Sera za Chadema kuhusu wazee ni hizi hapa wadau mwasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera za Chadema kuhusu wazee ni hizi hapa wadau mwasemaje?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kaa la Moto, Oct 2, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tudodose sera za vyama,

  Watu wengi wamekuwa wakizungumzia Chadema kama chama kinachojali elimu na afya tu maana hayo ndiyo chama cha sisi m wameshikia bango.

  Nimegundua kuwa Chadema imewaangalia hata wazee wa nchi hii na kuwajali sana.

  Hapa chini sera hii inawahusu wazee wa nchi hii kama Chadema itapewa ridhaa.

  "7.2.2 Kuhusu mfumo wa pensheni na huduma kwa wazee
  Mfumo wetu wa ulipaji wa pension nchini una mapungufu mengi sana . Baadhi ya mapungufu haya ni ; idadi ndogo ya Watanzania ambao wameandikishwa katika mifuko ya hifadhi jamii , mafao duni kwa walengwa, tofauti kubwa ya mafao kwa makudi
  63
  mbalimbaliya wastaafu na hivyo kujenga matabaka, kutoratibiwa kwa mfumo mzima na hivyo kuruhusu kila mfuko kufanya kila unachoamua na kutowashirikisha kikamilifu na kuwanyima mamlaka ya kutoa maamuzi wachangiaji katika mifuko hiyo.
  Ili kuboresha mfumo wa pensheni kwa wazee, Serikali ya CHADEMA inakusudia kufanya yafuatayo:
  a) Kuboresha mfumo wa utoaji pension (contributory pension) kwa :
  1. Kuanzisha utaratibu utakaowawezesha wachangiaji katika mifuko hii kuwa na sauti katika uendeshaji wa mifuko husika kwa kuteua wawakilishi katika bodi zinazosimamia mifuko hiyo
  2. Kuimarisha uratibu na usimamizi wa mifuko hii na utoaji wa pensheni nchini na kuwa na mafao bora na yanayowiana.
  3. Kupanua wigo wa mifuko hii kwa kusajiri wafanyakazi /watu wengi katika sekta binafsi.
  b) Kuanzisha pension jamii kwa wazee wote (universal social pension )
  Kuna wazee takribani 2.1 milion katika nchi yetu. Asilimia 82 ya wazee wote nchini wanaishi vijijini. Mpaka sasa ni asilimia 4 ya wazee wote nchini wanaopata pensheni. Wazee hawa ni wale ambao walikuwa wameajiriwa katika ajira rasmi. Mbili ya tatu ya wapatao pensheni kwa sasa ni wanaume. Asilimia 96 ya wazee wote kwa sasa ( wengi wao wakiwa ni wakulima na wafugaji hawana pensheni ingawa nao wamechangia kwa kiasi kukubwa kulijenga taifa letu. Takribani asilimia 30% ya walemavu wote ni wazee. Takwimu zinaonyesha kuwa kaya zilizo na wazee (ambazo ni karibia robo ya kaya zote nchini) ni maskini sana. Kiwango chao cha umaskini katika kaya hizi kiko juu kwa asilimia 22.4, ukilinganisha na wastani wa umaskini wa taifa ( 40.9 %) ukilinganishwa na asilimia 33.4 ambayo ni wastani wa taifa.
  Wezee hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kuwatunza asilimia 50 ya watoto yatima nchini katika kipindi ambacho wao wenyewe wanahitaji kutunzwa, kushindwa kupata mahitaji muhimu kama chakula cha kwao na wategemezi wao,
  64
  kushindwa kupata huduma za afya bure kama ilivyokubaliwa na serikali, kuuawa kwa tuhuma za uchawi. Inakadiriwa kuwa zaidi ya wazee 300 wanauawa kila mwaka kwa tuhuma za uchawi.
  Umaskini uliokithiri kwa wazee wengi unawafanya kushindwa kuzifikia huduma muhimu ambazo zinatolewa na serikali kwa ajiri ya makundi maskini. Mfano wazee kukosa nauli ya kusafiri kufika hospitali hata kama huduma hospitali zinatakiwa kutolewa bure, watoto wanaolelewa na wazee kutoweza kusoma vizuri kwa kukosa mahitaji muhimu kama vile chakula, sare , vitabu , nauli kwenda shuleni nk- hata kama serikali imeondoa karo katika shule za masingi, kushindwa kujipatia hata pembejeo ambayo tayari imewekewa ruzuku na serikali kwa vile hawawezi kulipia kiwango wanachotakiwa kuchangia, na kushindwa kujiunga na SACCOS kwa vile hawawezi kulipia mchango wa awali . Moja ya motokeo yaliyo dhahili ni wazee kuwa ombaomba mitaani wengi wao wakiongozwa na wajukuu wao. Wazee kukosa wawakilishi waliowachagua wao katika vyombo vya maamuzi kama serikali za vijiji, kata, halmashauri na bunge kama walivyo wanawake, na sera ya taifa ya wazee (2003) kutotungiwa sheria imechangia kwa kiasi kikubwa kudidimia kwa maisha ya wazee.
  Kwa kutambua ukweli huu na kwa kuzingatia kwamba katiba ya nchi ibara ya 11( i) inatambua haki ya kila mtu kupata hifadhi ya jamii wakati wa uzee CHADEMA unakusudia kufanya yafuatayo:
  i) kuazisha mfumo wa utoaji pension kwa wazee wote (non contributory- universal social pension ) Malipo ya pensheni ( universal social pension) yatatolewa na serikali kwa kila raia wa nchi hii ambaye atakuwa amefikia umri wa kuitwa mzee (miaka 60) kwa mujibu wa sera ya taifa ya wazee . Ili kugharimia mfuko huu taifa litatenga kiasi kisichopungua asilimia 1 ya GDP kila mwaka kwa ajiri ya mfuko huu. Matokeo ya utafiti wa hivi karibuni unaonyesha ( A study into the feasibility of a universal social pension May 2010) kuwa utoaji wa pension kwa wazee wote utachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza umaskini kwa wazee na wategemezi wao wakiwamo nusu ya yatima wote hapa nchini. Hivyo basi, Serikali ya CHADEMA itatenga fedha katika bajeti ya 2011/2012 ili kutoa kiwango cha Tsh 15,000/= kwa mwezi kwa kila mzee (mtu yeyote mwenye umri wa miaka 60 na kuendelea). Kiwango hiki kitafanyiwa mapitio kipindi kwa kipindi. Hatua hii itapunguza umaskini miongoni mwa wazee kwa asilimia 57.9. Zaidi ya yote, mfumo wa pensheni kwa wazee wote itanufaisha takribani asilimia 25 ya kaya zote nchini ( robo ya Watanzania) na hivyo kupunguza wastani wa kiwango cha umaskini cha taifa kwa asilimia 11.9% ( (kutoka 33.4% - 29.4% cha sasa).

  ii) Serikali ya CHADEMA pia itatunga sheria itakayowawezesha utoaji wa matibabu bure kwa wazee wote . Katika kutekelezeka bila usumbufu wowote, na kuwaruhusu wazee kuwa na mwakilishi angalau mmoja waliomchagua wao katika vyombo vya maamuzi (serikali za kijiji, kata, halmashauri na bunge) ili mawazo yao yapate kuwakilishwa kwa ukamilifu wakati wote.

  iii) Serikali itapitia upya sera ya taifa ya wazee na kuiboresha na kuitungia kanuni zitakazosaidia utekelezaji wake .
  iv) Juhudi mahususi zitafanyika kudhibiti mauaji ya wazee na kuagiza vyombo husika kufanya uchunguzi wa kesi za mauaji zilizopo kwa haraka na kukamiliha kesi zilizoko mahakamani.
  "

  Hapa sera ya sisi m kuhusu wazee inasemaje?
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Nimeelezea kupinga kwangu hii nanny welfare state wanayotaka kuileta CHADEMA hapa

  Angalia kuhusu hili hususan paragraph ya 15 nilipoongelea mifumo kama hii inavyopata matatizo hata katika nchi tajiri, na ni nchi za aina gani Africa zimeweza kuweka mifumo hii etc.
   
 3. M

  Masauni JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani wewe uelewi vizuri. Nchi mojawapo iliyoweza ni Namibia.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Asante, mwenye swali aulize!
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Takwimu zinaonyesha kuwa kaya zilizo na wazee (ambazo ni karibia robo ya kaya zote nchini) ni maskini sana. Kiwango chao cha umaskini katika kaya hizi kiko juu kwa asilimia 22.4, ukilinganisha na wastani wa umaskini wa taifa ( 40.9 %) ukilinganishwa na asilimia 33.4 ambayo ni wastani wa taifa
  Maelezo hayajajitosheleza hapa, asilimia hizi kama hazina uwiano au hesabu iliyotumika haiko wazi kwenye maelezo. Tunaomba ufafanuzi.


  asilimia 50 ya watoto yatima
  Asilimia 50 ya watoto yatima ni watoto wangapi? Can Chadema please quantify this?

  1% ya GDP kwa ajili ya pensheni
  Chadema inatarajia GDP kuwa kiasi gani na ni tofauti kwa kiasi gani na GDP ya sasa?
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Kwenye hiyo link nimeelezea kuhusu si Namibia tu, bali pia Botswana na Mauritius nchi pekee za Africa zenye mfumo kama huu (pamoja na figures zao za GDP PPP na populations, kulinganisha na Tanzania) na sababu iliyofanya wao waweze ambayo itaweza kututatiza sisi.

  Jaribu kusoma kuelewa na kujadili kwanza kabla kusema wengine hawajaelewa.
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mchukia fisadi

  mbona umetuacha tuna hang na masuala kibao bila majibu?

  btw.......hii ni direct quote kutoka electronic manifesto ya chadema au umeongeza na kupunguza lako?

  manake makosa katika matumizi ya lugha ya kiswahili na matumizi yasiyokuwa sahihi ya kanuni za uandishi inanipa shaka.
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Gaijin hii ni direct quote kutoka manifesto. Hayo makosa ni kitu cha kawaida wala hayaondoi maudhui ya kilicho katika maandishi. Hata sisi m wanayo makosa kama haya ambayo hayaondoi malengo yao.

  Jadili tu yale ya maana kama ulivyofanya kwenye post #5 na subiri uletewe majibu kama kuna wa kukujibu, usipindishe mjadala.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli

  makosa ya kuto tumia lugha ya taifa kisahihi si madogo kama unavyofikiria.........ila ili kuachana na kupindisha mjadala (as if i will want that), naomba tu unijibu niliyoyauliza kwenye post #5.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  CCM kwao wazee ni kuwapiga virungu wakiandamana kudai haki zao.
  Na ndo maana wengi wanakwapua mari bse wanajua uzeeni hakuna ela kama wasipokwapua now
   
Loading...