Serikali iachane na mfumo wa boarding school

Teknocrat

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
3,803
8,420
Tuanze kuelewana,

Elimu ni gharama sana, hasa ukiongelea hizi shule za sekondari za boarding zinazoendeshwa na serikali. Serikali kuendesha shule za boarding kwa sasa imeshapitwa na wakati.

Shule zote za serikali zilitakiwa kuwa za day (mchana tu) na hii itasaidia kila mkoa kuzitumia shule zilizo mkoani kuinua kiwango cha elimu cha mkoa huo badala ya kujazwa na wanafunzi kutoka mikoa mingine.

Najua tatizo nyingi zimejengwa vijijini hasa ndani ndani huko na kuwa vigumu, lakini ndio mwelekeo uliotakiwa. Duniani shule za boarding ni zote huwa za private na ni watu wenye uwezo ndio wanapeleka watoto wao, kitu cha ajabu na kushangaza nchi masikini kama Tanzania inajing'ang'aniza kuendesha huo mfumo na matokeo yake shule zinakuwa kama ni bora liende tu hivyo hivyo.

Shule za boarding iliwezekana wakati ule wa zamani wa kuchuja wanafunzi na kubaki na wachache ambao ilikuwa na uwezo wa kuwaghamia, na ilikuwa njia sahihi sababu umasikini wa wananchii wake.
 
Tuanze kuelewana,

Elimu ni gharama sana, hasa ukiongelea hizi shule za sekondari za boarding zinazoendeshwa na serikali. Serikali kuendesha shule za boarding kwa sasa imeshapitwa na wakati.

Shule zote za serikali zilitakiwa kuwa za day (mchana tu) na hii itasaidia kila mkoa kuzitumia shule zilizo mkoani kuinua kiwango cha elimu cha mkoa huo badala ya kujazwa na wanafunzi kutoka mikoa mingine.

Najua tatizo nyingi zimejengwa vijijini hasa ndani ndani huko na kuwa vigumu, lakini ndio mwelekeo uliotakiwa. Duniani shule za boarding ni zote huwa za private na ni watu wenye uwezo ndio wanapeleka watoto wao, kitu cha ajabu na kushangaza nchi masikini kama tanzania inajing'ang'aniza kuendesha huo mfumo na matokeo yake shule zinakuwa kama ni bora liende tu hivyo hivyo.

Shule za boarding iliwezekana wakati ule wa zamani wa kuchuja wanafunzi na kubaki na wachache ambao ilikuwa na uwezo wa kuwaghamia, na ilikuwa njia sahihi sababu umasikini wa wananchii wake.
Wewe utakuwa umesoma day school ndio maana huoni umuhimu wa boarding school.
 
Boarding school zinasaidia wanafunzi kuinua kiwango chao cha elimu wakiwa bweni watoto ni kusoma tu tofauti akiwa anajichanganya mtaani.
 
Boarding school gharama yake ni ndogo sanaaaaa hasa Kwa shule ambazo serikali zinatia mkono hujui kuhusu Boarding school Yani gharama zake ni sawa tu na day ambazo wanakula shuleni hazitofautiani hata kama Niko Ruvuma dogo akasome Tabora Boys bado ambae wewe unalipia chakula na Mimi ninaetoa nauli wewe ndo unatoa Hela kubwa fikiria tena sikuafiki hata kidogo
 
Kuondoa shule za boarding ni jaribio baya la kuleta ukanda na ukabila na kuondoa umoja wa kitaifa.
kuwaleta pamoja vijana wa mikoa, kanda, kabila na dini tofauti kupitia shule za bweni ni kuwapa taswira kuwa wamo katika taifa la watu wa namna nyingi kukubaliana kuishi kwa upendo, mshikamano, na umoja.
 
Boarding iwe kwa watoto wa A level tu hawa wadogo wanateseka sana. Mtoto unampokea katoka boarding utasema ni mkimbizi wa Yemen
 
Back
Top Bottom