Sensa ya kilimo, uvuvi, ufugaji mbioni

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1565021391751.png


OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakusudia kufanya sensa ya kilimo, uvuvi na ufugaji nchini ili kupata matokeo ya mchango wa sekta hiyo, kwenye pato la Taifa na kupanga mikakati mingine mipya.

Kwa kuanzia, timu ya wataalamu wa NBS ipo mkoani Morogoro kwa ajili ya kufanya zoezi la majaribio katika mikoa sita ya Bara na miwili Zanzibar na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kusaidia kupatikana kwa takwimu hizo.

Akizungumza katika Maonyesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea mkoani Simiyu, Mtakwimu Mwandamizi kutoka ofisi hiyo, Samwel Kawa, alisema kupatikana kwa takwimu hizo zitawezesha kupanga, kupima na kufuatilia Tathimini ya Programu ya Pili ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP II) .

Alisema pia kupatikana kwa takwimu hizo kutasaidia kufikia uchumi wa kati wa Tanzania ya viwanda pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mpango wa pili wa Taifa wa Maendeleo na Usalama wa Chakula pamoja na vita dhidi ya umaskini.

Kawa alisema sensa ya kilimo ya mwisho ilifanyika mwaka 2007/2008, hivyo kufanyika kwa sensa mpya kutatoa takwimu mpya kuhusu uzalishaji wa mazao, idadi sahihi ya mifugo pamoja na mazao yatokanayo na mifugo.

“Lengo la sensa hii ni kupata taarifa sahihi za hivi karibuni za 2018/19 zinazohusiana na uzalishaji wa mazao, idadi ya mifugo na mazao yatokanayo na mifugo,” alisema Kawa. Kwa upande wake, Ofisa Masoko wa Ofisi hiyo, Andrew Punjila, alisema sensa hiyo itakusanya taarifa kuhusu takwimu na hali ya takwimu nchini.


Alisema kupitia takwimu hizo, itasaidia serikali kujua mchango wa sekta katika pato la taifa, kupima mikakati yake ya kufikia Tanzania ya viwanda na inatoa fursa kwa wadau wengine kujua fursa na changamoto ya sekta hiyo.
 
Back
Top Bottom