Tume ile ya bunge ya Richmond ndio ya kulaumiwa kwani kwa kauli ya Mwakyembe hawakuwasilisha yote kwa sababu ya kuilinda serikali. Sasa jiulize kuilinda serikali ipi je hii ambayo imeundiwa tume na Bunge ? na kama ni hivyo kwanini walitumia fedha za wapiga kura kuichunguza serikali ambayo wanailinda na hawako tayari kutoa uchunguzi, ni nani yuko juu ya sheria, kuyumba kwa serikali maana yake nini? kama ni Raisi tumeshaona watatu na si ajabu akijiuzulu huo ni uungwana.
Tayari tunaona kuwa hata tume ilikuwa na ufisadi, kwani kama kweli wanatume walikuwa na uchungu wa kweli na wazalendo wasinge nunuliwa kwa kuficha info ambazo leo hii kila kitu kingekuwa hadharani na wahalifu wangekuwa jela au serikali ingekuwa mufilisi.
Sasa maisha ya kulindana ndio yanatufikisha hapa, nani yupo tayari kumfunga paka kengele. Ukichora kutoka kwa Mohamed Gire mpaka Rostam unamkuta JK mara tatu. Sasa kweli mkulu ataachia.
Moja JK alipitisha kununuliwa kwa mitambo ya Mohamed Gire bila ya utafiti yakinifu, wakikubaliana kiusanii kwamba ni dharura, huku akiwa na ripoti za usalama wa taifa kwamba kampuni ile ni fafa. Akiwa na karatasi za tenda mkononi akasema mpeni.
Jk alibariki Richmond kuwa Dowans huku rafiki yake mweka hazina wa CCM akiwa mstari wa mbele kuona yanafanikiwa.
Jk alikuwa anabariki akisaidiana na DR. Idrisa wanunue mitambo mibovu ambayo ilinunuliwa kisanii. unganisha mchoro.
JK ndiye aliyemteua Dr. Idrisa kuwa mkurugenzi Tanesco, JK ndiye aliyemteua Rostam kuwa mweka hazina wa CCM, Jk ndiye aliyepitisha Tenda ya richmond, na JK ndiye alikubali mitambo iuzwe tena Tanesco kupitia kwa Dr. Idrisa.
Kumbuka DR. Idrisa aliposhindwa kazi JK ndiye aliyekataa asijiuzulu baada ya yeye mwenyewe kuomba huku JK akijua kuwa pamoja na yote Dr. Idrisa ni mshiriki wa rushwa ya Radar.
Sasa nani atamfunga paka kengele? zote ni ngonjera majibu wote wanayo wanatuchezea cheusi chekundu wajinga huliwa maisha yao mbele kwa mbele. hata Mobutu alikuwa na wapinzani vyama mia tano kwenye payroll yake, hivyo kelele hizi wanajipanga tu hakuna kitu hapa. Novemba itapita na tutasahau kama mengi yalivyosahaulika. Kwani kipi hatari kama sumu ya North Mara imeua, inaua na itaendelea kuua na mgodi unatema fedha huliwa USA na Canada, watoto , wake, waume na wanyama wakifa bila huruma and no body give a .......................................!!!!!!