Acha uvivu wa kufikiri,mbona dai la waisilamu lipo wazi ...usitake kuudanganya uma kwa maneno yako ya kusadikika eti "wanataka maboresho ndani ya maswali ya sensa" ...Inamaana kujua huyu ni Mtanzania muislamu na huyu ni Mtanzania Mkristo ama Mpagani hapo kuna tija!!!
wewe hujui sasa hivi islamic finance imeshika kasi duniani ? hujui kuwa hapa Tanzania napo baadhi ya mabenki wameanzisha idara ama islamic banks? hujui kama sasa pia kuna full islamic bank-Amana Bank ?
hujui pia kuwa ili banki hizi ziweze kufanya kazi zake sawa sawa inahitajika kuwepo islamic insurance inayo itwa Takaful ? na Commssioner wa bima karibuni aliteua watu kwenda Malayasia, Sudan Qatar na UAE..kwenda kufanya study ya Takaful?
hivyo jua kwamba data hizi ni muhimu kwa investors ambao watataka kuja kuwekeza katika shughuli hizi ama kuwekeza katika islamic financial institutions?
jee si humu ndio unaweza kufanya research work yako ujkajua idadi ya waislam , elimu zao, na pia itasaidia kujua market ipo namna gani ?
hii ni faida moja mbili za data kama za dini, umuhimu upo ila serikali na baadhi ya watu huwa wanapinga kwa sababu tu walio taka ni waislam na si venginevo ?
sasa mbona hawaatuelezi sababu za kwa nini data hizi si muhimu ? ama data za makabila sio muhimu? jee si itasaidia kuijua mfano kabila gani wapo nyuma kielimu ? na jee kama Taifa lina wajibu gani wa kurekebisha hali hiyo ?
kwa hiyo faida ni nyingi zaidi kupata data hizi na hasara ya kuweka data hizi ni hakuna hasara yoyote.
jee hujui kwamba jumuia za dini zimekuwa mbele katika kukoa huduma za kijamii kama elimu , afya na huduma nyengezo ?
jee hujui kwamba labda ( as sina uhakika)50% ya wakristo wanakwenda kanisani jumapili ? jee hujui kwamba zaidi ya nusu ya waislam IjUMAA wanakwenda misikitini ?
jee sio kweli kwamba watanzania ni wengi zaidi katika dini zao kuliko vyama vyao ? jeee wingi huu hauwezi kuwekewa taratibu ukajulikana ? jee hii si itaweza kusaidia kuondoa ubaguzi kwa wale minority ?
Data on religious affiliation zinaweza kutumiwa katika kupanga mipango ya eleimu , huduma kwa wazeee,na huduma nyengine muhimu kwa waumini na hizi zitaweza kupatikana kwa ufanisi kama kutakuwa na data za wana dini.
itasaidia kujua uwepo wa makanisa ama misikiti katika mji , ama kijiji
unaweza ku dai si data hizi mutazipata misikitini ama makanisani ? hili haliwezekani sio wote wanaenda makanisani , sio wote wanaonda misikitini.
hivyo kina ponda wao sawa kudai data hizi kupatikana .