Serekali na shule za kata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serekali na shule za kata

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by oldekenya, Apr 10, 2012.

 1. o

  oldekenya New Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wadau wa Jamii Forum na wasii katika blog hii tukumbushe serikali yetu kuwa kuna haja yakutupia macho shule za kata Tanzania kwani shule hizi zinaongoza kwa kufelisha wanafunzi na hata kukatisha tamaa wazazi wasikiapo wanao wamefaulu na kupangwa shule za kata. Wanaamini wanapoteza fedha zao pasipo na mafanikio na kupoteza muda wao kwani sikozote wanashuhudia wanao maliza ktk shule hizo hurudi na kukaa kijijini na badala yake kumkuta yule ambaye akwenda kabisa amempiga atu kimaendeleo kwa upande wa uzalishaji kama kilimo, ufugaji na kazalika. Lakini hawa ambao wanatoka mashuleni pasipo na mafanikio nao wanakua niwepesi sana kujiingiza katika matendo maovu kama ulevi, bangi na hata mambo mengine ambayo ayafai katika jamii kwa imani ya kwamba wamepoteza ramani.

  Mataizo yanayokabili shule nyingi za kata:-
  1. Upungufu mkubwa wa waalimu
  2. Uhaba mkubwa wa vitabu vya kiada na dhiada
  3. Kukosekana kwa umeme na badala yake wanafunzi 300 karabai 2 kweli!
  4. Hakuna miundo mbinu ya maji
  Sasa kwa taarifa yenu shule sio kusimamisha majengo tu imekwisha, ila shule nikile kinachopatikana na kutolewa kama elimu ndo maana ya shule sasa kama wangeimiza ktk kununua vitabu na vifaa vya mahabara na kupunguza idadi ya majengo tungeona matunda kwa namna moja ama nyingine ktk shule hizi lakini badala yake kila mwaka tunavuna sifuri

  Niombe serikali itumie siasa ktk kupata vifaa vya maabara, vifaa vya kufundishia, vitabu na nyenzo zingine kama ambavyo ilitumia siasa katika kujenga majengo shule hizo
   
Loading...