'Selfie' yaondoka na uhai wa msichana huko Urusi

'Selfie' yaondoka na uhai wa msichana huko Urusi

Kaondoka na utamu wake wote, huyu selfie kwanini asikamatwe
 
Tunaishi katika dunia ambayo watu wengi wanapenda kujipiga picha ‘selfie’na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Tabia hiyo ya kujipiga selfie inatajwa kuwa ni mapinduzi makubwa ya tasnia ya upigaji picha duniani. Pamoja na uzuri wake kuna matokeo hasi ambayo yanaweza kujitokeza kwa mtu pale anapotumia vibaya teknolojia hiyo.

Moja ya madhara hayo ni vifo kwa mshtuko wa moyo ambavyo hutokana na watu hao kujipiga picha kwenye maeneo hatarishi na muda usiofaa. Baadhi ya watu waliofariki kwa mshtuko wa moyo wakati wakijipiga picha katika maeneo mbalimbali duniani.

Huko Urusi, msichana mdogo aitwae Xenia Ignatyeya alifariki wakati akiwa juu ya jengo refu nchini humo. Taarifa zinaeleza kuwa hakushika vizuri fimbo aliyokuwa imeshikilia simu ambayo alikuwa anatumia kujipiga picha, alikosa mwelekeo na akaanguka chini kutoka kwenye jengo hilo ambalo lina urefu wa futi 820.

Chakushangaza ni kwamba alifariki kabla hajafika chini kwasababu aligusa nyaya za umeme wakati akishuka chini.

View attachment 733729

Kufahamu vifo vinavyotokana na kujipiga selfie soma hapa => Kujipiga picha za ‘selfie’ kunavyoweza kuhatarisha maisha yako

Siamini sababu mazingira ya tukio, kwanza hiyo fimbo alishikaje hapo, pili sioni nyaya za umeme hapo, na tatu naamin katika miji mikubwa miundo mbinu ya umeme inapita chini, lete ushahidi zaidi ili niamini
 
Back
Top Bottom