Serikali acheni kulala tunachakachuliwa.

Tumaini edson

Member
Feb 1, 2011
54
0
Serikali ilitangaza kubinafsishwa kwa kiwanda cha nyuzi Tabora miaka kadhaa iliyopita, na kweli wakaja Wahindi ambao walionekana pale wakiendesha shughuli za uzalishaji. Kiwanda hiki kiliendelea kufanya kaz kwa kusua sua, hali iliyopelekea nyakati zingine wafanyakaz kusimamishwa kwa madai ya malighafi kupungua. Kiwanda hk kimekuwa na migogoro ya hapa na pale kat ya wahind na wafanyakaz juu ya mishahara na madai mbalmbali, hali iliyopelekea baadhi ya viongozi akiwemo aliyekuwa waziri wa kipindi hicho Mery Nagu, kuingilia kat kuwatetea waTanzania walokuwa wakinyanyaswa na hawa tunaowaitwa wawekezaji. Wahindi waliendelea kupoteza mwelekeo kiasi cha kupunguza karibu robo3 ya wafanyakaz wake. Sasa ktk hali isiyo ya kawaida, mwez november waliita baadh ya wafanyakaz tena kwa mbwembwe, wakiahidi kulipa mishahara minono na kwa wakati, eti kwa kuwa wanaboresha kiwanda kiwe cha ksasa zaidi. Ndg zangu, vjana walipoanza kazi walishangaa kuona wanafanya kazi tofauti na ile waliyokuwa wakiifanya awali, badala yake wakishinda wanafungua mashine zile na kuzipaki nje. Baada ya kama wiki 3 hivi yalianza kuja magari makubwa, yakiwa na watu walio tambulishwa kama wataalam toka Palestina, walianza kupakia na kusafirisha mashine mfululizo kwa mda kama wa mwez hivi na zaidi, ndipo siku moja alifika pale mkuu wa mkoa Abeid Mwinyi Musa, na kuuliza 'jamani nimestushwa, naambiwa kiwanda kinahamishwa kimya kimya?' wale wahindi wakishirikiana na waTanzania vibaraka wakajibu, "tunazipeleka kuzifanyia matengenezo". Ndg zangu, naomba wote tutafakari juu ya hatma ya mali za nch yetu, kwani taarifa za siri toka ndani ya kiwanda zinasema, Mashine ni kubwa sana 12 ambazo kulingana na ukubwa wake na uhaba wa pamba hazikuwah kufanya kazi toka upya wake, badala ziliishia kutumika mashine 8 tena kwa kupokezana. Viongozi wetu wamekalia majungu, Rais wetu kageuka Mbayuwayu kushinda angani 'MALI ZA WATANZANIA ZINABEBWA KAMA HAZNA WENYEWE.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom