SERIKALI (CoET, UDSM): MSIPOLIFANYIA KAZI HILI MAPEMA.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SERIKALI (CoET, UDSM): MSIPOLIFANYIA KAZI HILI MAPEMA....

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BIG X, Nov 6, 2011.

 1. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Niongelee hasa upande wa CoET pale UDSM;

  Hivi karibuni serikali imekuwa ikiajili sana vijana wanaomaliza chuo kama maTA. Wengine wameunganisha moja kwa moja kwenda kusoma masters n.k. Lakini hawa vijana pamoja na kufanya vizuri underGRAD ( GPA nzuri n.k) bado wanahitaji wapate mafunzo ya vitendo mapema iwezekanavyo ili waje kuwa walimu wazuri na watakapokuwa wanafundisha waelewe wanafundisha nini kulingana na experience watakazo kuwa wamepata wakiwa site. Lasivyo wanafunzi watakaofundishwa nao hawatapata mafunzo mazuri kutoka kwao, Sababu kuna maswali kutoka kwa wanafunzi ambayo ni rahisi mwalimu kuyajibu ukiwa unauzoefu na mazingira ya jinsi kazi zinavyofanyika.

  Ushauri wangu ni kwamba: Serikali ina miradi mingi, basi ijaribu kuwachomeka hawa vijana huko wapate kujifunza zaidi, sababu nina uhakika hawa vijana watakuwa wepesi kujifunza haraka, ili waje kutoa elimu bora kwa wanafunzi. Angalau kuwe na utaratibu wa kuwashirikia kwenye miradi inayoendelea nchini.

  Elimu ndio ufunguo wa maisha.
   
 2. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kabisa BIG X, mi naweza kutoa ushuhuda kwenye hili.

  Kuna Dr. mmoja ambaye yupo kwenye moja ya hvyo chuo. Kuna siku aliniuliza eti kwenye SLAB zile nondo za juu (Top bars on slab edges) zinasimama vipi, nilimshangaa sababu alikuwa hajui kwamba kuna nondo zinawekwa (maarufu kama magoli) kabla ya kucast concrete. Dah! nikapata picha sijui huko madarasani vipi, enzi zetu mbona walimu walikuwa wanajua haya mambo, walijifunza vipi!!

  Kwahiyo nakubaliana na wewe kabisa ushiikishwaji wao kwenye miradi ya serikali inayoendela sababu wanafunzi watakaowafundisha ndio wanapoelekea huko. Na vilevile miradi mingi inafanywa na kampuni za kigeni kwahiyo wanaweza kusaidia kupata elimu kutoka kwenye hizo kampuni za kigeni na kuwaongezea elimu wanafunzi.
   
 3. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  kaka kampuni gani ya kigeni ije hapa nchini halafu impe mbongo nafasi katika mambo ya ki-technical? Ushahidi angalia uundwaji wa panton pale kigamboni,ujenzi wa majengo marefu na miradi ya madaraja na barabara za kilomita ndefu,zote wanafanya ngozi nyeupe na ndio wananufaika katika maslahi ya ujenzi sio mbongo.Sisi labda siasa ndio tuko fiti ila teknolojia vijana wa coet,dit na mist wakomae waje kuwa ma-TA maana ndio ajira ya uhakika nje ya hapo ni kula bench au kupiga dili za kitoto.
   
 4. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ngudu ndio mana tunasema serikali ilifanyie kazi hilo!! Mbona we unaonekana kama umeridhika na hiyo hali.
   
 5. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana DASA kwa huo ushuhuda. Yapo mengi tu mengine ni aibu kusema. Lakini tatizo sio walimu wetu, Tatizo kubwa ni namna ya kumuandaa huyu mwalimu, Na hili ni jukumu la vyuo husika na serikali kwa ujumla. Nchi za wenzetu ndivyo wanavyofanya. Dr. au Prof. akiingia darasani pamoja na kufundisha anatoa ushuhuda na picha mbalimbali kutokana na kazi na experience aliyoipata akiwa site au design office.
   
 6. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndugu nadhani huelewi linaloongelewa. Labda soma tena kwa makini.
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ni upuuzi kuwa mwalimu tena Engineering harafu hujui vitu kwenye industry/professional yako vinakwendaje. Cha msingi ni mhusika mwenyewe, taasisi husika na taifa wana wajibu wa kuhakikisha kunawekwa mazingira mazuri ya kuendeleza professional zao/za watu kwa manufaa ya nchi.

  TA anaajiliwa sawa, lakini scholarships za kumpeleka akasome ni shughuli pevu, vipindi/kazi anavyopewa pale COET huwezi kuamini kama kweli ni TA au ni manamba wa enzi za mkoloni. Tuna tatizo kwenye mfumo wetu wa elimu, siyo COET tu! chunguza utagundua afadhali hata hapo COET unapoona kuna walimu wako kiwango cha chini!!

  We need to tune some parameters in our education institutes so as we can be able to compete with others, Lakini kwa style hii bado hatuko tayari kushindana katika kila nyanja.
   
 8. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Sasa hzo kazi za consultancy huwa wanazifanyaje?
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kuuuuuuuuuuuuuuuuumbe, ndo maana ile sredi ya wadada engineer wabaya ilianzia kwa hawa watuuu! Ama kweli ndege wa rangi moja huruka pamoja. Aisee Big na DASA nataka kujenga kagorofa mshenzi unaweza kuja nisaidi seting ya kitako wakuu?
   
 10. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  swali la msingi sana ..
  Lakini hizi kazi nyingi nimeona zinafanywa na bico wengi ni dr na prof wa zamani
   
 11. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  kamanda umenena kwa kweli nimeshuhudia hii sana hapo coet mfumo wa elimu yetu huu tena wa madesa wa kwakweli kuna umuhimu mkubwa sana wa jamaa zetu wanaobaki kama mata wangepractise engineer atleast 3yrs halafu ndio warudi kushika chaki kwa kweli .
  Unajua baada ya chuo kustuka walikuwa hawajiiri mata wakaanza kubakiza mata kwa fujo sana sasa hili ni tatizo kubwa kweli hasa kwenye engineering field mimi i believe hata kama unataka kuwa lecturer mzuri in engineering pracise engineering is mandatory kwa kweli
  nawasilisha ...
   
 12. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  speaker sense sometime wewe ni great thinker right? Uwe unazungumza na fact acha ushabiki kama huna cha kuchangia kaa kimya
   
 13. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  inaonekana wewe walimu wako walipata shida kukielewesha kichwa chako maana nimetoa hoja na nimeweka na mifano(ushaidi) ila bado unaniandikia nitoe facts,tembelea sites ujionee miradi inafanywa na nani.
   
 14. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mjomba vipi, na we mhandisi tena setting inakushinda kweli!! Juzi tu umemaliza, au ulikimbia fani.
   
 15. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bico kweli ipo pale!! Lakini Je!! ina kazi!! na labda haiwashirikishi hao vijana!!. Kazi wanapeana wazoefu tu, ili wale pesa. maTA utakuta siku hizi ndio wanafundisha na kusahisha mitihani. Sasa pengine hapa napo kuna tatizo.
   
 16. Engager

  Engager JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  TA Siwezi kumwita Engineer hata siku moja.
   
 17. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  utake usitake sasa ndio hao wanaozalisha maengineer wa leo na wa kesho. Sasa wasaidiwe wawe maenginer wakweli. otherwise watatoa vituko.
   
 18. b

  bagain JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60

  umeongea jambo la muhimu sana kwa maendeleo ya elimu hapa nchini. Mimi ni mmoja wa wahitimu wa uhandisi wa chuo kimojawapo, kwa sababu wahadhiri wanakosa uwezo wa kivitendo matokeo yake huwa wanashindwa hata kusimamia ipasavyo projects za wanafunzi hasa finalists.

  Tatizo jingine ni kuwa vyuo vinakuwa na mitaala mizuri sana lakini haifuatwi, unakuta course inatakiwa kufanya laboratory works na ipo kwenye mtaala lakini mwisho wa siku hakuna kinachofanyika.

  Kwa kweli inauma pale unapomaliza degree level lakini ukweli umejaa theory tupu.
   
 19. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hao walimu kuna wakati huwa wanakuja kuwatembelea wanafunzi wakati wa field. Mwalimu anafika field na wengi ni hao vijana anashanga tu naye haelewi chochote, mwisho wa siku anauza sura anaondoka zake. Wakati mwingine hata hawaji.

  Wapo ambao ni wazuri, angalau walipata bahati ya kufanya kazi labda muda mfupi au walipata sehemu ya field nzuri. Lakini ukweli ni kwamba wanahitaji muda wa kutosha kushiriki kwenye projects mbalimbali ili waje kuwa walimu wazuri.

  Serikali itambue kwamba kwa level ya university mwanafunzi anaandaliwa kufanya kazi, sasa kama wanaowafundisha hawajawahi kufanya hizo kazi tutakuwa tunacheza makidamakida.

  Labda na suala lingine ni haya makampuni yaliyopo sababu ndio wanaoajili vijana wanapomaliza chuo, watuambie uwezo wa hao wanafunzi, na kama uwezo hawana wamechukua hatua gani. Sababu kuna makampuni mengi ambayo yamekuwa yakilalamika uwezo wa hao freshers lakini hawajaribu kusaidia kusolve hilo tatizo au kusaidia kutafuta kiini cha tatizo.

  Tukumbuke kazi za Engineering zinacheza sana na maisha ya watu. Tusipokuwa na maandalizi ya msingi kwa vijana wetu tutakuja kupata madhara makubwa sana huko baadae. Serikali iache kufikiria siasa za kila siku badala yake iinvest kwenye Elimu.
   
 20. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Yaani mimi nakubaliana na wewe mia kwa mia,kwa kweli experience inahusu,there is a lot to learn n relate with class,nina uhakika ukimuweka engineer wa civil aliyekaa field kwa miaka miwili na aliyetoka direct na kwenda masters utampa wa miaka miwili kazi c wa masters,kwa nini watu wanasoma masters?mi nadhani ina umuhmu ukishakaa kazini kidogo,
   
Loading...