SoC04 Serikali ifanye mabadiliko kwenye Elimu ya Vyuo vya Ufundi VETA: Electrical installation, electronics na programmable logic controler (plc) kiwe kitu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mappy Bunga

New Member
May 23, 2024
3
3
Tunaona kuna wabunifu walishatokea ambao hawakuwa na elimu ya kutosha kuweza kuendeleza vipaji vyao.

Hii italeta maendeleo makubwa sana kwa Elimu ya ufundi upande wa Engineering.
Endapo kama serikali itafanya mabadiliko kwenye Elimu ya mafunzo ya ufundi wa Electrical Installation, Electronics na Programable logic controler (PLC) kuwa ni somo moja.

Kisha kuwapatia vijana wetu Elimu hiyo basi watakuwa na uwezo mkubwa sana kwenye utendaji wao wa kazi, kwa sehemu ambayo watakuwa wamepata ajira au wamejiajiri.

Dunia ya sasa hivi ipo katika mfumo wa Digital vitu vingi sana vinakuja katika mfumo wa Electronics na Programmable Logic Controller (PLC)

39027BCF-0BA5-4986-8771-4CA7E0063D55.jpeg

Chanzo: ni Picha yangu mwenyewe.

Mfano: Mitambo ya kiwandani mingi inatumia sana mfumo wa kielectronics na hata vifaa vingi vya Majumbani kwa sasa vipo katika mfumo wa kieletronics zaidi, kwa sasa tunaona kuna majiko ya umeme ya kielectronics na baadhi ya vitu vingine pia.

Electrical na electronics vinategemeana, electrical na electronics vikiungana ndo vinaenda kuunda kitu kinaitwa PLC, na kwa sasa PLC ndio mfumo unaotumika sana kwenye mitambo na kwenye machine za viwandani.

Mwanafunzi kupata mafunzo pekee ya Electrical Installation ni sawa na kumludisha kwenye zama za Analogy, hawezi kufanya kazi katika mifumo ya kidigital ambayo mifumo mingi inatumia PLC.
3FC14DDA-6D1D-42C2-AFAF-E863877AD534.jpeg

Chanzo: Ni picha yangu mwenyewe

Na aliyesoma Electronics peke yake bado atakuwa na shida ya kumuitaji Fundi Umeme, kiasi kwamba huenda ni kitu tu kidogo ambacho angeweza kukifanya yeye mwenyewe lakini kwa vile hana taaluma ya Umeme inabidi amtafute Fundi wa Umeme.

Wakati mwingine inamlazimu mtu kuludi tena shule, kama mwanzo alisoma Electrical Installation basi safari hii ataludi tena shule kusoma Electronics na kama alisoma Electronics basi ataludi tena shule kusoma Electrical Installation ili aweze kwenda sawa sawa na soko la ajira kwa sasa jinsi lilivyo.

EA6FD9FE-6AEF-4679-B7B2-982E82D6DE89.jpeg

Chanzo: Ni picha yangu mwenyewe

Na ikumbukwe kuwa umri unazidi kusogea na ili aweze kuajiriwa anatakiwa awe na uzoefu.

Sasa kama muda mwingi ataupoteza kuludi shule kusoma na muda atakaoutumia kupata uzoefu adi kuja kupata ajira ni miaka mingapi atakuwa ametumia?

Na tena apo bado itaitaji uyu mtu ripoti zake za kazi awe anazituma kwa njia ya computer kwenda kwa mkuu wake wa kazi.

Itamlazimu aludi tena shule kusoma maswala ya microsoft word, excel.

Na tena sehemu nyingine waajiri wanataka Fundi awe anajua na kuendesha gari ili wasiajiri dereva wa kumpeleka fundi sehemu ya kazi.

Sasa kwa mtu ambaye bado ajapata ajira asipojua ivi vitu hapo awali itakuwa ni ngumu sana kwake kupata ajira kwa sababu soko la ajira sasa hivi limebadilika sana.

Kwa hiyo inabidi na sisi tubadilishe mifumo yetu ya Elimu tutoke kwenye ANALOGY tuende kwenye DIGITAL ili tuende sawa sawa na soko la ajira lilivyo kwa sasa na hata hapo baadae.

Mifumo mingi bado inawapiga sana chenga wanafunzi wa vyuo vya ufundi kwa sababu Elimu wanayoipata kwa sasa bado haitoshi au haiwatoshelezi ili kwenda sambamba na mifumo wanayokutana nayo kwenye kazi.

4F16B7D9-0024-4B7F-9BDD-76E8655EB559.jpeg

Chanzo: Ni picha zangu mwenyewe

Kwa kifupi ni kwamba Elimu wanayoipata Darasani ni ndogo kuliko kitu wanachoenda kukutana nacho kwenye kazi na taaluma yake haimtoshelezi kukabiliana na ukubwa wa kazi anaokutana nao.

Akiingia kwenye ajira anakutana na kazi kubwa kuliko uwezo wa Elimu alioupata Darasani.

Serikali inabidi iunganishe somo la Electrical Installation, Electronics na PLC kuwa kitu kimoja ili kumpatia unafuu wa kupata ajira kwa haraka au kujiajiri mwenyewe kwa sababu mwanafunzi akipata Elimu ya hivyo vitu vitatu kwa wakati mmoja nina uhakika tayari atakuwa na elimu ya kutosha kuweza kuajiriwa kwa urahisi au kujiajiri mwenyewe.

Kwa sababu mifumo yote ya kazi inayomzunguka tayari ana elimu nayo tofauti na ilivyo sasa

Hivyo basi ataitaji kujifunza vitendo kwa muda mchache tu ili kupata uzoefu wa Kazi na atakuwa tayari ameweza kukabiliana na ukubwa wa kazi uliopo mbele yake kwa ufanisi mzuri wa kazi.

Tukishabadilisha mfumo huu wa Elimu ya Ufundi upande wa Engineering katika vyuo vya VETA, serikali iwe inawapa nafasi ya kuchaguliwa kwenda kusoma kwenye vyuo vya serikali vya Ufundi VETA, Kama ilivyo kwenye level ya Diploma, Mfano: Dar es salaam Insitute of Technology (DIT)

Mana sio wazazi wote wanaoweza kusomesha watoto wao kwenye vyuo kama DIT.

Wazazi wengine uwezo wao ni kuwasomesha VETA, hivyo ninaiomba Serikali ifanye jitihada za dhati kabisa ili kuboresha Elimu ya Ufundi Umeme upande wa Engineering kwenye vyuo vya ufundi VETA.

Naamini tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana katika kuwapa wanafunzi wa vyuo vya Ufundi, Elimu bora inayokidhi Mahitaji ya soko la Ajira Tanzania.

Ahsante.
 
Kwa kifupi ni kwamba Elimu wanayoipata Darasani ni ndogo kuliko kitu wanachoenda kukutana nacho kwenye kazi na taaluma yake haimtoshelezi kukabiliana na ukubwa wa kazi anaokutana nao.

Akiingia kwenye ajira anakutana na kazi kubwa kuliko uwezo wa Elimu alioupata Darasani.
Duuuh! Sa si atachanganyikiwa.!
Ndiyo maana insha zoye kuhusu elimu humu zinataka mfumo uendane na mazingira ya sasa. Ni kawaida kabisa ya elimu kubadilika kulingana na mazingira ya wakati huo. Wazungu walishasema life long learning

Naamini tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana katika kuwapa wanafunzi wa vyuo vya Ufundi, Elimu bora inayokidhi Mahitaji ya soko la Ajira Tanzania.

Ahsante.
Sawa sawa mkuu
 
Duuuh! Sa si atachanganyikiwa.!
Ndiyo maana insha zoye kuhusu elimu humu zinataka mfumo uendane na mazingira ya sasa. Ni kawaida kabisa ya elimu kubadilika kulingana na mazingira ya wakati huo. Wazungu walishasema life long learning
Ni kweli lakini utakuta mtu anaandika kwamba mfumo wa Elimu ubadilike pasipo kurekebisha kiini cha tatizo ambalo serikali ingeweza kushughulikia kwa haraka zaidi na mfumo kubadilika.

Mana hata huyo anayetaka mfumo wa Elimu ubadilishwe nae hajui unabadilikaje?

Sasa huoni kuwa hilo bado ni tatizo?

Shida kubwa kwa wanafunzi wa vyuo vya ufundi ni uelewa mdogo sana wa vitu kiasi kwamba itamchukua muda mrefu sana kupata experience ya kazi.

Elimu wanayoipata kwa sasa bado haiwatengenezi kuwa na uelewa mkubwa wa vitu.

Ndo mana mimi nimetoa majibu ya Jinsi ya mfumo wa Elimu ya vyuo vya ufundi unavyotakiwa kubadilika.

Serikali Iunganishe somo la Electrical Installation, Electornics na PLC kuwa somo moja hapo tutakuwa tumeweza kumpatia mwanafunzi uelewa mkubwa sana na kuweza kumudu kazi kwa ufanisi mzuri.
 
Back
Top Bottom