Kwa sasa matabaka manne yanaibuka na kuzidi kuimarika kila kukicha. Tabaka la kwanza linaundwa na matajiri. Tabaka hili linaweza kumiliki sehemu kubwa ya uchumi wa nchi kwa njia ya ufisadi
kwa Lugha ya Kigiriki tabaka hili linaitwa Oligaki.
Inasemekana uchumi wa Tanzania kwa sasa unamilikiwa na familia tisa za matajiri. Hizi familia tisa zinaweza kutoa fedha ya kuendesha nchi. Tabaka hili la oligaki linatengeneza tabaka la pili ambalo ni tabaka la wateule wanaojiona bora kwenye jamii kwa Kigiriki linaitwa Aristokrasi.
Oligaki wataweka watu wao kwenye sehemu muhimu na nyeti kwa ajili ya kulinda maslahi yao kwa mwavuli wa maslahi ya Taifa, mfano benki, wizara nyeti (fedha) na kwenye ofisi za mabalozi za nje. Wanaowekwa katika sehemu (ofisi) hizo ndiyo wateule, yaani aristokrasi
Tabaka la tatu ni la watu wenye tamaa ya madaraka kwa Kigiriki tabaka hili huitwa Timokrasi. Hili ni tabaka linaloundwa na wanafiki wanaounga mkono hoja za oligaki (matajiri) na aristokrasi (wateule wa matajir