ostrichegg
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 12,052
- 6,197
Unazungumzia ujamaa unaohubiriwa na bepari
Ubepari una practice uJamaa kwa kiwango kikubwa sana kwani asiye Nacho anahudumiwa na aliye nacho . Unajua tabia Ya binadamu akitoka Kwenye njaa iliyopitiliza akipewa chakula huwa ana tabia Ya kula kupitia uwezo wake hii ni tabia tuliyo nayo waafrika wengi . Wanaopata nafasi Mara nyingi back ground zao ni ufukara tuu sasa ile nafasi walionayo wanatamani wanyakue kila kilicho ndani Ya upeo wa macho yao. Sisi sasa tumekuwa mabepari kuliko mabepari orijino
day dream
Con chama chenye dhamira ya kweli ya kuikomboa Tz yetu!!cha msingi ni kila mtanzania ajue n vp atajikwamua aweke tonge mdomoni!!N mtazamo wangu tuu!!
Unazungumzia ujamaa unaohubiriwa na bepari
Sera ya ujamaa haiwezi kutekelezeka karne hii.
ACT mafisadi. Aeleze 10 mil alizochotewa na mafisadi
That's true mkuu . Hata mimi huwa nawaza ACT akiibeba ujamaa kama ilivyo hawezi kufanikiwa na atapata upinzani wa Hali ya juu. Nadhani ujamaa anaoumaanisha si wa enzi ziwe kwani mashani hata dunia haiwezi kumkubali . Nadhani ujamaa anaosema ACT ni ule uliobeba elements zile ulizozisema Kwani hata mabepari tu wa sasa watamwanzishia vita. So ACT kwa mtazamo wangu angefanya kazi Ya ziada kuelezea umma modern ujamaa anaosema ni upi tofauti na ule wa kunyang'anyana mali.Ninaona point yako lakini tukubali pia kuwa matatizo yanayojitokeza si ya mfumo wa uchumi bali mapungufu kama efficiency, cost-effectiveness, financial discipline, strategic management and control, planning na social responsibility. Bila kushughulika na hayo tutabaki hapa hapa tulipo!!!
Ningependa ACT atilie mkazo katika niliyotaja hapo juu badala ya mfumo wa kijamaa. Hivi kweli anataka kusema Azimio la Arusha kufilisi mali za watu ilikuwa ni jambo sahihi?? Wachukue shule binafsi ili kutoa elimu kwa umma bure halafu ziwashinde kuendesha?? Kwani hatuwezi kutoa huduma kwa jamii bila kufanya wealth redistribution?? Kwanini watu wote walazimike kuwa na utajiri unaowiana wakati watu wenyewe wana hulka, tabia na uwezo tofauti??
Ujamaa ni nini?
Mimi niko vijijini sijawaona au ni vijiji vya mwandiga?.
Magesa Mwita
UNGANA NAMI KATIKA IMANI YA UJAMAA WA
KIDEMOKRASIA YA ACT-WAZALENDO
SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI
ACT-Wazalendo imejengwa kwenye IMANI, imani
ya Ujamaa wa Kidemokrasia. Imani tu haitoshi,
bali inahitaji kuenezwa na kutekelezwa na watu,
hapa ndipo unapata team ya Uongozi na
Wanachama wa ACT-Wazalendo na waumini
wengine wa falsafa ya Ujamaa wa Demokrasia
waliokwishajiunga na watakaojiunga baadaye.
Kwa hiyo dhana ya kujiunga ACT-Wazalendo ni
kumfuata mtu ni dhana ya maadui wasiojua
wanapambana na nini, watapoteza muda na
watakuja kushangaa hata kama mtu huyo hayupo,
upinzani dhidi yao utazidi kushamiri. Msingi mkuu
wa ACT-Wazalendo siyo mtu ni IMANI yetu ya
Ujamaa wa Kidemokrasia.
Tangu tupate uhuru tumekuwa tukifuata mfumo
wa Ujamaa, Pamoja na mazuri yake kama vile
kutokuwa na gap kubwa kati ya masikini na
matajiri, fursa sawa katika kupata huduma za
kijamii kama vile Elimu, Afya, n.k, katika miaka
ya 1980 mfumo huu ulianza kufeli. Sababu ziko
nyingi, nyingine ni ufisadi tu! Lakini kubwa ni la
kiimani, ambalo ni matakwa ya kila mwenye
juhudi kutaka anufaike na matunda ya juhudi
zake bila kuwa na mipaka, namaanisha tama ya
utajirisho au ukwasi kwa kiwango atakacholizika
nacho yeye. Imani ya Ujamaa kwa watu
ikapungua na taratibu tukaanza safari ya
kuelekea kwenye Ubepari. Katika mfumo wa sasa
Ubepari Matajiri wameongezeka, mafukara
wamekuwa wengi kupindukia, huduma za msingi
zimekuwa za matabaka, kama wewe ni mtu wa
chini mtoto wako hawezi kusoma shule nzuri,
then atakuwa na elimu duni na mwisho wa siku
si rahisi kumudu ushindani katika ajira! Huduma
bora za afya ni kwa wenye fedha. Matajiri
wanamiliki maelfu ya hekari za ardhi kwa
matumizi yao leo na kwa vizazi vyao vya kesho.
Mtoto wa masikini siku za usoni hana chake
katika nchi yake kwa kuwa tu wazazi wake ni
masikini.
Upinzani tuliokuwanao kwa kiwango kikubwa
unafuata mrengo wa kati. Ni ngumu mrengo huu
kuaminika kwa kuwa ni ngumu kujua katika
jambo gani utaegemea kwenye uelekeo wa
Ujamaa na ni katika jambo gani utaegemea
uelekeo wa Ubepari! Lakini practice ya Upinzani
tuliokuwanao inaonyesha dhahiri kuwa
unaegemea zaidi mfumo wa kibepari, kwa
mantiki hiyo basi bado hatuna suluhisho la
matatizo ya kimfumo tuliyonayo sasa, matatizo
ya matajiri kumiliki ardhi yote. Matatizo ya elimu
bora kwa wachache wenye fedha na hivyo ajira
kubaki za kwao tu. Matatizo ya mwenye fedha
ndiye mwenye haki ya kupata huduma bora za
afya. Matatizo ya mafukara wengi mno
kuongezeka huku wachache wakitumia fursa za
rasilimali zetu sote kujitwalia ukwasi uliopindukia,
n.k. Hapa ndipo IMANI ya Ujamaa wa
Kidemokrasia inapoweza kutusaidia katika
kutatua matatizo haya:
1. ACT-Wazalendo katika Ujamaa wa
Kidemokrasia tunaamini kuwa kila mtu anayohaki
ya kujitajirisha. Lakini ni jukumu la Serikali
kutumia rasilimali zilizopo kuwainua watu wa
tabaka la chini ili kupunguza gap kati ya masikini
na tajiri.
2. ACT-Wazalendo katika Ujamaa wa
Kidemokrasia tunaamini kuwa huduma zote za
msingi serikali ina wajibu wa kuzisimamia na
kutoa fursa sawa kwa raia wote bila kujali tofauti
zao katika vipato au kitu kingine chochote.
Masikini aliye na ugonjwa ana haki ya kupata
matibabu na kuishi sawasawa na tajiri mgonjwa.
Mtoto wa masikini ana haki ya kupata elimu bora
sawasawa na mtoto wa tajiri ili wote waweze
kuwa na fursa za kuchangia katika maendeleo ya
nchi.
3. Utajiri wa nchi au rasilimali nyeti kama madini,
mafuta, gesi, ardhi, n.k lazima zisimamiwe na
serikali kwa manufaa ya wote. Na zaidi zitumike
katika kuwawezesha wanyonge ili wawe na
uwezo wa kushiriki katika uchumi wa nchi
(Uchumi Shirikishi)
Na kadhalika.
Nchi ni lazima iongozwe na uelekeo unaoeleweka
wazi, na katika nchi yetu Ujamaa pamoja na uzuri
wake bado ulikuwa na mapungufu yaliyopelekea
ukashindikana, Ubepari ndio umetufikisha kwenye
matatizo tuliyonayo leo. Ni mtazamo wangu kuwa
IMANI hii ya Ujamaa wa Kidemokrasia ni
suluhisho la matatizo haya ya sasa.
Haki Ya Mtu Kamwe Haipotei, Hamuwezi Mkavamia Mchana Kweupe Mkapola Chama Cha Limbu, Mkammilisha Aya, Tolah.