Serikali haiwezi kukwepa jukumu la kuwaongoza wananchi namna bora ya kuishi maisha mazuri

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Juzi nilisikia kiongozi wetu akiwaambia wananchi kuwa "wale wanaojenga mabondeni wanachagua wenyewe na hivyo taifa halitawaonea huruma".

Mkuu mwingine kabla ya hapo alisikika huko Lindi akituambia wanaokumbwa na mafuriko wanajifurikisha.

Dare es salaam miaka ya nyuma kidogo tulishuhudia watu wakibomolewa makazi maeneo ya bonde la msimbazi "over night" na kusababisha taharuki kubwa kwa wakazi wale.

Kila mwaka mvua zikinyesha tunasikia viongozi wakiwaambia wakazi waliojenga mabondeni kuhama na kuwaambia hawatapewa msaada kwamba wanajitakia.

Miaka ya nyuma kidogo tumeshuhudia bomoa bomoa nyingi maeneo mengi na serikali ikidai wananchi ni wavamizi hivyo wote wanaobomolewa hawalipwi chochote.

Binafsi taarifa hizi za viongozi zimekuwa zikinifadhaisha saaana maana ninatambua mwananchi mmmoja mmoja hawezi kutambua eneo sahihi la kuweka makazi yake au kuweka shughuli yake bali kwa serikali kutumia wataalamu kuwaongoza wananchi kuwa anayetaka kufanya maendelezo haya katika ardhi afanye hapa.

Yaani hili la kupanga matumizi bora ya ardhi ndilo jukumu la msingi la wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi.

Pale serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa kuwaambia wananchi

1. Hapa ni sehemu ya kukaa makazi ya watu tu
2. Hapa ni sehemu ya kuweka shughuli za ibada
3. Hapa ni sehemu ya kuweka viwanda
4. Hapa ni sehemu ya vyanzo ya maji
5. Hapa wanaotaka kufanya kilimo
6. Hapa wanaotaka kujenga mashule, hospitali, masoko au huduma za kijamii wafanye hapa

Kama serikali isipotimiza wajibu wake huu wa kupanga matumizi ya ardhi ili kuleta tija katika maisha ya watu ni wazi utakuta viwanda vimejengwa makazi ya watu na watu wanaishi maeneo ya viwanda, huduma za jamii hazina nafasi katika makazi ya watu.

Haiwezekani kuwaacha watu wenyewe wajiamulie pa kukaa au pa kuweka shughuli za maendeleo alafu utegemee kila mmoja atafanya kwa mujibu wa sheria zinasemaje au mazingira yanataka nini.

Mambo mengi yanahitaji uelewa, yanahitaji uzoefu, yanahitaji mtizamo wa pamoja ili kuweka utaratibu wa kijamii nzima na pale mtu mmoja mmoja anapoachiwa kuyatizama kivyake ndio mwanzo wa migogoro na matatizo.

Binafsi nilisikitika sana pale nilipoona nchi imeunda wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi na badala ya wakuu wa nchi kumuuliza waziri husika ni kwanini watu wnakaa mabondeni, sehemu ambazo hazifai kuweka makazi ya watu iwe ni vijijini au mijini bado wakuu hawa wanawaambia wananchi hakuna atakayewajali maana mliamua kukaa wenyewe.

Yawezekana kweli waliamua kukaa wenyewe lakini ni nani aliyewaonyesha sehemu sahihi ya kuweka makazi wakakaidi?

Leo hii tunahangaika kupeleka umeme na maji vijijini lakini practically sote tunajua vijiji vyetu vimekaa holela, nyumba moja hapa nyingine kule kiasi ambacho ni haiwezekani kwa wana kijiji hawa kupata huduma hii kutokana na kutokuwepo mpangilio wa makazi.

Kila mwananchi anapochukua eneo iwe ni peke yake akiwa kilomita kadhaa kutoka wenzake anakaa na serikali baada ya kukaa ni kuanza kufanya jitihada za kuwapa huduma watu hawa wanaotawanyika ovyo.

Kama Mwalimu Nyerere miaka hiyo akiwa na wataalamu wachache na rasilimali kidogo alibaini wananchi kukaa holela kusikokuwa na mpangilio kulikwamisha jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi akaamua kuanzisha vijijji vya ujamaa ili kuwaleta wananchi pamoja ili awahudumie, ni kwanini wakubwa hawa wasimuulize Waziri mhusika wa Wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi ni kwanini hajabuni mpango wa makazi vijijini ambao utahakikisha wananchi wanakaa pamoja ili serikali iwahudumie kwa wepesi?

Mfano zinaweza kuanzishwa centers za makazi vijijini na maeneo ya mashamba pembeni ya makazi.

Katika haya makazi wananchi waishi pamoja na huduma za msingi kama maji, umeme, zahanati, shule, masoko vinapatikana hapo kwenye hizi centers na wanatoka kwenye center zao na kwenda kulima au kuvua au shughuli nyingine za kiuchumi nje ya centers zao.

Kuanzisha makazi haya tutumie wataalamu katika kila halmashauri kubaini maeneo bora ya kuweka makazi na kubaini maeneo bora ya kuweka shughuli za kilimo. iwe ni sheria kila mwananchi anayeanzisha makazi ni lazima akae kwenye makazi na ni marufuku kufanya kilimo au kitu chochote kisichoruhusiwa ndani ya makazi.

Watu wakae pamoja na serikali ikisema tunapeleka umeme kijiji fulani ukifika na ukasema 27,000 kuunganisha una uhakika zaidi ya 50% ya wanakijiji watapata umeme na sio mazingira kuruhusu only 5% na tukaendelea kujipongeza.

Najua wapo watakaokurupuka na kuanza kutaja athali zilizotokana na kuhamishia watu vijiji vya ujamaa lakini kwangu mimi naamini tukifikiri positively tunaweza kuboresha.

Sio kwa kuhamisha watu kwa nguvu kama miaka ya zamani bali kwa kuweka dira kuwa ndani ya miaka 20 ijayo tutaondoa mfumo wa vijiji holela na ikifika miaka ishirini tunataka vijiji vyote viwe vimengia katika utaratibu maalumu. watu wajipange taratibu, serikali ibainishe maeneo na watu wahamishe makazi yao ndani ya mda utakaotengwa.

Inasikitisha kuona tunaweza kuwaondoa watu kwenye kutumia Tv za vichogo kwa kuweka ukomo lakini hatuwezi kuwaondoa katika maisha holela yenye adha na karaha na kuwaweka katika maisha yenye utaratibu yatakayotatua changamoto nyingi hasa kwenye huduma za msingi kama elimu. afya, maji, umeme, ulinzi n.k

Hii wizara imeshindwa hata kudhibiti makazi mijini, yaani leo hii hata ukinunua hekari 5 katikati ya mji na kuziweka kusubiri miaka ijayo uuze ruksa, hata ukiamua kusogea kilomita mbili nje ya mji, ukajenga nyumba yako na kuanza kuipigia kelele serikali ikuletee maji, umeme, shule na kadhalika wanasiasa watakufuata na kuanza kukupa ahadi, hata ukiamua kwenda katikati ya makazi ya watu ukaweka kiwanda ruksa, ukiamua kukodi vyumba vitatu kwenye makazi ya watu na kwenda kusajili kuwa shule unasajiliwa na kuanza kutoa elimu.

Sina maana ya kushauri tuanze kuwekeana vikwazo bali nashauri wizara husika itoe dira, itumie wataalamu katika kila halmashauri kuanza kubadilisha miji yetu, tupewe kipindi cha mpito cha kubadilisha makazi yetu.

Kama maeneo hayana sehemu za huduma basi sehemu zibainishwe na watu waondolewe na yawezekana tukawa tunachangia kupitia kodi maalumu kuwafidia wanaohama.

Kila mwananchi apewe dira ya kutazama na kipindi cha mpito kikiisha ajue anatakiwa makazi yake yaweje.

Ni kwa bahati mbaya sana tunachagua mfumo wa uongozi kama wa baba diamondi, mfumo wa baba diamondi ni kumtelekeza mtoto usijue anakua vipi ila unaibuka akisha kuwa mkubwa, kama atakuwa amefanikiwa basi unamlilia akusaidie na kama kaharibikiwa basi unamhukumu kwa maovu yake.

Serikali isijifikiri kama Afisa Elimu niliyemuona kwenye mitandao ya kijamii akijitetea kwa nguvu kuwa yeye kama Afisa Elimu wa Wilaya hana wajibu wowote katika mabweni ya wanafunzi yanayoratibiwa na wazazi wenyewe na mkuu wa wilaya akamuweka ndani masaa 48 baada ya mabweni kuungua kwa kumkumbusha kuwa yeye kama Afisa Elimu wa Wilaya anawajibika kwa kila jambo linalogusa elimu katika wilaya yake.

Liwe linafanywa na serikali au wananchi wenyewe ni lazima aratibu na kushauri au kusimamia kuhakikisha mazingira bora ya elimu katika wilaya yake.

Hivyo hivyo Waziri wa Ardhi anawajibika kwa jambo lolote linahosu makazi katika nchi hii ili kumkukusha kuwa hata kama mambo yalishavurugika huko nyuma lakini aonyeshe anafanya jitihada gani kututoa huko na kutuweka katika dira mpya katika miaka kadhaa ijayo

Mijini
 
Mawazo kama haya kama yanatumika na kuchambua mbona linawezekana tu
Kweli ni jukumu la serikali kubuni na kuweka mikakati kila wizara na ndio maana walipewa hizo kazi
Ukiangalia wenzetu miradi na maendeleo yote yanafanyika ili kurahisisha maisha ya watu.
Hebu fikiria sehemu kama Dar ambapo ukiangalia ramani ya zamani kulikuwa na streams kama sio mito ikipita maeneo mengi
Sasa mbona serikali iliacha watu wakafunga vyanzo vyote vya maji kwa kujenga na kubaki wanaangaliwa tu?
Ni wakati sasa watengeneze man made rivers ili kupunguza hii kadhia ya kila mwaka
Hata mkakati huo ukipangwa kwa miaka 10 kuanzia sasa linawezekana ila
tatizo tunataka kila kitu kifanyike siku moja


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom