Series 5 za kikorea ambazo mastaa (Protagonist) walikufa

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Juzi juzi hapa nilikuwa naangalia series ya MOUSE starring LEE SEUNGGI moja ya vitu vilivyonishangaza kwenye series ile ni jambazi kuu Doctor Han Seo Joon kukamatwa na kuwekwa ndani kwenye episode ya kwanza.

Sasa nikajiuliza kama main villain amekamatwa kwenye wpisode 1 huku mbele kuna nini? Series si ishaisha?

Yes! Korean dramas zinakuwaga na plot zisizotabirika yaani starring mnayesema hauwawi atakufa na jambazi ataishi ukiangalia series ya SKY CASTLE utaona kuwa Protagonist Kim Hye Na anafariki alafu Kwak Min Hyang na Coach Kim wanabaki hai. It is what it is.

Kwa kuona hivyo hizi ni series tano ambazo protagonist au lead actors walikuja kufa kwenye mwisho wa series.

5. FASHION KING

Seriea hii ilirushwa na kituo cha SBS mwaka 2012 kuanzia Machi 10 mpaka May 22.

Series hii ilikolea sana kutokana na kuwa stori ya tofauti na uigizaji makini wa YOOH AH IN aliyeigiza kama Kang Young Gul aliyeanza biashara ya kuuza nguo sokoni hadi kuwa na kampuni kubwa na SHIN SE KYUNG aliyeigiza kama Lee Ga Young mwanadada mwenye kipaji cha designing.

.
Of course tulitegemea kwenye series hii GA YOUNG na YOUNG GUL wangeishia pamoja lakini series inaisha kwenye episode ya 20, Young Gul anajipiga risasi kichwani na kujiua. So sad!

4. CITY HUNTER.

Hii wengi tunaifahamu. Series ya 2011 na iliweza kumtambulisha vyema Lee Min Ho. Kituo cha SBS kilirusha series hii kuanzia May 25 mpaka July 28.

Kwa mara nyingine tena pamoja na Lee Min Ho aliyeigiza kama Lee Yoon Sung kutaka kulipa kisasi kwa wale mawaziri waliomuua baba yake mzazi aliyekuwa mwanajeshi, mwisho kabisa wa series hii Lee Min Ho alimiminiwa risasi nyingi tu walinzi wa Rais kisha kufariki.

Ilikuwa ni scene iliyohuzunisha sana na watu wengi walihoji kuwa kulikuwa na umuhimu gani Lee Kufa kwenye series hiyo angeachwa tu aenjoy na Kim Nana

3. IRIS 2.

Iris ya 2 starring Jang Hyuk muendelezo wa Iris ya kwanza ambapo series hii ilirushwa mwaka 2013 na kituo cha KBS2 kuanzia February 13 mpaka April 18.

Series hii tangu mwanzo ilionesha kabisa kuwa steringi mwishoni angekufa tu maana Jung YooGun alikuwa na tatizo la kichwa kuuma lakini sisi kama watazamaji tulijipa moyo kuwa hatofariki.

Lakini Director Kim Tae Hoon na Pyo Min Soo walituvunja moyo baada ya Yoo Gun ambaye ndiye Protagonist kwenye series hii kufariki kwenye episode ya mwisho baada ya kubeba bomu la nyuklia kwenye gari kuelekea kwenye bahari ili aweze kuokoa nchi yake.

2. EMPEROR OF THE SEA.
Series hii ilirushwa na kituo cha KBS mwaka 2004 na nadhani nikitaja Jang Bogo basi utakuwa ushaikumbuka series hii ambayo kwa hapa Tanzania ilioneshwa na ITV pamoja na Capital TV.

Basi bwana pamoja na plot kunoga sana ambapo Jang Bogo aliyetokea kwenye hali duni mpaka kuwa mfanya biashara mkubwa kwenye ufalme wa Silla mwisho wa siku alifariki na hivyo kufanya watazamaji kuhuzunika sana

1. IRIS : THE ORIGINAL

Series iliyomhusisha Lee Byung Hun na Kim Tae Hee waigizaji wakubwa kutokea South Korea, of course plot yake ilisifiwa sana sana na watazamaji lakini mwisho wake ulimhuzunisha kila mtu.

Humu kuna uzi niliuweka ukionesha taarifa kumi muhimu kuhusu series hii.

Sasa kwenye scene ya mwisho kabisa ya series hii Kim Hyeonjun alipigwa risasi na Agent Ray kutoka IRIS na kupoteza
maisha.
Sad as it is.

Je kuna series nyingine ya kikorea unaijua na starring alifariki?
2ffcaf7479ebabe6f29b54a81bbff274.jpg
IRIS-2-02.jpg
IRIS_Korean_Drama__18122010025332.jpg
1daae35717756cc4be5cb47706c32a5c.jpg
City-Hunter2011-Season-1-Complete-480p-720p-All-Episodes.jpg
 
Korea Kusini ndiyo nchi inayoongoza kwa wanaume kutumia vipodozi yaani (Make-Up)
Yaaani nawaangaliaga hawa machalii na uhusika wanaouvaa naseme hiiiiiiiii.
Japo kuna filamu zao huwa nazipenda zinafikia kiwango cha Hollywood.
 
Bro ukiangalia hizo series zote kuna sbabu maalum ya hao wote kufa,

Fashion King...Yoo Ah In alikua kijana alie hustle mno lakn baada ya kupata mafanikio aliwaz sana kulipa kisasi kwa waliomfanyia mabay kwa kusahau kua hao ndio walimjenga mpka yy kua hapo.Hyo ikapelekea akapoteza kila kitu hadi mpenzi waliekua wanapendana sana na kilichobaki kwake ilikua ni majuto.Akaamua kuliko kuiah na regrets bora afe.

IRIS 2
Baada ya Jang Hyuk kupigwa risasi ya kichwa akatibiwa na IRIS then akarudi NSS kama unakumbuka vizur yule mzee mwanasayansi alisema kwa jins risas ilivyokaa kichwa mwamba ni ngum sana kupon.Sasa ukiona pale scene ya mwisho bom lilishakua activated kulikua hakuna namna ya kulitegua zaidi y mtu ku sacrifice na kwakua jang hyuk alijua hana muda mrefu wa kuishi ilibidi tu afanye vile

CITY HUNTER
Kaangalie vizur Lee Min Ho hakufa aliekufa ni baba yake ,scene ya mwsho kabisa kweny movie ni yKe n Kim nana wakiwa darajani.

Alafu kwny Mouse the real Villian walikua ni wale watoto wawili waliokua na DNA za pschopath ambapo mmoja wao alikua mtoto wa doctor ambae ni lee seung gi.Mouse imeisha jana cjaangali hadi mwisho ila Lee seung gi kaua watu weng mno,the guy is the real villian na ndio mtoto wa doctor

All in all huo ni mtazamo wangu bro pMoja sana
 
Umeiweka vizuri sana una facts.

Asante kwa ufafanuzi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom