote za usalama wa taifa zinafanya nini?. Huo wizi ulianza siku nyingi tu. Nilimaliza Chuo kikuu na kuanza kufanya kazi kwenye Wizara ya Ujenzi katika mwaka wa 88. Kuna kijana tuliokuwa tunasoma wote akaishia form four Div 4, alikwenda kusomea store keeper mwaka mmoja na akaajiriwa depot ya mafuta ya Serikali Kurasisni. Sikuamini maisha niliyomkuta nayo maana yalikuwa ya kifahari sana. Alikuwa amenunua mpaka bus ya kwenda kijijini kwao. Kuna mambo ambayo yapo kwenye hii Serikali ya CCM yanaumiza sana watu. Anyway kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake lakini yanaumiza wengi na ni wachache wanaofaidi kwa kutumia kodi zetu.
 
Mabosi kwa kutumia sheria mbovu wanafuja fedha za kodi za wananchi kununua magari badala ya kuchimba visima vya maji n.k

Toka maktaba :
Mkurugenzi ajitetea manunuzi ya gari


Hili ndilo gari aina ya V8 lenye thamani ya shs. Mil. 400 alilonunuliwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita ambapo Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) amedai kuwa ununuzi wa gari hilo ni ufujaji wa fedha za umma.


Mkurugenzi huyo wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Modest Apolinary amejibu tuhuma hizo na kusema kuwa gari hilo lilinunuliwa kwa kufuata utaratibu na waliomba kibali kutoka kwenye ofisi ya Waziri Mkuu na walipewa kibali hicho.

 
Nilishangaa siku engine ya hilux double cabin ilipo vuliwa na kuwekwa kwenye gari binafsi na ile ya gari binafsi yenye knock ikafungwa kwenye ya serikali ndipo nilipo ona serikali inajua kununua na sio kusimamia.

Magari mengi sana ya serikali yamebadilishwa usajili na kumilikishwa watu binafsi.
 
Kauli za Hangaya kumnanga Simba wa Yuda na kumdhalilisha marehemu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM ilikuwa ndo mlango wa haya yote.

Nchi imewashinda, kilichosalia ni kusaka na kuua watu wanaowapinga waziwazi.

Tuendelee kula nyama mtori upo chini
Simba wa yuda au shetani yule
 
Ni watumishi wote wa kipato cha chini
  1. Makarani wanauza sana stationery
  2. Polisi ndiyo usiseme rushwa imeshamiri
  3. Wakuu wa shule nao wanabuni mbinu kila kukicha
  4. Madereva wanauza sana mafuta (sijui wanayatoaje kwenye matank) na vipuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…