Serikali, acheni uhuni huu, ni kujitafutia laana

juve2012

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
3,339
2,000
Hii nchi watu wanapiga hela at the expenses of wananchi wa hali ya chini,ila maufisadi mengine ni kujitafutia laana tu.

Juzi ofisini alinijia mzee mmoja mstaafu wa jumuiya ya africa mashariki upande wa ttcl(alikuja kuniomba nauli),anasema hadi leo wanadai pensheni yao hawajalipwa.

Anasema serikali ilifanya uhuni wakalipwa pensheni kwa hesabu za mishahara ya zamani badala ya scale ya mshahara waliyostaafu nayo.

Wakapeleka kesi mahakamani,wakashinda,hivyo serikali ikaamriwa iwalipe.

Wakaambiwa watalipwa kwa awamu tatu(miaka mitatu) kuanzia last year.

Malipo ya mwaka jana wamelipwa mwaka huu robo tatu tu,hiyo robo iliyobaki hawajamaliziwa hadi leo.

Awamu ya pili ilikuwa walipwe mwezi uliopita,tena wameambiwa watapewa nusu tu(kumbuka ile robo ya mwaka jana bado hawajalipwa) lakini
juzi juzi hazina wamewaambia hakuna fedha za kuwalipa hadi liidhinishwe fungu lingine.

Pesa wanayodai haizidi bilioni 2!na hii ni halali yao kwa sababu ni jasho lao,wala haina mjadala.

Kilianzishwa kitengo kinaitwa "Simu 2000" ambacho kazi yake ilikuwa kuuza mali za ttcl ili kuwalipa wazee hawa.

Zikauzwa mali nyingi,sote tunajua,pale Ilala flats,hapa karibu na mawasiliano tower ,chuo kikuu,tena tunajua ambaye alichukua mali hizi nyingi ni mtu mmoja,na jamaa zake kutoka familia ya juu ya awamu iliyopita.

Walisema zimepatikana bilioni 15 kuwalipa hawa wazee,lakini watu wakachakachua mahesabu na kuwapunja wazee wa watu.

Wazee wakastuka,wametumia sheria kudai stahili zao,wameshinda.

Leo hii malipo wanalipwa nusu nusu,tena kwa kupigwa dana dana hivi.!

Wazee wa watu wamejichokea,hawana means za maisha,wanategemea hivyo vihela ambavyo hata wakivipata vitawasaidia kwa muda mfupi tu lakini bado wanavisotea hivi?!

Pesa za simu 2000 ziko wapi?
Kwa nini serikali iliua CHC wakati bado kuna issues hizi zilizokuwa zikienda vizuri chini ya kitengo hicho kuliko hazina?

Kuna mtu kapewa bilioni moja za escrow peke yake,tena zote kwa wakati mmoja,bila chenga,tena kama ziada tu,lakini wazee hawa wanadai billioni 2 iliyo jasho lao,wanasoteshwa kwa malipo nusu nusu yanayocheleweshwa hivi?

Wengine ni wagonjwa n.k
Mmewasumbua kudai haki mahakamani,wamesota miaka yote hadi mahakama imewatetea,halafu bado mnawasumbua hivi,MNATAKA WOTE WAFE,PESA ZAO MPELEKE WAPI?

Serikali acheni kutafuta laana,mmetuibia fedha escrow,bado na hawa wazee maskini wa Mungu mnawadhalilisha hivi?

Wana jf,hivi ukiwa kiongozi serikalini huwa roho ya kibinadamu inaondoka au?

Nauliza hivi manake kuna mambo nashindwa kuyaelewa jamani,dah!
 
ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,375

kusema watapata laana kunaonyesha kukata tamaa, na kwa taarifa yako laana the way unaidefine does not exists kama ingekuwepo wapo watu wamefanya ufisadi mwingi au wameonea watu sana wangekuwa wamekwisha katika viungo vyote lakini ndio wanazidi kutajirika. cha msingi ni kudai haki, ukinyimwa haki yako ndiyo laana yako hiyo na usidhani aliyekunyima ndiye anapata laana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom