Serikali: Changamoto ya utekelezaji wa bajeti ya 2017/2018 imetokana na kupungua kwa shughuli za uchimbaji wa madini

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Serikali imesema changamoto ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/2018 imetokana na kupungua kwa shughuli za uchimbaji wa madini kwa baadhi ya migodi na kupunguwa kwa wafanyakazi kwenye migodi hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ambapo amesema mpango wa maendeleo ya Taifa umeshindwa kutekelezeka kwani mwaka wa fedha 2019/2020 mishahara inakadiriwa kuwa ni shilingi trilioni 7.6 na kuongezeka hadi shilingi trilioni 8.42 kwa mwaka 2021/2022.

KwanzaHabari

Kumbukizi:
Kwenye kongamano la kupongeza Rais kwa miaka 3 alisema mapato yatokanayo na madini yamepaa kuliko wakati wowote ule toka nchi kupata uhuru. Ila leo wanaongea mengine
 
Serikali imesema changamoto ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/2018 imetokana na kupungua kwa shughuli za uchimbaji wa madini kwa baadhi ya migodi na kupunguwa kwa wafanyakazi kwenye migodi hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ambapo amesema mpango wa maendeleo ya Taifa umeshindwa kutekelezeka kwani mwaka wa fedha 2019/2020 mishahara inakadiriwa kuwa ni shilingi trilioni 7.6 na kuongezeka hadi shilingi trilioni 8.42 kwa mwaka 2021/2022. #KwanzaHabari
Mbona kama kuna majungu unataka kuandika ila kichwa cha habari kinakushinda?
 
Mimi kiwango changu cha kuelewa taarifa kam hizi kimeshuka kwa kwa miaka 3 sasa....hebu tupe ufafanuzi Mkuu !
 
Namba haziongopi watanyooka tu
Tatizo wanakurupuka bila kutafakari hao, mpaka nchi ianguke na ikae chini kitako ndio wataamka.

1) Walikurupuka kuwa vuruga wachimbaji madini, na walipewa onyo ila hawakusikia.

2) Walikamata mzigo wa almasi wa mgodi wa Mwadui/Shinyanga na kujisemesha kua wame UNDER-DECLARE VALUE ya huo mzigo, wakati jamaa hao walikua na form halali za valuation. Sasa hili sakata liliishia wapi??? Mbona kimya???

3) Walikamata contener za MAKINIKIA, na kusema vitu kibao. Sakata la makinikia nani anajua mwisho wake???

4) Walikamata viongozi wa migodi BULYANHULU/ACACIA na kuwasweka ndani kwa kigezo cha utakatishahi fedha na ukwepaji kodi USD 190 MILIION $ imeishiwa wapi??? Walisema tunalipwa mbona kimya???

5) Walikamata wafanya biashara wadogo wadogo wa machimbo/uuzaji wa madini nchini.

6) Walifungia lesseni kibao za uchimbaji madini nchini.

Yote haya, walitegemea uzalishaji utakua??? Utaleta faida kubwa kwa Taifa letu ambayo hawakutegemea??? Au utaongeza ajira kwa watanzania???

***Hii haihitaji mtu kua hata na CHETI CHA DARASA LA SABA kuelewa/kutambua madhara yake.
 
Serikali imesema changamoto ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/2018 imetokana na kupungua kwa shughuli za uchimbaji wa madini kwa baadhi ya migodi na kupunguwa kwa wafanyakazi kwenye migodi hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ambapo amesema mpango wa maendeleo ya Taifa umeshindwa kutekelezeka kwani mwaka wa fedha 2019/2020 mishahara inakadiriwa kuwa ni shilingi trilioni 7.6 na kuongezeka hadi shilingi trilioni 8.42 kwa mwaka 2021/2022. #KwanzaHabari
Asubiri kufukuzwa kazi na Jiwe aliyesema mapato yanaongezeka
 
Kokotoa Kokotoa ana bahati sana CAG sio yule mtata....mishahara ya wafanyakazi imeongezeka ilihali kuna maelfu ya wafanayakazi vyeti feki,hewa walipunguzwa hakuna walioajiriwa hakuna hakuna au ni hao ma bodyguard kutoka RWANDA.............. bado tutakokotoa tuu haku hakuna namna.. ushamba mzigo jamani nawaambia time will tell
 
Back
Top Bottom