Richard Robert
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 632
- 340
Kuhusu Bunge kutakuwa na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na Wabunge wa kuchaguliwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha Watu wenye Ulemavu.
Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake.
Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hata hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa kipindi chake.
Inapendekezwa pia kusiwepo na uchaguzi mdogo isipokuwa kama nafasi inayokuwa wazi inatokana na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo, lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na Mbunge wa Chama cha Siasa basi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.
Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe Viongozi wa vyama vya Siasa.
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.
Ndugu Richard someni Rasimu yote kwanza kwa makini. Hii ni Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Shirikisho la Zanzibar na Tanganyika. Majimbo ya ubunge yaliyobainishwa ni mikoa ya Tanganyika na wilaya za Zanzibar. Kila mkoa unafanya jimbo ambalo litakuwa na nafasi mbili za ubunge, ambazo nazo zimegawanywa kati ya wanaume na wanawake. Mimi ninafikiri ni njia bora kuliko vitu maalumu. Sasa kuhusu bunge la Tanganyika na majimbo mangapi hiyo ni raundi nyingine ya rasimu ya katiba ya Tanganyika (ambayo ndio imebakia kiini macho - mchakato unaanza lini). Ninakubaliana na pendekezo lako la kupunguza majimbo ya bunge la Tanganyika wakati utakapofika wa kuunda katiba tutalipigia debe. Tunaweza kukubaliana tuwe na hiyo idadi ya 100 tu na tutatafuta fomula ya kushirikisha jinsia zote mbili.Maoni yangu:
Sikubaliani na uwakilishi wa wanaume na wanawake kwenye majimbo kwa sababu zifuatazo:
1. Mfumo huu utaongeza gharama kubwa sana za kuendesha bunge.
2. Mfumo huu utakuwa ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi.
3. Hii inamaana majimbo 239 yatatoa wabunge 478 (pengine yataongezwa mengine)
4. Je, usawa wa kijinsia ukiibua hoja za usawa wa dini, na makabila tutaelekea wapi?
Nini kifanyike
1. Tume ipunguze majimbo ya uchaguzi na kufikia 100;
2. Nguvu ielekezwe kukomboa wanawake kielimu na kupanua wigo wa ajira.
3. Wanawake wagombee majimboni kama wengine, vinginevyo serikali iandae utaratibu wa uwiano wa kidini na kikabila.
4. Ukombozi uelekezwe kwa wanawake walio wengi.
imekaa kama vile wanataka kuoza watu bungeni,Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.
Tulimumu,
Ukifuatilia mjadala wa bunge unaoendelea utagundua CCM ina wabunge wanne tu ambao wanawatendea haki wananchi waliowachagua na watanzania kwa ujumla.
Wabunge hao ni Alphaxard Kangi Lugora (Mwibara), Deo Filikunjombe (Ludewa), Ally Keissy Mohamed (Nkasi Kaskazini) na Luhaga Mpina (Kisesa). Wengine waliosalia ni magalasha tu wa kujaza viti bungeni kupiga makofi meza zetu hata kwa mambo ya kijinga kabisa.
Ndio maana utawasikia wanasema wanaunga mkono asilimia mia kwa mia kitu ambacho hakuna wizara inayopata mia kwa mia katika utekelezaji.
Hawa wanne nawatia moyo wasiogope kukolimbwa kwani vita yao ni ya wananchi si ya CCM.
ni ujinga usipopingika... kwanini wabebwe siku zote
Ni kweli itaongeza gharama endapo majimbo hayatapunguzwa ila mi naona ni afadhali zaidi kuliko kwani itapunguza idadi ya wabunge vimeo dizaini ya Sofia Simba
PROF. Baregu Amewasaliti WANACHADEMA ambao siku zote wanapinga MLUNDIKO Wa Uongozi wa Serikali pasipo na MSINGI wowote.
Ndugu Richard someni Rasimu yote kwanza kwa makini. Hii ni Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Shirikisho la Zanzibar na Tanganyika. Majimbo ya ubunge yaliyobainishwa ni mikoa ya Tanganyika na wilaya za Zanzibar. Kila mkoa unafanya jimbo ambalo litakuwa na nafasi mbili za ubunge, ambazo nazo zimegawanywa kati ya wanaume na wanawake. Mimi ninafikiri ni njia bora kuliko vitu maalumu. Sasa kuhusu bunge la Tanganyika na majimbo mangapi hiyo ni raundi nyingine ya rasimu ya katiba ya Tanganyika (ambayo ndio imebakia kiini macho - mchakato unaanza lini). Ninakubaliana na pendekezo lako la kupunguza majimbo ya bunge la Tanganyika wakati utakapofika wa kuunda katiba tutalipigia debe. Tunaweza kukubaliana tuwe na hiyo idadi ya 100 tu na tutatafuta fomula ya kushirikisha jinsia zote mbili.