Senegal rasmi ndio wababe wa Soka la Afrika

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
1678781413313.png

Senegal mji mkuu Dakar hawa jamaa wapo serious sana na mpira tangia wajifunze makosa yao kupitia kizazi ya kina Tony Silva, Ferdinand Coly, Fadiga, Diof...nk chini ya Kocha fundi Bruno Metsu(Rip) baada ya kutikisa World cup ile jamaa kama walijisahau na baada ya kizazi kile kupotea walipata tabu sana kutengeneza kizazi kingine cha soka kilicho bora.

Baada ya kulifahamu kosa lao walikuja na hasira kubwa na kuwekeza kuanzia soko la vijana hadi la wakubwa nashangaa vilabu vyao havifanyi powa sana kwenye michuano ya Afrika wajipange na hapo ili waanze kuleta upinzani kwa timu za Kaskazini mwa Afrika.

Kwanini wababe kwanini wameshindikana tambua mpaka sasa Senegal wamebeba makombe yote muhimu ya Africa unayoyafahamu anzia AFcon Wakubwa, Afcon 20, Chan kama sikosei na Soka la Ufukweni beach soccer, Senegal hawajaibuka kama uyoga bali yalikua malengo ya muda mrefu kwa maslahi mapana ya timu yao na kuzalisha ajira kwa vijana wake.

Haitakua vibaya kama Tff wakipeleka wataalamu wake kujifunza toka Senegal.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom