Poleni sana Walimu, Madaktari na Watumishi wengine.

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,622
Reaction score
3,147
Ndugu zanguni, naomba tuungane kuwapa pole Walimu, Madaktari na Watumishi wengine wa umma wa hali ya chini.
Serikali imeweka Matabaka makuu mawili ya Watumishi wa umma.

1. Walimu, Madaktari na Watumishi wengine wa umma (wa hali ya chini)

Hili ni tabaka la Watumishi wa umma wanaopata mshahara mdogo na kwa shida sana.
Mshahara wao hutumika:-
*Kupanga nyumba.
*Kununulia chakula, matibabu, usafiri na huduma zote katika familia.

2. Mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa Idara, Wabunge, Wakuu wa Mikoa/Wilaya nk.

Hili ni tabaka la Watumishi wa umma linalopendelewa zaidi na Serikali.
Watumishi waliopo katika tabaka hili hupata mishahara mikubwa na malupulupu ya kila aina.
Lakini kama haitoshi, Watumishi wa kundi hili mahitaji yao yote ya kila siku kwa asilimia kubwa hugharimiwa na Serikali.
Kwa mfano, chakula, gari+mafuta+Service, nyumba, muda wa maongezi nk.
Je, Serikali haioni kama hapa hakuna usawa?
Je, Walimu si Binadamu sawa na hawa wengine?
Kwa nini kundi moja lionekane ni bora zaidi kuliko kundi jingine?

Mimi naamini, Mkuu wa Mkoa ana Mahitaji ya kibinadamu sawa kabisa na Mahitaji anayohitaji Mwalimu.

Waziri mwenye dhamana, naomba majibu kabla sijaanza kuruka Sarakasi.
 
Siwezi kumpa pole mtumishi mimi hata siku moja..

Pole yangu nitampa mkulima sio mtumishi..

Ukimchukua mtumishi na mwanakijiji ukawaweka pamoja ,mtumishi kanawili na mwanakijiji kapauka..Kati yao wawili nani anastahili pole?.

Nimpe pole mtu mwenye uhakika wa salary,ana Bima ya Afya na anakopesheka,kuwa serious Mzee..

Mwisho hao sekta ya Afya ukiacha wizi wa dawa nk huwa Wana dharau na kauli mbaya kwa wananchi.
 
Well said
 
Hata wewe mwenyewe umeweza kuandika ujumbe huu kwa sababu ulifundishwa na mwalimu.
Elimu ni ufunguo wa maisha.
Kwa hiyo, hata mkulima anahitaji Elimu kwanza ili aweze kufanya kilimo chenye manufaa.
Kwa hiyo, vyovyote itakavyokuwa, Mwalimu alitakiwa kupewa kipaumbele sana.
 
Kwa hiyo? Kazi ya kuwa Mwalimu ni ipi kama sio kufundisha? Huruma itoke wapi sasa na ya nini hasa?
 
hatutaweza kuwa sawa maana hata mbinguni kuna mataji yanayong'aa na wale wa kuvaa mataji yasiyong'aa kabisa
 
Si sahihi kuwaweka makapuku Walimu wenye mshahara wa TGTS 771,000 mwezi mzima bila posho yoyote na Madaktari wenye TGHS 1,500,000+ Kwa mwezi na posho juu.

Anyway ualimu ni kazi ya kimaskini sana na huko wamejaa maskini hasa ambao Hadi akili zao zimelock.

TAIFA HILI HALINA USAWA NA HAKI.
 
Yan unawaweka walimu kundi moja na madaktar kwel hauko serious, hao walimu wangekuwa Wanafanana mishahara na posho na hao madaktar mbn wangevimba Mjini......
 
Back
Top Bottom