Serikali awamu ya tano tafadhali tanueni barabara ya Nyuki-Bunju

Basi tufanye huku kuna wananchi wengi wanaoishi Mabwepande...wastaafu wengi hasa wa vyombo vya ulinzi wapo huku...mnadhimu nae yupo huku mradi wa nyumba za TBA na Watumishi Housing upo huku...viwanda lukuki kikiwemo cha Hill water na vya chuma vipo huku...mabasi ya mikoa ya Kaskazini asilimia karibia 60 yanapita huku...Bagamoyo tourist town barabara ndio hii...kipi kitazuia...kubwa zaidi huku tupo wapiga kura.
Hahaha labda nyie ni wananchi/ wapiga kura lakini siyo wanyonge.
Bunju B mradi wa bomba ulipita hapo wanaita bomba la mchina, lakini mpaka leo Bunju B hawana maji ya DAWASCO. Kulikuwa na mradi wa tanki la watu gani sijui walikuwa wanauza maji, Sasa hawapo na DAWASCO hawajapeleka maji. Lakini kwenye TV MKUMBO, na MBARAWA wanasema bunju maji yanatoka lakini sijui ni wapi?!.
Barabara ndio hata siongei ni mbovuuuu, lakini sio kipaumbele chao.
Walipo mnyang'anya Sumaye shamba nikajua sasa kikwazo kimeondolewa labda wangetengeneza barabara, lakini badoooo.
Hivyo nadhani wananchi siyo kipaumbele chao.
 
Hali ni mbaya foleni toka Boko Magengeni to Kibo Complex. Tunachoka jamani masaa 2 to Bunju toka Kibo. Halafu Gulio na Jumanne ni Kero liondolewe kwa kuwa linazuia magari kupita. Gari za mikoani na Malori na Daladala kupishana ni hatarishi
Kipande korofi sana kwa foleni hicho hasa nyakati za jioni. Nadhani malory yote yanayotoka mikoa ya kaskazini yanapita njia hiyo siku hizi badala ya Chalinze

Kuna ile njia inayotengenezwa na TANROADS ya kuingilia Kunduchi, Ununio, Mbweni hadi Kutokea Bunju Beach ingekamilika mapema nayo itasaidia kupunguza foleni

Lakini suluhisho la kudumu ni kutanua/kupanua kipande cha Tegeta hadi angalau Boko Magengeni
 
Asante kwa kunisupport. Serikali ianze na kuondoa Gulio/mnada la Jumanne. Walipeleke pale uwanja wa Chama au Dawasa. Foleni ni ndefu tena pameinuka , barabara ni nyembamba, Mabasi na Malori, private na waenda kwa miguu. Wanunuzi wanapaki magari njiani. Hapo unalala unaamka bado hujasogea.
 
Naunga hoja 100 kwa 100..
Kwa kweli Serikali ifanye mkakati wa dhati na wa haraka kutanua barabara hii..toka Tegeta mpaka Bunju...barabara imeshakuwa finyu sana
Wafanyakazi tunaokaa Bunju kufika mjini ni mbinde..foleni ni kubwa sana ..tunafika kazini tumechelewa.
Vile vile suala la kupitisha mabasi ya mikoa ya kaskazini njia hii..asubuhi ni heka heka
Tunashauri mamlaka husika pls hebu ingilieni kati haraka
 
Siku ya Jumanne hicho kipande kuanzia Boko Basihaya, Msikitini, Chama, California, Kwa Mpemba hadi Boko Magengeni ni balaa!
Sijui ilitumika logic gani kuweka ule mnada eneo lile pale Chama maana barabara ni nyembamba sana kama ulivyoelezea mkuu
 
Mataa ya kuongozea magari yamekua mengi hata mahali pasipostahili kuwekwa taa.

Makutano Mengi yalipaswa yawekwe round about
 
Yaani barabara hii nadhani ndio the most congested in Dar yaani shughuli kweli
Naunga hoja 100 kwa 100..
Kwa kweli Serikali ifanye mkakati wa dhati na wa haraka kutanua barabara hii..toka Tegeta mpaka Bunju...barabara imeshakuwa finyu sana
Wafanyakazi tunaokaa Bunju kufika mjini ni mbinde..foleni ni kubwa sana ..tunafika kazini tumechelewa.
Vile vile suala la kupitisha mabasi ya mikoa ya kaskazini njia hii..asubuhi ni heka heka
Tunashauri mamlaka husika pls hebu ingilieni kati haraka
 
Yaani hata haipaswi kuishia Boko inatakiwa ifike Bunju kabisa

Back
Top Bottom