Serikali Iache Kamata Kamata Wapinzani

Serikali Iache Kamata Kamata Wapinzani

Bowie

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
4,373
Reaction score
6,086
Hili jambo la kukamata viongozi wa upinzani na kunyima dhamana watu wenye kesi mbalimbali imeanza kuleta dosari kwa serikali ya awamu ya tano.

Mheshimwa Rais Magufuli angalia sana suala hili kwani imeanza kuweka dosari kwenye legacy ya utawala wako.

Unafanya mazuri kwa watanzania maoni ya wapinzani ni muhimu kwa kurekebisha mabaya kwenye serikali yako. Kumbuka ulivyomsifia Kafulila alivyoibua hoja ya Escrow wakati akiwa mbunge wa upinzani bungeni.

Tanzania ilikuwa ni nchi pekee kwenye ukanda huu katika kutimiza demokrasia ya kweli itakuwa vigumu kwa wawekezaji kuja hapa Tanzania kama demokrasia itakufa
 
Siwezi kudhibitisha pengine labda inawezekana ni kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna kitu kibaya kama ukiwa na tabia hiyo,maana wale walio na uelewa mpana wanapokuchallenge unaona kama vile wanakudharau sasa ukiwa kiongozi unatumia madaraka yako kuwaumiza sababu unajifia kama watakufanya nini bila kujua unaharibu zaidi badala ya kuwakomoa
 
Kama watakusikia.....lakini ushauri wako ni mwema sana.
 
Back
Top Bottom