Hercule Poirot
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 1,770
- 1,555
Mkuu shukuran at least wewe umekuja kujadili kuliko BAK yeye anatanguliza Profesa Lipumba kuwa ndiye suluhisho kana kwamba aloyasema ndio rasimu ya wananchi ama huyu ndiye mwenye majibu ya serikali ya 3 tukamuulize yeye. Mimi najua fika kwamba hadi sasa matumizi ya kugharamia serikali ya Muungano yanafanywa kwa asilimia kubwa na Tanganyika pengine zaidi ya asilimia 99. Na vyanzo vyake ni vile ambavyo vimo ktk mambo ya muungano na inafahamika sasa hivi kuwa JMT ni Tanganyika yenyewe hilo halina shida, hivyo mimi nimeyaweka matumizi ya JMT ya sasa hivi iwe kama Tanganyika lakini ile ya Muungano mpya wa serikali ya 3 itakayo undwa haitakuwa na vyanzo tofauti na serikali iliyopo. Hivyo kuna tofauti kubwa sana kusema leo hii gharama hizo zinatumikia serikali ya muungano ambayo ni Tanganyika, ila tutakapo unda hii ya 3 itategemea sana serikali za Tanganyika na Zanzibar kuchangia mfuko wa kuendesha serikali hiyo na hapo ndipo maswali yanapokuja.Ofcourse gharama itaongezeka ila haitaongezeka kama watu wanavyosema sababu mambo ya muungano sio mengi na sio kwamba sasa hivi hayafanyiki.
Pili tukitenga tutajua ni pesa ipi inakwenda wapi na inafanya nini (kuongeza accountability) na sio necessarily kwamba kodi zitaongezeka sababu kuna option ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima AKA kufuja pesa hence kufunga mikanda kwa hawa wasaka utawala na kama pesa itakuwa ndogo basi hiyo misafara, posho, mishahara n.k. ndio itabidi ipungue kwa hao viongozi, ambao nadhani hawalazimishwi wakiona Siasa hailipi tena basi warudi kufanya shughuli nyingine
Cha kujiuliza ni kwamba faida ya Serikali Tatu ni kubwa au ndogo kulinganisha na faida inayopatikana in so called kuepuka gharama wakati hilo punguzo linaishia kwenye matumbo ya watu wanaojificha kwenye hii confusion ya sasa ?
Sasa iweje serikali ambazo hazijitoshelezi leo kwa kuomba misaada ziweze kuihudumia serikali ya muungano ambayo haina mamlaka yoyote ktk vyanzo vya mapato ya serikali hizi isipokuwa wanategemea ushuru wa bidhaa zisizo za kodi jambo ambalo litaweza kuwepo ktk shirikisho la EAC? Lakini leo hii wategemee mchango wan chi ambazo zinategemea misaada kujiendesha zenyewe kutoa fungu lao ili kuchangia mfuko wa pamoja? Does it make sense kweli?
Mimi nachoomba ni darasa tu siko hapa kubishana isipokuwa kufahamishwa yale yalonikinza kichwani.
kama serikali ya Tanganyika ipo ni kwanini wazanzibar wanaajiriwa Tanganyika na hakuna mtanganyika anayeajiriwa serikali ya zanzibar? hatutaki mambo ya kivuli sijui mwamvuli, tunataka the government of Tanganyika. Rasimu ya warioba imeelezea kabisa idadi ya wabunge wa muungano na namna watavyopatikana.
kama serikali ya Tanganyika ipo ni kwanini wazanzibar wanaajiriwa Tanganyika na hakuna mtanganyika anayeajiriwa serikali ya zanzibar? hatutaki mambo ya kivuli sijui mwamvuli, tunataka the government of Tanganyika. Rasimu ya warioba imeelezea kabisa idadi ya wabunge wa muungano na namna watavyopatikana.
Sawa mathlan kutakuwa na wabunge 60, hawa wabunge watachaguliwa kwa vigezo gani na kazi yao haswa ni ipi? Je, ni kuwakilisha wananchi ama kuiwakilisha serikali ya Jamhuri maana ukiwa na wabunge sawa na wizara na idara za seriiali hiyo ina maana tutapoteza maana ya uchaguzi wa wabunge ambao huwakilsha wananchi na sio serikali. Na kama ni maana ya wananchi swali langu ni Je wabunge 60 wanatosha kutunga sheria za serikali ya muungano na sheria hizo zikakubaliwa nchi zote za Muungano? watasimamia vipi bajeti ya mambo ya maendeleo ya nchi zetu ikiw ani pamoja na mikataba! mtanisamehe kwa maswali haya maana najaribu kutazama mbele kuelewa tunachokifanya.Naona hapo juu umesema kwamba wabunge 600 jumla namba ambayo sidhani kama ni lazima iwe hio, inaweza ikawa pungufu (ukizingatia bado kutakuwa na Katiba ya Tanganyika ambayo huenda ikatuondolea mizigo minginge ya kufuja pesa kama wakuu wa wilaya) anyway according to Rasimu wabunge wa Jamuhuri watakuwa kama 60 ambao am sure kutokana na vitu vya muungano sio vingi na pesa itakuwa sio nyingi ya muungano hata vikao vyao havitakuwa vya muda mrefu na kuhusu Uongozi as far as I know just imagine sasa hivi huyu JK ndio angekuwa raisi wa Muungano (minus safari zake za kila siku sababu washirika wasingekubali asafiri hivi kwa kutumia pesa zao) Pinda angekuwa kiongozi wa Bara na Zanzibar wangekuwa na kiongozi wao (tuondokane na haya mambo ya Makamu wa Raisi na upuuzi kama huo).
Alafu unasahau hapa issue sio kwa upande wa Bara tu hata Zanzibar ambao kwa sasa wanaona Bara inawanyonya tukiwaridhisha kwa yote wanayoyataka ni dhahiri kwamba Bara watu wataanza kunungunika.., Kwahio kama kweli tunataka kuepuka gharama basi tufanye serikali moja..., kama haiwezekani basi ni tatu na kama hio ya Muungano itakosa pesa ya watu kujinafasi am sure kuna wazalendo ambao watakuwa tayari kuwa kiongozi wa hii serikali kama symbolic tu hata kama kutakuwa hakuna marupu rupu ya kutosha. Na kama Serikali 3 itakuwa ni njia ya Muungano kuvunjika hapo baadae and so be it....
Gharama ya serikali ya muungano kwa mujibu wa data kutoka hazina ni 1.8b.
Hao wabunge 60 ni according na TUME ila binafsi hata mimi naona hawa ni wengi sana ukizingatia mambo ya Muungano yapo 7 binafsi ningependa hii irekebishwe hii namba ipungue zaidi au watu wapewe kofia mbili yaani katika hao hao wabunge wa Zanzibar na Bara baadhi yao (lets say 7) wawe wanakaa kwenye vikao vya Muungano ambavyo navyo viwe vichache sioni faida ya kuwa na kila mwakilishi wa Muungano katika kila jimboSawa mathlan kutakuwa na wabunge 60, hawa wabunge watachaguliwa kwa vigezo gani na kazi yao haswa ni ipi? Je, ni kuwakilisha wananchi ama kuiwakilisha serikali ya Jamhuri maana ukiwa na wabunge sawa na wizara na idara za seriiali hiyo ina maana tutapoteza maana ya uchaguzi wa wabunge ambao huwakilsha wananchi na sio serikali. Na kama ni maana ya wananchi swali langu ni Je wabunge 60 wanatosha kutunga sheria za serikali ya muungano na sheria hizo zikakubaliwa nchi zote za Muungano? watasimamia vipi bajeti ya mambo ya maendeleo ya nchi zetu ikiw ani pamoja na mikataba! mtanisamehe kwa maswali haya maana najaribu kutazama mbele kuelewa tunachokifanya.
Mkuu hapa ndipo watu wengi hawaelewi ama wanachanganya madawa na hivyo kuleta mkanganyiko. Sababu kubwa ya kuitaka serikali ya 3 ni kuwezesha seriiali hizo zijue malaka yake na mipaka yake na sii kugawana mambo. Leo Hii Chikawa ni waziri wa mambo ya ndani ya serikali ya Jamhuri (mambo yaliyopo ktk Muungano) lakini amekuwa akiitumikia bara kutokana na madai kwamba tuna serikali 2 ndiyzo zilizosababisha. Sasa ili kusahihisha makosa kama haya ndipo swala la serikali 3 limejitokeza ili Tanganyika iwe na mkuu wake na Zanzibar iwe na mkuu wake chini ya serikali kuu inayoongozwa na Chikawa.Mkandara umesema sahihi mwanzoni - kisichokuwapo ni serikali ya muungano. Yaani mawaziri wote na Rais wao wanafanya mambo ya bara pamoja na kusemwa kuwa ni wa muungano. Kwa mfano Chikawe - Waziri wa Mambo ya Ndani - ni waziri wa muungano - lkn kila mara anashughulika na mambo ya bara tu! Sawa kabisa nami nakubali. Sasa huoni kuwa wanaopendekeza serekali tatu wanataka ufanisi zaidi kwa mambo ya muungano? Ili Chikawe akiwa waziri wa muungano asijisahau na kufanya ya bara tu huku kavaa kofia ya muungano.
Kuhusu gharama. Nilimsikiliza vizuri Awadh Said mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Warioba. Anasema walichopendekeza ni kumweka Chikawe wazi - Waziri katika serikali ya muungano anayeshughulikia mambo ya ndani. Anahama toka serikali ya sasa hivi - ya bara na muungano- kwenda kwenye serikali ya muungano pekee. Kumbuka bara hawatakuwa na wizara ya mambo ya ndani. Gharama gani zinaongezeka hapo?
Kwani tunauunganisha kila kitu? Nijuavyo mimi tunaunganisha baadhi tu ya mambo na ndivyo walivyokubaliana waasisi. Hatuunganishi kilimo na ufugaji, hatuunganishi tawala za mikoa na serikali za mitaa, hatuunganishi rasilimali nk. Tunaunganisha ulinzi na usalama, tunaunganisha mambo ya nje. Yale mambo ambayo huunganishi yatashughulikiwa na serikali washirika. Yale tunayounganisha yatashughulikiwa na serikali ya muungano. Ugumu unatoka wapi? Kwanini unanga'ng'ania serikali ya Tanganyika iwe na Wizara za muungano pia? Kwa nini leo hii Zanzibar haina Membe wao? Mimi nadhani tunachamba mno na matokeo yake ndiyo haya.Mkuu hapa ndipo watu wengi hawaelewi ama wanachanganya madawa na hivyo kuleta mkanganyiko. Sababu kubwa ya kuitaka serikali ya 3 ni kuwezesha seriiali hizo zijue malaka yake na mipaka yake na sii kugawana mambo. Leo Hii Chikawa ni waziri wa mambo ya ndani ya serikali ya Jamhuri (mambo yaliyopo ktk Muungano) lakini amekuwa akiitumikia bara kutokana na madai kwamba tuna serikali 2 ndiyzo zilizosababisha. Sasa ili kusahihisha makosa kama haya ndipo swala la serikali 3 limejitokeza ili Tanganyika iwe na mkuu wake na Zanzibar iwe na mkuu wake chini ya serikali kuu inayoongozwa na Chikawa.
Hivyo ni lazima Tanganyika nayo iwe na wizara yake ya mambo ya ndani ambayo kisheria haitakiuka sheria mama yaani katiba ya Muungano. Kifupi Chikawa atakuwa kama kiongozi wa FBI kwa nchi ya Marekani yaani kwa mambo yaliyo juu ya sheria za nchi husika japo kila nchi ina mku wake na hutekeleza majukumu yake kulingana na sheria za hapo, tena badi kila Mji una polisi yake na mamlaa yake polisi wa Mwanza haweza kuwa na mamlaka Kilimanjaro unless amehamishiwa huko ila Polisi wa taifa anaweza kufanya kazi yake mahala popote na wakati wowote wanaingia sehemu yoyote within mipaka yetu..
Hivyo, maelezo ya Awadh Said ni ya kupotosha zaidi kwa sababu huwezi kuonyesha Chikawa awe wa Muungano ambavyo ndivyo tulivyo ukaiacha Tanganyika haina mambo ya ndani ni yale yale ya serikali 2, ni sawa na tummetoa mfuko mmoja wa suruali na kumweka mfuko mwingine na kuuacha mfuko ule wazi hauna kitu. Kuna tofauti kubwa kati ya kugawna malamaka na kugawana mambo mana unaweza kuwa na mambo yote lakini mamlaka yake yakashuka hadi serikali za mitaa haina maana tumegawana mambo ya Utanganyika au Uzanzibar, ila shughuli zetu ndizo zinaweza kuwa ktk makundi ya mipaka na maeneo.
Kifupi tu ni kwamba muundo huu wa serikali 3 uloainishwa na rasimu hauwezi kutekelezeka ipaswavyo kwa sababu tumegawa mamlaka hayo kwa nchi ndogo na tukaiacha serikali kubwa bila meno maana hata ukichukuliasheria mama ya kuwaendeleza na kuwanufaisha wakulima/ wavuvi na wafugaji wakati haya sii mambo ya muungano, serikali kuu itaweza vipi kusimamia shughuli zao iwe hata kutoa mafao (subsidies) kwa walengwa ilihali sii kazi yao?. Zaidi ya hapo hili swala la kuunda sera ya Kitaifa kama lengo kuu ni kuwanufaisha kundi la watu ili kuwainua ni swala la vyama vya siasa kiitikadi. Chama ndicho kinaweza kuweka malengo hayo kama dira yao pindi wakishika uongozi na vyama vingine vikawapa kipaumbele Wawekezaji na Wajasiriamali ama hata Matajiri maadam malengo hayo wananchi wengi watayachagua.
Mimi sii mwanasiasa lakini kwa jinsi navyoliona swala hili linavyokwenda na ujadiliwa naona kama tunazidi kupotoshwa zaidi. Serikali kuu yenye mambo 7 haiwezi kabisa kuwa na nguvu juu ya serikali ndogo wala kuendesha Jeshi letu lenye matumizi makubwa kuliko wizara zote ukizingatia siasa za leo na mahitaji yake.
Mkuu nakuomba sana unisome kwa taratibu upate kunielewa. Sing'ang'anii kitu chochote ila hunielewi tu. Kila jambo na wakati wake mkuu wangu hakuna nchi serikali kuu na hasa chombo kama TRA hawana mamlaka ya kodi ya wananchi wake ila nchi washirika ndiyo mambo yao! na kodi zetu zipo katika kila jambo hivyo umuhimu wa serikali kuu kuwa ni yake pia upo. Hii habari ya mfuko wa pamoja sijui nchi zichangie mfuko wa hazina inatisha!Kwani tunauunganisha kila kitu? Nijuavyo mimi tunaunganisha baadhi tu ya mambo na ndivyo walivyokubaliana waasisi. Hatuunganishi kilimo na ufugaji, hatuunganishi tawala za mikoa na serikali za mitaa, hatuunganishi rasilimali nk. Tunaunganisha ulinzi na usalama, tunaunganisha mambo ya nje. Yale mambo ambayo huunganishi yatashughulikiwa na serikali washirika. Yale tunayounganisha yatashughulikiwa na serikali ya muungano. Ugumu unatoka wapi? Kwanini unanga'ng'ania serikali ya Tanganyika iwe na Wizara za muungano pia? Kwa nini leo hii Zanzibar haina Membe wao? Mimi nadhani tunachamba mno na matokeo yake ndiyo haya.