Sensa haina mbadala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sensa haina mbadala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kavulata, Aug 9, 2012.

 1. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3,202
  Likes Received: 1,559
  Trophy Points: 280
  Kujua idadi ya watu unaowahudumia ni muhimu sana kuliko kitu chochote unachopaswa kukifamu. Hata mama nyumbani anahitaji kufahamu watu (idadi, umri, jinsia, afya zao) walioko nyumbani kwake ili ajue apike chakula kiasi gani na cha aina gani, ajue idadi ya sahani, vijiko, mashuka ya kujifunika, na mahitaji mengine yatakayowatosha watu wake.

  Serikali pia inahitaji kufahamu idadi na aina ya watu wake ili iweze kupanga mipango ya kuwahudumia wananchi wake. Mfano, idadi ya watu kwenye wilaya husika ni kigezo kimojawapo katika kugawanya fedha (keki ya taifa) katika mawilaya, uchapishaji wa fedha/sarafu za nchi, kujenga shule, zahanati/hospitali, vituo vya police katika eneo fulani. Kuna njia tatu za namna ya kujua idadi ya watu nchini: 1. kuhesabu watu wote (sensa) kila baada ya miaka 10, kukadiria kulingana na idadi ya kuongezeka kwa watu kwa mwaka (growth rate) ambayo unatumia (waliozaliwa kwa mwaka - waliokufa kwa mwaka) + (waliohamia - waliohama nchi)+ Idadi ya watu mwaka uliopita, na njia ya tatu ya kujua idadi ya watu ni kwa kutumia takwimu (vital statistics) kwa kuweka kumbukumbu sahihi za vizazi na vifo, wahamiaji na wanaohama. Njia hii ya tatu ndiyo inayotumiwa na mataifa yaliyoendelea kwakuwa wana mfumo mzuri wa kusimamia vizazi, vifo, uhamiaji na uhamaji. Lakini sisi bado tuhahitaji sensa ili tujuane tuko wangapi.

  Sasa kama wako watu ambao wanasema hawatashiriki sensa kwa sababu ya aina yoyote ile basi wanahitaji kuelimishwa na kuombewa, maana baada ya sensa kukamilika pesa, na huduma mbalimbali zitagawanywa kulingana na idadi ya watu kwa mujibu wa sensa 2012 kwenye eneo husika, watu watanza kushangaashangaa na kulalamika tena huduma nyingi zitakapoelekezwa sehemu zenye "watu wengi".
   
 2. B

  Bull JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nadhani wanaoandaa sensa ndio wanaoitaji kuelimishwa, kwa sababu ktk faida ya sens ni pamoja pia kujua idadi ya dini kama watu wengi wanavyo ishauri serikali lakini bahati mbaya waandaaji wao serikali uwezo wa kufahamu nimdogo au kwa makusudi wanataka kuondoa kipengele cha dini

  Kumbuka hivi karibuni bungeni Waziri mkuu alikaririwa akitoa takwimu ya watu wa Zanibari, alisema "Waislam znz ni 99% hivyo wanahaki kufunga hoteli mwezi wa Ramadhani" takwimu hizi kazipata wapi? kwanini kazitowa wakati hataki kipengele cha dini kwenye sensa?
  Niwazi Pinda na wenzake hawajui walifanyalo serikali!!
   
 3. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3,202
  Likes Received: 1,559
  Trophy Points: 280
  Serikali kujua watu wake kwa misingi ya dini sio kipaumbele, kwasababu hiyo taarifa ya dini serikali haina kazi nayo, kwakuwa serikali haitoi huduma kwa wananchi wake kwa kutegemeana na dini zao. Serikali haijengi nyumba za ibada, haipeleki waumini kwenda kuhiji, haigawi wala haifugi kiti moto nchini, kwahiyo taarifa ya dini kwake haina maana yotote. Mfano, kwani serikali ikijua kwamba Tanzania ina waislamu 46%, wakristo 44% na dini nyinginezo 10% itafanyia nini taarifa hiyo?
   
 4. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaa"ALLAH"Natamka kwa Ulimi ninakiri kwa moyo kuwa wewe"ALLAH"ukiwa Shahidi,kua sito Shiriki zoezi la SENSA mpaka Kipengele cha "DINI" kiwemo katika "DODOSO"za "SENSA"Sitoshiriki maana huo ndio msimamo wa "WAISLAMU",na kama nitashiriki, Allah unajua nini malipo ya "WANAFIKI"Nlinde nisiwe miongoni mwa WANAFIKI,Amina! TUMA ZAID KWA WAISLAM

  Ujumbe Huu unatumwa kwa SMS kwa kasi ya ajabu imekaaje Hii?
   
 5. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3,202
  Likes Received: 1,559
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jiulize, aliyesema tusishiriki sensa ni kipofu mtatumbukia wote. Akili za kuambiwa changanya na zako
   
 6. B

  Bull JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba unifahamishe, kwanini Pinda aliliambia bunge kuwa 99% ya wazanzibari ni waislam, aliipata wapi? na kwanini aliitumia kujibu hoja bungeni kama serikali hawana kazi nayo ??
   
 7. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani nimetoka kwenye Semina ya sensa dodoso refu but malipo hakuna wanapiga danadana,hv tunakula,kulala na kusafiri vp ktk kpnd hki kigumu?
   
 8. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maoni yangu ni kuwa kwa kuwa zoezi la sensa na vitambulisho vinafanyika karibu wakati mmoja, kwa nini zoezi la vitambulisho lisitumike kupata sensa - killing two birds with one stone na kupunguza gharama?

  Vitambulisho visitenge watoto chini ya miaka 18 waliozaliwa nchini, hakuna sababu ya msingi.
   
 9. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  You can't be serious....How differently would you be receiving social services because of your religion?
   
 10. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  hivyo hivyo tu wacha tutumbukie humohumo wala lisikupe presha hilo. si ni sisi, wewe inakuwasha nini?????
   
 11. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  HAKUNA KIPENGELE CHA DINI KWNY SENSA, BUSARA KUBWA NA LOGIC IMEZNGATIWA!HUO NDIO USOMI, MWNY KTAKA 2JUE IDADI YA WA2 NA DINI ZAO NI U-FREEMASON AMA USHETANI/LOUSFA KABISAAA... Toa taka2 dini toa kabisa hko!
   
 12. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  kutoshirki sensa ni kuhujumu taifa.
   
 13. d

  danizzo JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada umenifanya nijiulize maswali yafatayo; {1}inawezakana kua maisha magumu yanatokana nakua serikali haijui idadi ya watu wake? {2}sasa itawezekana vp kupata takwimu itakayo saidia maendeleo ikiwa kuna wananchi ambao hawaesabiwa? {2}nakama watahesabu na takwimu itakayo patikana itakua na maana gani tena? {4}inakuaje bahazi ya wananchi/kundi flani, wapotayari fedha zipotee kwaajiri ya sensa uchwara ilimradi tu wengine waonekane hawana mana? {5}je ni matabaka mangapi yamegomea sensa wampaka malalamiko yao yatakapo tendewa kazi? {6}namangapi yamesikizwa na mangapi hayaja sikilizwa? (7)kwanini? Naombeni msaada kwahayo wadau
   
 14. d

  danizzo JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
Loading...