Sera mpya ya faragha ya WhatsApp inavyowafukuza wateja

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Mapema wiki hii, programu tumishi ya mawasiliano ya WhatsApp ilianza kutoa taarifa kwa watumiaji wake wa Android na iOS kuhusu mabadiliko ya sera ya matumizi na sera ya faragha, ikiwafahamisha wateja wake kuhusu jinsi mtandao huo utakavyomudu taarifa binafsi za watumiaji wake.

Sera hizo mpya sasa zitawezesha taarifa za watumiaji wa WhatsApp kuonekana na kuhifadhiwa na huduma za Facebook, yaani kampuni zinazoshirikiana na Facebook kutoa huduma kwa programu zinazomilikiwa na Facebook, kwa lengo la kuboresha huduma zao. Hii inamaanisha kuwa taarifa yoyote utakayoitoa kwa WhatsApp itafahamika na Facebook, ikiwamo taarifa unazotoa wakati wa kuunda akaunti yako ya WhatsApp.

Taarifa zinazokusanywa na WhatsApp
WhatsApp inakusanya taarifa za shughuli zako unazozifanya mtandaoni, kwa kiasi gani unatumia mtandao huo, mpangilio wa programu unaopendelea, picha ya wasifu (profile photo) na taarifa kuhusu wewe ('about' information).

Vilevile WhatsApp inakusanya taarifa kuhusu kifaa chako cha kielektroniki unachotumia, mtandao wako wa simu, anwani ya IP na eneo la kijiografia unalopatikana.

WhatsApp imesema kuwa itatumia taarifa hizo kusaidia "kuendesha, kutoa, kuboresha, kuelewa, kusaidia na kuchagua huduma zinazowafaa watumiaji, ikiwamo kwa Bidhaa za Kampuni ya Facebook."

Taarifa zako zinaweza kutumiwa na mtandao wa Facebook na Bidhaa zake kutoa mapendekezo na kukuchagulia huduma na maudhui, kukusaidia kukamilisha malipo ya bidhaa na kufanya miamala, kukuonesha ofa zinazoweza kukufaa na kuchagua aina ya matangazo ya kukuonesha katika mitandao yote Bidhaa za Kampuni ya Facebook.

Bidhaa za Kampuni ya Facebook ni pamoja na Facebook Messenger, Instagram, Oculus Products, Facebook Shops, Spark AR Studio, Audience Network, Programu za NPE Team, nk.

Kwa sasa, unaweza kukubaliana au kutokubaliana na sera hii mpya, ila utalazimika kukubaliana na sera hii itakapofika Februari 8, 2021, vinginenvyo hautaweza kutumia programu hiyo.

Hata hivyo WhatsApp imeendelea kusisitiza kuwa haihifadhi jumbe za watumiaji katika seva (servers) zake, na kuwa mawasiliano baina ya mtumiaji mmoja na mwingine yanalindwa na mfumo wa usimbaji fiche (encryption) wa taarifa za mawasiliano. Ujumbe unaotumwa kupitia kwa WhatsApp huhifadhiwa kwa muda wakati ukisubiri kupokelewa na mtumiwaji, kisha hufutwa kwenye seva za WhatsApp baada tu ya kupokelewa. Ujumbe wa mtumiaji huweza kuhifadhiwa katika seva za WhatsApp kwa muda wa hadi siku 30 ikiwa hautapokelewa na mtumiwaji, kisha baada ya hapo huondolewa katika seva.

Hisia za watumiaji
Tangu kuanza kuonekana kwa taarifa hizi, kumekuwa na mijadala mingi mitandaoni juu ya usalama wa taarifa za watumiaji, wengi wakiona kuwa kampuni ya Facebook inavuka mipaka kuhusu usalama wa taarifa zao.

Bila kuelewa kinachoendelea, wengi wamekiri kukubaliana na sera hiyo mpya bila hata kuisoma, wakishangaa kuona mjadala unaendelea kuhusu jambo ambalo wameshakubaliana nalo bila kujua! Mjadala mpya unaibuka kwa watumiaji wa WhatsApp kuhamisha matumizi katika programu tumishi zingine, ikiwamo Signal na Telegram.

Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Tesla, SpaceX na Boring, Elon Musk alichapisha taarifa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akiwashawishi watumiaji wa WhatsApp kuhamia Signal.



Musk ni mmoja tu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walioonesha wasiwasi wao kuhusu sera mpya ya faragha ya mtandao wa WhatsApp. Mitandao mbadala inayotajwa ya Signal na Telegram nayo haikuchelea kukamata fursa na kujinadi kuwa watumiaji watakaoamua kuhamia kwao watakuwa salama.



Mtandao wa Telegram ulichapisha video maarufu ya 'wajuba' wabeba majeneza wa Ghana ikiwa na ujumbe wa WhatsApp unaokutaka ukubaliane na sera mpya ya faragha, ukiibua maswali mengi katika kipengele cha maoni.



Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walikwenda mbali zaidi kuelezea tofauti ya mitandao hiyo na matumizi ya taarifa binafsi za watumiaji, huku wakibainisha kuwa katika mitandao yote minne (Facebook, WhatsApp, Telegram na Signal) mitandao yote miwili ya Facebook inahifadhi taarifa nyingi zaidi za watumiaji, ikiwamo manunuzi, utambuzi wa eneo la kijiografia, nk. Mitandao ya Telegram na Signal haina taarifa zinazomtambulisha mtumiaji moja kwa moja.

Nini cha kufanya?
Ikiwa umeridhia mpangilio huu mpya wa mtandao wa WhatsApp, bila shaka unaweza kuendelea kutumia mtandao huo.
Ikiwa haujakubaliana na mpangilio huu mpya wa sera za faragha za WhatsApp, unaweza kuendelea kutumia WhatsApp bila kuhofia usalama wa taarifa zako hadi Februari 8, 2020, ambapo utalazimika kukubaliana na mpangilio huo mpya kama utahitaji kuendelea kutumia WhatsApp. Ikiwa umekwisha kubaliana na mpangilio huo, lakini hautaki WhatsApp kutoa taarifa zao kwa Facebook, una muda wa chini ya siku 30 kufuta akaunti yako katika mtandao wa WhatsApp.

Kitu gani kitatokea ikiwa utafuta akaunti yako?
Sera za mtandao wa WhatsApp zinaeleza kuwa utakapofuta akaunti yako, jumbe zako ambazo hazijapokelewa zitafutwa katika seva zake, pamoja na taarifa zako zote ambazo hazihitajiki katika uendeshaji wa shughuli zake.

Hata hivyo, unatakiwa kuwa makini: kufuta programu ya WhatsApp kutoka kwenye simu yako hakumaanishi kuwa taarifa zako zimeondolewa kutoka kwenye seva za WhatsApp. Ili kuondoa taarifa zako inabidi ufute akaunti yako kwa kufuata hatua zifuatazo:
Nenda kwenye settings > Account kisha chagua "Delete my account."
 
Hii Inshu yaweza kuwa pigo Kwa Zuckerberg, Tangu Mtaalamu Musk aponde hio sera mpya na kushauri watu watumie Signal App, wengi washaanza kuilalamikia WhatsApp.

Ukiangalia Musk ni mtu mkubwa sana(sasa hivi yupo Juu pale ya Mabilionea) kitu kidogo tuu atakachosema kinaondoka na lundo la watu..

Kuachana na hilo, hawa jamaa kama wana bifu fulani hivi la chini chini.
 
Hii Inshu yaweza kua pigo Kwa Zuckerberg, Tangu Mtaalamu Musk aponde hio sera mpya na kushauri watu watumue Signal App, wengi washaanza kuilalamikia WhatsApp..
Ukiangalia Musk ni mtu mkubwa sana(Asaivi yupo Juu pale ya Mabillionea) kitu kidogo tuu atakacho sema kinaondoka na lundo la watuu..

Kuachana na hilo, hawa jamaa kama wana bifu flan hivi la chini chini,
Ila kiukweli sioni mtu wa kumshusha tena Musk pale juu hivi karibuni.
Kazi ipo. Jamaa wanadaka raia balaaa
IMG-20210110-WA0131.jpg
 
Musk na Zuckeberg wana bifu la siku nyingi. Hii ni ukweli Facebook wanakusanya sana taarifa za wateja wao na kuziuza ila bila hivyo bado wateja hawawezi faidika. Mfano ukitoa tangazo la biashara unachagua eneo la kuoneshwa tangazo hilo, bila Facebook kuwa na taarifa za watumiaji wako wapi wasingeweza kuwa na feature hii.

Kuna kampuni isiyohusika nayo inaanza na jina la Signal ilipanda hisa zaidi ya 1,000% ndani ya masaa baada ya Musk kutweet vile. Watu walikurupuka kununua hisa kumbe wamekosea majina. Musk sasahivi akitweet kitu watu wanawahi fursa ila atakuja tengeneza bifu sana. Ndio maana Tesla waliwahi mpiga marufuku kupost chochote kuhusu kampuni kwa muda.
 
Kifo cha Zuckerberg kibiashara, tunahamia SIGNAL na Telegram.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Hakuna kama telegram kwa sasa. Toleo jipya lina "voice chat" hii ni kama radio call mnachat live kabisa na sio mpaka urecord afu utume hapana unaongea na mwenzako anaongea. Nineipenda sana hii
 
Hakuna kama telegram kwa sasa. Toleo jipya lina "voice chat" hii ni kama radio call mnachat live kabisa na sio mpaka urecord afu utume hapana unaongea na mwenzako anaongea. Nineipenda sana hii

Voice chat ina tofauti gani na voice call ya whatsapp*?
 
Kilichowaponza Whatsapp ni kuwa 'Honest', ki uhalisia Hakuna Mtandao wa kijamii wa Dunia ya Kwanza Usiofanya kitu wanachofanya Whatsapp. Walichofanya Whatsapp/Fb ni kukueleza tu kuwa Taarifa zako tutazitumia kibiashara, Je unafahamu mitandao mingine inatumia vipi taarifa zako? Njia rahisi ya Kulinda Faragha zako mtandaoni ni Kutokutumia Mtandao kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom