Hao Lowassa na papa fisadi ni wapambe wako maana wanakupamba kwa kila namna ili ukamuondoe mbaya wao kule Kyela.
Mimi sijakulink kabisa na hao mafisadi bali kilichokulink na hao mafisadi ni unachoandika hapa cha kuwatetea kwa nguvu zako zote bila kujali maslahi ya nchi yetu na kuthubutu kusema eti tufukie mashimo na kusonga mbele bila kutafutia ufumbuzi madudu chungu nzima ambayo yanaitafuna nchi yetu kila kukicha. Unayoyaandika yanaonyesha kabisa hufai kupewa wadhifa wowote ndani ya nchi yetu hata ujumbe wa nyumba 10 haukufai.
Katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inapita katika wakati mgumu kuliko wowote ule hatuhitaji Wabunge wa kufukia mashimo ili tu tusonge mbele wakati huko mbele kuna kiza cha kutisha na nyuma pia kuna madudu ya kutisha. Hatuwahitaji kabisa ndani ya Bunge letu Wabunge wenye kutaka kufukia mashimo kama wewe utakavyo.
Duh leo tangu asubuhi nilikuwa naipitia hii thread kwa makini sana sikupenda kuchangia ila kufyonza elimu taratibu.
Napenda kuwapongeza wachangiaji wafuatao.
[1] Bubu Ataka kusema
[2] Masanilo
[3] mzee Mwanakijiji
[4] Mkandara
[5] Steve D
Naomba tusikate tamaa tuendelee kupiga kelele kwa nguvu zetu zote hadi kieleweke.
Hapo ethiopia wengekuwa jela na vizazi vyao vyoe mana wangewachunguza kila mmoja wa familia kapataje hela kama kuna kauhusiano na hiyo deal ya richmond nae anaenda jela.na hapa bwana wanakuweka jela kama mwaka au zaidi ndio wanaanza kusikiliza kesiNapata shida sana kuelewa wanaoibeza kazi nzuri ya kamati iliyoongozwa na Dr Mwakyembe! Ni mfumo mbaya tulionao ingekuwa nchi zingine kama China RA na EL wameishanyongwa!
Kupiga kelele?? Kelele zitasaidia nini!! Nilidhani ungesema zichukuliwe hatua fulani ili kuzuia. Lakini kelele tu mtapiga wee usiku na mchana na hakuna kitachotendeka. Si umeona mwenyewe kelele za wabunge zilipolifikisha suala la Richmond!! Waliapa kuwa ikiwa serikali haitokuja na majibu ya kueleweka kwenye kikao cha Bunge lililopita wangepiga vote of no confidence kwa serikali. Mbonan hawakufanya hivyo na imo ndani ya uwezo wao? Wamebaki kulalamika tu.. Hebu jamani tuwe realistic for once..Watu wote wamo katika maslahi tu. Hakuna cha utaifa hapa..
Mzee wa NATO (No Action Talking Only), sisi huku tunaita wazee wa kubwabwaja. Kazi kujaza posts JF huku hakuna kinachofanyika. Afadhali hata sisi wengine tumehamasisha CHADEMA hapa Kyela na wamepata vitongoji vitano.
Kama unataka wafukia mashimo njoo huku Kyela uwasaidie, vinginevyo tegemea kubwagwa chini bwaaa! Mtavimba sana 2010.
Unaonaje wewe ukawe mfukia mashimo kwa kugombea huko kwenu?
Wewe isikie tu Kyela, hatuna habari na hao akina Lowassa au RA. Kyela hainunuliki. Mengi amejaribu kutaka kutununua kwa kugawa pikipiki lakini zimeishia kuchukuliwa na matapeli ambao hawawezi hata kumshawishi mtu mmoja. Wengi wao ndio hao walibwagwa na CHADEMA juzi.
Ha ha ha ha ha Mtetezi wa mafisadi!! by the way yule Mtanzania aka Mwakalinga ni engineer na wewe unajiita engineer je ni mtu yule yule katika jitihada zake za kuwakingia kifua wafadhili wae Lowassa na papa fisadi Rostam? Watu tumeshakushtukia ha ha ha ha ha.
Kwa sababu wewe unataka kuwa Mbunge wa Kyela basi unadhani kila mtu anataka Ubunge!!!!? LOL! unachekesha kweli wewe Mbunge Mtarajiwa 🙂
Kwa taarifa yako miye si mwanachama wa chama chochote kile cha siasa Tanzania na wala sina mpango wa kufanya hivyo katika siku za karibuni, lakini inapokuja kwenye kutetea maslahi ya nchi yangu hata siku moja sintosita kufanya hivyo kwa kuogopa kubandikwa lebo ya CHADEMA.
Mkuu wangu ni kelele hizo hizo zinakufanya wewe leo hii unaandika kuhusu Richmond.. Pasipo hivyo ungekuwa unazungumzia vitu vingine kabisa. Umeamka asubuhi na kutafuta mada ya mahusiano ya Richmond na ndio kwanza umeweka ubani wako...Hii inaonyesha wazi unakereka hivyo tutaendeleza kelele na imechukua miaka mitatu lakini kila Mtanzania anajua Richmond/Dowans ni kitu gani hata yule aliyeingia nchini jana..Kwa kukufahamisha tu nasikia hata Obama kisha mwagiwa radhi hiyo hana hamu na Afrika baada ya kutanguliza kumwamini JK..Kupiga kelele?? Kelele zitasaidia nini!! Nilidhani ungesema zichukuliwe hatua fulani ili kuzuia. Lakini kelele tu mtapiga wee usiku na mchana na hakuna kitachotendeka. Si umeona mwenyewe kelele za wabunge zilipolifikisha suala la Richmond!! Waliapa kuwa ikiwa serikali haitokuja na majibu ya kueleweka kwenye kikao cha Bunge lililopita wangepiga vote of no confidence kwa serikali. Mbonan hawakufanya hivyo na imo ndani ya uwezo wao? Wamebaki kulalamika tu.. Hebu jamani tuwe realistic for once..Watu wote wamo katika maslahi tu. Hakuna cha utaifa hapa..
Nina mashaka huyo mama wa mipasho katumwa na serikali kutuchanganya wananchi,ila mahali alipokosea ni kutaka kumsafisha lowasa kwa gharama yoyote ile.Nashukuru mungu watz siku hizi hatudanganyiki kirahisi.Hi,
Hii nchi ni ya watanzania,samahani kwa kuwa mbaguzi,na mwarabu(Rostam Azizi) hana nafasi kuvuruga hii nchi ya mzee kifimbo,huyu Rostam ni fisada na sheria ichue mkondo wake,na huyu mama wa mipasho rais amemtoa wapi ?
Elisante Yona
Mzee wa NATO (No Action Talking Only), sisi huku tunaita wazee wa kubwabwaja.
wala hawajagawanyika ila wapo wanaopiga kelele kwenye vyombo vya habari na wengine wanapiga kelele ndani ya chama, sasa hilo hatuwezi kusema kuwa wamegawanyika ila wanatofautiana jinsi ya kuwasilisha ujumbe tuu .sikonge mgawanyiko wa CCM uliopo sasa ni wa kipuuzi; it is purely personal.. hilo haliwezi kuwa msingi wa mabadiliko.
wala hawajagawanyika ila wapo wanaopiga kelele kwenye vyombo vya habari na wengine wanapiga kelele ndani ya chama, sasa hilo hatuwezi kusema kuwa wamegawanyika ila wanatofautiana jinsi ya kuwasilisha ujumbe tuu .
Mgawanyiko wangejitokeza hadharani na viongozi wao wangepaswa kujulikana hadharani na sio vinginevyo.