Sendeka: Kikwete ni kinara wa vita ya ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sendeka: Kikwete ni kinara wa vita ya ufisadi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Albedo, Oct 2, 2010.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Daniel Mjema,Moshi
  MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro,Christopher Ole Sendeka (CCM) amemtetea mgombea Urais wa CCM, Jakaya Kikwete kuwa ni kinara wa vita ya ufisadi.

  Alisema rais Kikwete ni kinara wa ufisadi na inavyoelezwa na viongozi wa vyama vya upinzani na kwamba wabunge wa upinzani walidandia hoja ya kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Sendeka alitoa kauli hiyo mjini Moshi jana katika eneo la uwanja wa kuoshea magari linalomilikiwa na Baraza la Wazee wa CCM Mkoa Kilimanjaro, katika mkutano wa kumnadi mgombea Ubunge Jimbo hilo, Justine Salakana.

  Mbunge huyo mteule ambaye alikuwa mwiba mkali katika mjadala wa kashfa ya ufuaji umeme ya kampuni ya Richmond, alisema kumnyoshea kidole Kikwete na CCM kuwa hakijashughulikia mafisadi nchini si sahihi hata kidogo.Katika mikutano ya kampeni, baadhi ya wagombea wa upinzani wamekuwa wakimtuhumu Kikwete kwa kutochukua hatua madhubuti za kupambana na rushwa ikiwemo kutowachukulia hatua watuhumiwa muhimu wa ufisadi.

  Wagombea hao akiwemo mgombea Urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amekuwa akimtuhumu Kikwete kwa kutowakamata wamiliki wa kampuni ya Kagoda iliyochota Sh40 bilioni za EPA na wale wa Deep Green Finance.

  “Jakaya Kikwete kwa mkono wake mwenyewe alimwandikia barua waziri wa fedha wakati huo Zakhia Meghji akimtaka aanzishe ukaguzi akaunti ya EPA, lakini bahati mbaya wapinzani wakainasa barua ile,”alidai Sendeka.

  Sendeka alidai kuwa baada ya wabunge wa upinzani kuinasa barua hiyo ndiyo, waliidaka hoja ya ufisadi na kuifanya ni yao kwao.

  “Kama kweli Kikwete angekuwa hachukii ufisadi angelivunja Baraza la Mawaziri na kukubali mawaziri wake kujiuzulu?, Vita ya ufisadi haikuanzishwa na wabunge wa Chadema wala CUF,”alifafanua.

  Alitumia mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wanachama wa CCM na wananchi wa Jimbo hilo, kuwaomba wamchague Salakana na kuwataka kupuuza mbegu za chuki zinazopandikizwa asichaguliwe.

  Akimnadi Salakana, Ole Sendeka alisema kama atachaguliwa, atakuwa kiungo muhimu kati yake na Rais wa awamu ya nne ambaye alisema hakuna shaka kwamba atafufua viwanda na kuongeza ajira kwa vijana.

  Awali ilielezwa kuwa mkutano huo ungehutubiwa pia na Mgombea Ubunge Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela lakini hata hivyo hakutokea katika mkutano huo na hakuna sababu zozote zilizoelezwa kuhusu jambo hilo.


  Source: Mwananchi
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi Akitokea Mtu Akamuuliza Sendeka Swali, Ana maoni Gani juu ya Kikwete Kusema kwamba Rostam ni Mtu Safi atasemaje?
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kikwete amtakasa Rostam, ASEMA NI MTU SAFI ALIYEENEA KAMA TIMU YA MPIRA Send to a friend Saturday, 02 October 2010 07:11 0diggsdigg

  [​IMG]Ibrahim Bakari, Igunga
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amemsifu mweka hazina wa zamani wa chama hicho, Rostam Aziz kuwa ni mtu safi na aliyeenea kila sehemu.Kikwete alisemna hayo wakati akimtambulisha Rostam, ambaye anatetea kiti chake kwenye Jimbo la Igunga ambako amekuwa mbunge tangu mwaka 1995.

  Kikwete alitua Igunga baada ya kukamilisha mikutano ya kampeni katika Jimbo la Igalula na Tabora Kaskazini katika mkoa wa Tabora.

  Akimnadi Rostam mbele ya halaiki kwenye mkutano uliofanyika Igunga Mjini, Kikwete alisema kuwa Rostam 'ameenea' na anaweza, hivyo wananchi wa Igunga hawana sababu ya kuacha kumpa kura.

  "Rostam ni kama timu iliyoenea, timu iliyokamilika kila idara, sasa mnataka nini tena...mnamfahamu, anawasaidia ni mtu wa watu, anawapenda," alisema Kikwete na kushangiliwa na wafuasi wa chama hicho waliofurika kwenye mkutano huo.

  Kikwete alisema pia kuwa angeshangaa kama wanachama wa CCM wasingempa nafasi ya kuwa mbunge wa chama hicho.

  Kwa upande wake Rostam alimsifu Kikwete kwa uongozi safi na kueleza kuwa yuko tayari kuwatumikia wananchi wa Igunga katika kipindi kingine cha miaka mitano na kwamba Kikwete asisumbuke kuwaza kura za Igunga kwani zipo asilimia 99.99.

  "Nimepita katika kata zote 26 za Igunga, wananchi wamenihakikishia kuwa kura zote ni za CCM, usiwe na wasiwasi... usihofie porojo za majukwaani," alisema Rostam huku akishangiliwa.

  Pia Rostam aliahidi kusaidia ujenzi wa daraja la Mbuto linalounganishanisha Wilaya ya Igunga na Shinyanga.

  Awali katika mkutano wa kwanza kwenye Jimbo la Igalula pamoja na Tabora Mashariki, Kikwete aliwataka wananchi kutochagua vyama alivyoviita vya wanung'unikaji na wanaohubiri kumwaga damu.

  "Wenye vyama hivi hawana sera, wao ni wadandiaji sera na wanung'unikaji tu, hawana kipya wakati mwingine wanahubiri kumwaga damu. Sasa hakuna damu itakayomwagika kwa mtu wa kawaida na hata hao wanaohubiri," alisema.

  Akizungumza hali za wakulima, Kikwete alisema kuwa serikali itabeba madeni yote ya vyama vya ushirika na kuwapa fedha ili kuwapa nguvu wakulima waweze kuuza mazao yao kwa kuwa vyama vya ushirika sasa vimeshapata uwezo na vinakopesheka.

  Kwa upande mwingine, Kikwete alisema kuwa serikali imetoa ruzuku ya mbolea ya Sh40 milioni kwa wakulima wa tumbaku na mazao mengine. Hata hivyo alitoa ahadi mbalimbali za maji na barabara.
  Akiwa njiani kwenda Kiomboi mkoni Singida, Kikwete alisimama katika Kijiji cha Makomelo na kuelezwa shida ya maji inayowakabili wananchi wa kijiji hicho.

  "Haya nielezeni matatizo yenu, mnataka tuwafanyie nini," alisema Kikwete na baadaye akampatia kipaza sauti mama mmoja na kusema: "Sisi hapa kama unavyotuona, tunataabika kwa maji... tunaomba sana utupatie maji."

  Kikwete alisema: "Nimeyasikia, sasa nachukua 'notebook' yangu na kalamu, ninaandika na matatizo yenu nitayashughulikia."

  Kata ya Shelui, Kikwete alisimama tena na mwenyekiti wa Kijiji cha Mselebwe, Said Tunu alipewa nafasi azungumze matatizo yao na kuyataja kuwa ni pamoja na ukosefu wa maji katika vijiji sita, barabara na zahanati.

  Hata hivyo, Kikwete alisema kuwa atakachofanya ni kuwasaidia kujenga kituo cha afya na kuwataka wananchi kukaa na halmashauri yao kwa ajili ya ujenzi huo wa zahanati. Leo atakuwa Singida mjini.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hilo swali gumu sana bana kama la policy forum kwenye TV
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Yaani Sendeka anasimama Jukwaani Na Kumsifia Mtu ambaye Anawanadi Watu Amabo yeye (Sendeka) Alidai ni Mafisadi?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mbele ya kugombea tumbo, kauli hizo si ajabu...watatamka kila neno la kumsifu JK...Hivi mnasahau kuna kazi nyeti ya UWAZIRI just around the corner:mad:
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ndio maana CCM wameingia Mitini kwenye Midahalo, kwa sababu ya Maswali kama haya
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Sitashangaa nikiona Sitta au Sendeka au Mwakyembe wakikumbatiana na RA
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ndivyo siasa ilivyo mkuu
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Sendeka anathibitisha ule msemo kwamba siasa ni mchezo mchafu.
   
 11. e

  emalau JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Siasa = Si hasa !
   
 12. K

  King kingo JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ,

  Hilo ndio tatizo la wabunge wa CCM ndio maana wanaitwa wanafiki
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Huu ndo mchezo wa siasa za bongo, huyu bwana anajua kuwa anachokisema ni kunyume cha yaliyoko moyoni mwake lakini anasisitiza tu!
   
Loading...