Kwa wapenzi wa simu za Samsung Galaxy A series, ngoja leo tujuzane kitu kidogo

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
26,136
75,208
Wakuu!

Samsung Galaxy A series ni smartphone kutoka Samsung ambazo zipo za aina mbalimbali kuanzia low end (izi ni za bei ndogo na specifications za chini) hadi za mid rangers ambazo zina specifications kubwa chini kidooogo ya Note Series, S series na Z Series.

Sasa ukiwa unataka kununua Samsung Galaxy A series, ukiona imeandikwa mfano: Galaxy A53 namba za muhimu kuangalia hapo ni iyo ya mwisho (kwenye mfano wetu ni namba 3) kwani ndio inaonesha mwaka wa toleo la iyo simu.

Mtiririko uko hivi:

2020 Samsung Galaxy Ax1
2021 Samsung Galaxy Ax2
2022 Samsung Galaxy Ax3
2023 Samsung Galaxy Ax4
2024 Samsung Galaxy Ax5
2025 Samsung Galaxy Ax6

Kwahiyo mfano Galaxy A53 ni simu ya mwaka 2022.

Namba ya kwanza kwa mfano iyo 5 inavyozidi kua kubwa ndio simu inakua na specifications kubwa zaidi.

Kwa mfano Galaxy A73 (hii pichani)

Samsung_Galaxy_A73_5G_(09-11-2022).jpg
ina nguvu zaidi ya A53 ingawa zote ni za mwaka mmoja.
Galaxy-A53-5G_03.jpg


Weekend njema!
 
Back
Top Bottom