Selikali yasababisha matabaka tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Selikali yasababisha matabaka tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by silver25, Nov 12, 2010.

 1. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa matabaka manne yanaibuka na kuzidi kuimarika kila kukicha. Tabaka la kwanza linaundwa na matajiri. Tabaka hili linaweza kumiliki sehemu kubwa ya uchumi wa nchi kwa njia ya ufisadi…kwa Lugha ya Kigiriki tabaka hili linaitwa Oligaki.
  Inasemekana uchumi wa Tanzania kwa sasa unamilikiwa na familia tisa za matajiri. Hizi familia tisa zinaweza kutoa fedha ya kuendesha nchi. Tabaka hili la oligaki linatengeneza tabaka la pili ambalo ni tabaka la wateule wanaojiona bora kwenye jamii kwa Kigiriki linaitwa Aristokrasi.
  Oligaki wataweka watu wao kwenye sehemu muhimu na nyeti kwa ajili ya kulinda maslahi yao kwa mwavuli wa maslahi ya Taifa, mfano benki, wizara nyeti (fedha) na kwenye ofisi za mabalozi za nje. Wanaowekwa katika sehemu (ofisi) hizo ndiyo wateule, yaani aristokrasi
  Tabaka la tatu ni la watu wenye tamaa ya madaraka kwa Kigiriki tabaka hili huitwa Timokrasi. Hili ni tabaka linaloundwa na wanafiki wanaounga mkono hoja za oligaki (matajiri) na aristokrasi (wateule wa matajiri) kwa ajili ya kupewa chochote ili waseme lolote.
  Timokrasi ni watu wasio na msimamo wowote kwani wametawaliwa na tamaa na makuu, hivyo ni rahisi kuwasaliti wananchi.
  Tabaka la nne ni la wananchi wanaoishi kwa matumaini ya kupata maisha bora ambayo ni vigumu sana kuyapata kutokana na kuimarika kwa tabaka hizi.
   
 2. NTAKILUTA NDATO

  NTAKILUTA NDATO Member

  #2
  Jul 24, 2015
  Joined: Jun 19, 2015
  Messages: 27
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
   
 3. Mr Hero

  Mr Hero JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2015
  Joined: Jun 11, 2015
  Messages: 5,547
  Likes Received: 6,866
  Trophy Points: 280
  Sawa mgiriki
   
 4. NTAKILUTA NDATO

  NTAKILUTA NDATO Member

  #4
  Jul 24, 2015
  Joined: Jun 19, 2015
  Messages: 27
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Suala La Matabaka Linaogopesha Sana Kwa Maisha Yetu Wanadamu,
  Binafsi Naogopa Mtu Anayejiona Bora Kuliko Mimi Sijui Wewe, Halafu Mbaya Zaidi labda tunafanya kazi moja ktk eneo moja posho tofauti!, nakuwa namwomba Mungu Anipe Iman Tu/roho Ya Kumtegemea Kesho Japo Namwona (yeye udongo tu ua la kunyauka) Anauma Akipuliza.
  Kusema kweli penye MATABAKA kuna 'uadui', 'vita', 'mauaji,' wizi mkubwa',n.k japo kimya na kujitakasa kwa jina la DEMOKRASIA, na Amani Na Maridhiano Hutegemea Nguvu Ya Tabaka La Juu Kabisa Kwamba AMETUKUZWA?>ukitaka kuchomolewa roho uliza MKUU UNAFANYA NINI?... Uzoefu huu wa akili ya binadamu binafsi unapita ufahamu wangu..
   
Loading...