Serikali ianzishe whistle blower system, itasaidia kufichukua ufisadi na majipu

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
Baada ya kusoma thread ya mwana-jf mmoja aliyotoa kuhusu mambo yasiyo sawa ndani ya Mradi wa taifa wa TB Na ukoma (NTLP), napendekeza serikali iangalie uwezekano wa kuwa Na utaratibu Na mfumo wa wapiga filimbi (whistle blowers). Hii itasaidia kupata taarifa mbalimbali zinazohusu ufisadi Na majipu.

Hiki kitu si kigeni hapa nchini maana mashirika ya kifadhili kama USAID, DANIDA, DFID,CDC etc pamoja Na NGOs za kimataifa zilizo nchini zina utaratibu huo.

Advantage ni kuwa taarifa za ufisadi Na majipu zitapokelewa mapemana Kwa haraka. Na serikali izifanyie kazi. Haya hivyo iwe makini kutafuta ukweli ikiwa ni pamoja Na uchunguzi Na management audit.

Utaratibu wa whistle blowers unaweza kuwa chini ya chombo kinachojitegemea mfano chini ya presidential delivery bureau, au chini ya TISS au chini ya TAKUKURU au mamlaka nyingine itakayofaa.

Utekelezaji wake urahisishwe Kwa kuweka namba maalum ya kupiga simu au kutuma ukumbe au iwepo email.

If we want to succeed katika mapambano ya ufisadi basi naomba Waziri wa utumishi Na utawala Bora alifanyie kazi.

Thanks
 
Back
Top Bottom