Semina Elekezi! Funika Kombe Mwanaharamu Apite! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Semina Elekezi! Funika Kombe Mwanaharamu Apite!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndallo, May 13, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Haiingii akilini kiongozi wa nchi na wananchi wa nchi yako wanakuona ukipita kwenye kila taasisi kutoa hicho tunachoambiwa ni semina elekezi huku bado ile semina elekezi iliyopita hakuna hata cha maana ambacho kimetendeka. Hii inatuonyesha kua kiongozi wa nchi hana hasira na anachokielekeza kwa semina hiyo elekezi. nina mifano michache tu ambayo ukiwa kama baba nyumbani unatakiwa uwe namna gani kwa unachokitaka kifanyike endapo pale familia inakwenda kinyume namatakwa ndani ya familia yako:
  1. Baba mwenye nyumba wakati unatoa semina huna hata sura ya kukasirika kuonyesha umekerwa na sekta husika.
  2. Baba mwenye nyumba huwezi kuwa umekerwa na sekta husika halafu unamuuliza muhusika huku unacheka japokua tunakujua baba mwenye nyumba tabasamu kwako ni asili yako.
  3. Baba mwenye nyumba iko siku mwanao alishawahi kukushauri siku ile unaimbia familia yako pale kwenye nyumba kuu kwamba familia isi shangae kuwaona baadhi ya wanafamilia wanaofunga tai wataozea gerezani lakini mwisho wa kutoa tamko hilo mwanao huyu akakuambia ''baba ungetakiwa hata uwe serious kwa tamko hilo''.
  4. Baba mwenye nyumba haiingii akilini kutoa semina hii elekezi wanao wakakuelewa na wakatenda hayo unayoelekeza huku nyuma kuna baadhi ya wanao walioasi nyumbani halafu ukaambiwa baba hawa hawafai kuwarudisha nyumbani lakini wewe ukwashika mikono juu na kuiambia familia kua hawa ni watu safi sana tena walisingiziwa.
  5. Baba kwanini huna mamlaka ya kusema wewe umekosa hutufai ondoka kuliko kusema anayejijua amekosa ajitoe mwenyewe huu baba ni kama mchezo wa kuigiza haiwezekani wanao wakakuelewa.
  6. Baba tunajua ndani ya familia yako kuna watoto wanyeyekevu na wachapa kazi mno na wanataka kuleta maendeleo ndani ya familia kwanini wewe mwenyewe baba umvunje moyo kwakumwambia apunguze spidi ya utendaji? kweli maendeleo yatakuja ndani ya familia kwa njia hii ya semina yako elekezi?
  Sina mengi zaidi ya haya japokua ninahamu sana ya kujua nini maana ya semina hii elekezi baba! au ndio tuseme ''funika kombe mwanaharamu apite''???
   
Loading...