Sera ya kubeba wanawake ni mzigo kwa taifa: HAISAIDII TAIFA

Richard Robert

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
632
340
Rasimu ya katiba inasema:
Kuhusu Bunge kutakuwa na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na Wabunge wa kuchaguliwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha Watu wenye Ulemavu.

Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake.

Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hata hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa kipindi chake.

Inapendekezwa pia kusiwepo na uchaguzi mdogo isipokuwa kama nafasi inayokuwa wazi inatokana na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo, lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na Mbunge wa Chama cha Siasa basi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.

Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe Viongozi wa vyama vya Siasa.

Mpaka sehemu Hii hapo juu mambo safi! .........

Pabaya ni Hapa kwenye kijani:...

Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.

Huu ni ulaji tu!.. Hauna tija kwa mwanamke wala jamii ya kitanzania... Ni mfumo wa kunufaisha wachache na kuumiza wengi.

Maoni yangu:
Sikubaliani na uwakilishi wa wanaume na wanawake kwenye majimbo kwa sababu zifuatazo:
1. Mfumo huu utaongeza gharama kubwa sana za kuendesha bunge.
2. Mfumo huu utakuwa ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi.
3. Hii inamaana majimbo 239 yatatoa wabunge 478 (pengine yataongezwa mengine)
4. Je, usawa wa kijinsia ukiibua hoja za usawa wa dini, na makabila tutaelekea wapi?

Nini kifanyike
1. Tume ipunguze majimbo ya uchaguzi na kufikia 100;
2. Nguvu ielekezwe kukomboa wanawake kielimu na kupanua wigo wa ajira.
3. Wanawake wagombee majimboni kama wengine, vinginevyo serikali iandae utaratibu wa uwiano wa kidini na kikabila.
4. Ukombozi uelekezwe kwa wanawake walio wengi.
 
Ndugu Richard someni Rasimu yote kwanza kwa makini. Hii ni Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Shirikisho la Zanzibar na Tanganyika. Majimbo ya ubunge yaliyobainishwa ni mikoa ya Tanganyika na wilaya za Zanzibar. Kila mkoa unafanya jimbo ambalo litakuwa na nafasi mbili za ubunge, ambazo nazo zimegawanywa kati ya wanaume na wanawake. Mimi ninafikiri ni njia bora kuliko vitu maalumu. Sasa kuhusu bunge la Tanganyika na majimbo mangapi hiyo ni raundi nyingine ya rasimu ya katiba ya Tanganyika (ambayo ndio imebakia kiini macho - mchakato unaanza lini). Ninakubaliana na pendekezo lako la kupunguza majimbo ya bunge la Tanganyika wakati utakapofika wa kuunda katiba tutalipigia debe. Tunaweza kukubaliana tuwe na hiyo idadi ya 100 tu na tutatafuta fomula ya kushirikisha jinsia zote mbili.
 
Huu uwiano kwenye mambo yanayohitaji uwajibikaji sikubaliani nao.
Tutakuwa tunawezesha bunge kuwa na mipasho tu kama lazima nafasi itengenezwe kwa ajili ya mtu.
Wapo wanawake wenye uwezo na michango yao kwenye jamii tunaiona, watagombea na tutawapa kura.
 
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.
imekaa kama vile wanataka kuoza watu bungeni,
Inanikumbusha enzi hizo tuko Tabora School (T. Boys & T. Girls), selection ilikuwa kila wilaya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja.
Mkifika skuli kila mtu anakuwa na "Warsaw" (woso) wake.... wadau watajua nasema nini.
 
Tulimumu,
Ukifuatilia mjadala wa bunge unaoendelea utagundua CCM ina wabunge wanne tu ambao wanawatendea haki wananchi waliowachagua na watanzania kwa ujumla.

Wabunge hao ni Alphaxard Kangi Lugora (Mwibara), Deo Filikunjombe (Ludewa), Ally Keissy Mohamed (Nkasi Kaskazini) na Luhaga Mpina (Kisesa). Wengine waliosalia ni magalasha tu wa kujaza viti bungeni kupiga makofi meza zetu hata kwa mambo ya kijinga kabisa.

Ndio maana utawasikia wanasema wanaunga mkono asilimia mia kwa mia kitu ambacho hakuna wizara inayopata mia kwa mia katika utekelezaji.

Hawa wanne nawatia moyo wasiogope kukolimbwa kwani vita yao ni ya wananchi si ya CCM.

Haya ni maoni ya mdau mmoja - Tulimumu katika thread yake kuhusu wabunge. Tunajaza wabunge bungeni ili iweje?
 
Kweli hii siyo sera sahihi hata kidogo.Watafute njia nyingine ya kuongeza ajira kwa wanawake na sio kuwapatia ubunge. Huu uwakilishi wa mbunge mmoja tayari ni mzigo tosha kwa taifa.
 
Ni kweli itaongeza gharama endapo majimbo hayatapunguzwa ila mi naona ni afadhali zaidi kuliko kwani itapunguza idadi ya wabunge vimeo dizaini ya Sofia Simba
 
Nasikitika kuona LUNDO/ MZIGO wa Kodi kulundikiwa MTANZANIA. Kama Tunatafuta sifa UN basi yatosha. Iweje Jimbo moja WABUNGE wawili? Mfano mimi naishi hapa Dar es salaam Majimbo yapo (5) kwahiyo msimu ujao WABUNGE 10 Mkoa 1. Uhuni huu. Imenikera na Sitaunga Mkono Katiba Mpya.
 
Ni kweli itaongeza gharama endapo majimbo hayatapunguzwa ila mi naona ni afadhali zaidi kuliko kwani itapunguza idadi ya wabunge vimeo dizaini ya Sofia Simba

MKUU siyo Vimeo Wewe Unadhani Mfano jimbo moja waongoze MWIGULU na SHONZA si itakuwa MIPASHO KILA Siku
 
PROF. Baregu Amewasaliti WANACHADEMA ambao siku zote wanapinga MLUNDIKO Wa Uongozi wa Serikali pasipo na MSINGI wowote.
 
MAWAZIRI wengi NO, ila WABUNGE wengi YES.... Huu ni USHENZI na UFEDHULI wa hali ya JUU. WAKATI nchi ikilalamika ONGEZEKO la Deni la Taifa, Zahanati, shule n.k WAO Mafisadi kupitia Rasimu hii Watapata AHUENI.
 
Binafsi sikubaliani na hii hoja ya wabunge wawili kwa kifupi haina mashiko hapa kina warioba wameteleza, kwa mfano tujiulize wabunge wa sasa wanawake wameleta mabadiko gani kwa jamii nzima!
 
Cha msingi tukatae hicho kipengele! Huo mzigo ni mkubwa kwa mlalahoi jaman! Wote wagombee nafasi mambo ya upendeleo yamepitwa na wakati
 
Elimu ya Wabunge ianzie level gani? maana mtu kama Prof. Maji Mafupi naonaga anatoa povu tu bungeni nafikiri upeo wake ndipo ulipoishia na Std. 7 yake.
 
Ndugu Richard someni Rasimu yote kwanza kwa makini. Hii ni Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Shirikisho la Zanzibar na Tanganyika. Majimbo ya ubunge yaliyobainishwa ni mikoa ya Tanganyika na wilaya za Zanzibar. Kila mkoa unafanya jimbo ambalo litakuwa na nafasi mbili za ubunge, ambazo nazo zimegawanywa kati ya wanaume na wanawake. Mimi ninafikiri ni njia bora kuliko vitu maalumu. Sasa kuhusu bunge la Tanganyika na majimbo mangapi hiyo ni raundi nyingine ya rasimu ya katiba ya Tanganyika (ambayo ndio imebakia kiini macho - mchakato unaanza lini). Ninakubaliana na pendekezo lako la kupunguza majimbo ya bunge la Tanganyika wakati utakapofika wa kuunda katiba tutalipigia debe. Tunaweza kukubaliana tuwe na hiyo idadi ya 100 tu na tutatafuta fomula ya kushirikisha jinsia zote mbili.

Formula ni wanawake wajitokeze kugombea na wapigiwe kura kama wengine. si lazima kuiga kila kitu cha wa kenya
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom