Serikali awamu ya tano tafadhali tanueni barabara ya Nyuki-Bunju

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Kipande hiki ni kero kubwa sana kwa wananchi tunaoishi upande huu, kuna foleni kali sana majira ya asubuhi na jioni. Nafuu unakuja kuipata Tegeta nyuki inapoanzia 4 way.

Tafadhalini tutanulieni hiki kipande cha Bagamoyo Road Nyuki hadi Bunju 'B'. Ukanda huu una private cars nyingi sana kutokana na middle incomers wanaoishi Mbweni na Bunju yenyewe aidha watumiaji usafiri wa umma wanatumia masaa mengi sana kufika Mwenge.

Mathalani Bunju A hadi Mwenge Mataa ni kilomita 23 tu lakini unatumia hadi saa 3 kufika wakati wa asubuhi. Barabara hii itanuliwe ni moja miongoni mwa barabara kero hapa jijini Dar es Salaam.

Wasalaam.
 
Serikali imekusikia.

Kwa sasa unaweza kutumia njia ya Chama hadi Ununio - mtongani then unakunja pale polisi au unanyoosha hadi mbuyuni. Mbona fasta tu unaichungulia morocco!
 
Hiyo tunapita lakini nayo imeshakuwa congested asubuhi ni foleni mtindo mmoja naijua hiyo inayopita kwa Mwamunyange kule bado ina jam hatari asubuhi
Serikali imekusikia.

Kwa sasa unaweza kutumia njia ya Chama hadi Ununio - mtongani then unakunja pale polisi au unanyoosha hadi mbuyuni. Mbona fasta tu unaichungulia morocco!
 
Wananchi wa ukanda huo mlizinduliwa meri ya kuwabeba toka feri to Bagamoyo via masaki, msasani, kunduchi, Bunju, Chuo cha uvuvi na Bagamoyo hiyo ingewapunguzia kero so ombeni hilo dude lije.

Unapoomba phase 5 utasubili sana maana siyo kipaumbele kwa sasa, we've 5big deals kwanza.
 
Niliwai kudhani yale majumba yalijengwa kule mabwepande mradi wa watumishi housing yange chochea upanuaji wa kipande kilichobaki hadi bunju B, haikuwa hivyo. Sioni nini kitawashawishi serikali kuipanua barabara hiyo. Wananchi peke yao hawajawahi kuwa kishawishi kwa serikali kutekeleza mradi.
 
Nchi hii viongozi wajitahidi wawe na mipango endelevu!
Na kuhusu huyo ya bunju naona huo mpango upo ni kutanua Barabara kutoka nyuki hadi bunju

Ova

Ova
 
Lini kiongozi leo?....mimi mara nyingi napita chini sababu ya foleni...na pale ajali zinatokea sana ni kama ilivyo Boko Magengeni!
jumapili alfajiri mimi nilipita saa kumi na nusu aisee barabara ilikuwa ni midamu tupu na minyama..... lory lilikuwa linatokea bagamoyo limebeba kifusi , gari ya wale marehemu nadhani walitoka stareheni maana chupa za vinywaji vikali zilikuwepo ...... HAKIKA SIYO HADITHI NZURI.
 
Duuu itakuwa ni yule askari polisi wa bagamoyo, maana nae nasikia aligongwa na Lori mida hiyo hiyo.
 
Dah so sad imenikumbusha ajali ya bodaboda waliosangwa na lori boko magengeni wakati ule...hii barabara ni nyembamba kwa kweli waitanue
jumapili alfajiri mimi nilipita saa kumi na nusu aisee barabara ilikuwa ni midamu tupu na minyama..... lory lilikuwa linatokea bagamoyo limebeba kifusi , gari ya wale marehemu nadhani walitoka stareheni maana chupa za vinywaji vikali zilikuwepo ...... HAKIKA SIYO HADITHI NZURI.
 
Basi tufanye huku kuna wananchi wengi wanaoishi Mabwepande...wastaafu wengi hasa wa vyombo vya ulinzi wapo huku...mnadhimu nae yupo huku mradi wa nyumba za TBA na Watumishi Housing upo huku...viwanda lukuki kikiwemo cha Hill water na vya chuma vipo huku...mabasi ya mikoa ya Kaskazini asilimia karibia 60 yanapita huku...Bagamoyo tourist town barabara ndio hii...kipi kitazuia...kubwa zaidi huku tupo wapiga kura.
Niliwai kudhani yale majumba yalijengwa kule mabwepande mradi wa watumishi housing yange chochea upanuaji wa kipande kilichobaki hadi bunju B, haikuwa hivyo. Sioni nini kitawashawishi serikali kuipanua barabara hiyo. Wananchi peke yao hawajawahi kuwa kishawishi kwa serikali kutekeleza mradi.
 
Kipande hiki ni kero kubwa sana kwa wananchi tunaoishi upande huu, kuna foleni kali sana majira ya asubuhi na jioni. Nafuu unakuja kuipata Tegeta nyuki inapoanzia 4 way.

Tafadhalini tutanulieni hiki kipande cha Bagamoyo Road Nyuki hadi Bunju 'B'. Ukanda huu una private cars nyingi sana kutokana na middle incomers wanaoishi Mbweni na Bunju yenyewe aidha watumiaji usafiri wa umma wanatumia masaa mengi sana kufika Mwenge.

Mathalani Bunju A hadi Mwenge Mataa ni kilomita 23 tu lakini unatumia hadi saa 3 kufika wakati wa asubuhi. Barabara hii itanuliwe ni moja miongoni mwa barabara kero hapa jijini Dar es Salaam.

Wasalaam.
Foleni inatisha kuanzia Nyuki Tegeta hadi Bunju. Hatua zisipochukuliwa hasara ya muda na kiuchumi itatuumiza wengi. Kule private cars ni nyingi mno.
 
Back
Top Bottom