Selelii aapa kuiangusha Serikali Novemba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Selelii aapa kuiangusha Serikali Novemba!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M-bongo, Aug 10, 2009.

 1. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Park mjini Nzega Mbunge wa jimbo hilo Mh Lukas Lumambo Selelii pamoja na mambo mengine alisema kuwa serikali isipowawajibisha watuhumiwa wote wa Richmond,na isipowapeleka watuhumiwa wote mahakamani basi atahakikisha kuwa serikali yote inajiuzulu na uchaguzi ufanyike upya! maneno haya aliyasema akisikilizwa na watu wachache katika viwanja vya parking Nzega, wasi wasi wangu hapa ni kuwa endapo hayo anayo yataka Selelii yasipotimizwa sijui yeye atakuwa tayari kujiuzuru? maana kuhutubia mkutano wa hadhara na kudai kuwa serikali lazima ijiuzuru mwezi Novemba binafsi naona kama uchochezi mkubwa sababu Seleli anayo nafasi kubwa ya kulizungumzia hilo kwenye viako ambavyo yeye ni mjumbe na analijua hilo
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Huenda vikao ndani CCM wamezibwa mdomo wasiseme ndo maana anakuwa na uhuru kuongelea Nzega!

  Ila huyu ni mpiganaji!!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,608
  Trophy Points: 280
  Kama huyu atafanya kweli hiyo Novemba basi tutamuweka katika kundi la mashujaa katika vita vya kupambamna na kuzuia ufisadi.

  Selelii kila la heri katika juhudi zako, usilegeze kamba mpka kieleweke. Watanzania tumechoshwa na ufisadi uliokithiri ndani ya Serikali ambao unasababisha nchi yetu kutokuwa na maendeleo yoyote.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  nadhani huyo bwana hali yake kisiasa sio nzuri ndani ya CCM ndio maana anatamka hivyo, kwani yupo mguu ndani nje kurudi mjengoni(dodoma), hicho kitu anachokiongea ni wazi kabisa hakiwezekani kwa serikali ya sasa ya ccm, ngoja tuone
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kaka yangu Seleli ni Msanii tu.

  Kwani yeye mwaka 2005 wakati wa uchaguzi, hakulamba 5M kutoka kwa mweka hazina wa CCM?
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  huyu kuna mawili:
  1-mpiganaji
  2-ameshathibitisha kutolewa nje ya system,anataka kutoka kivyake

  mimi namchukulia kama MPIGANAJI!........pambana babaangu!unasikika na kila mtu.watu wameshachoka sasa.tunasubiri muda ufike ''tujibwage majihani''
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Alilamba kama nini? ruzuku for campagning au kama mgao wa rushwa au mgao wa hela waliyoifisadi?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hold on wakuu....Kuna mtu alimrekodi CAM recorder hata sauti yake? November si mbali ili akinifanya amesahau tunamkumbushia ku-play back...wanasiasa ni balaa hataona aibu kusema nilinukuliwa vibaya!
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kweli bwana!huenda jamaa ana ''presha ya novemba''
   
 10. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  M-bongo, hii imekaaje? Hauko biased kweli?
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Thubutu!
  Mbunge gani yuko tayari kuachia ulaji wa milioni 12 kwa mwezi?
  Sanasana atajitahidi kuomba radhi kwa kauli zake hizi, then watamsamehe!
   
 12. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,465
  Likes Received: 1,413
  Trophy Points: 280
  watu kama SELELII ndio wanaweza kuwa wapinzani wa kweli, kwa sababu wana mengi ya kupigania ila chama chao cha mafisadi kinawazuia kwangu selelii ni mpambanaji
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Lipumba anasema, kama wao (Selelii, Kilango, Mwakyembe, Kimaro na wenzao) ni wapambanaji kweli basi waende upinzani, sio kupiga kelele wakiwa ndani ya chama kichafu ambacho nao ni sehemu ya uchafu huo!
   
 14. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nikuulize M-Bongo, unataka kumbana Selelli kwa ahadi yake. Hebu nambie: Wakiwakamata ma pawn wawili wizarani wakasema hawa ndio watuhumiwa wa Richmond, matakwa ya Selelii yatakuwa yametimizwa? Selelli amewatamkia "watuhumiwa wote wa Richmond" ni nani na nani na nani, kwa majina, ili tujue kwa uhakika matakwa na ahadi yake ni nini specifically?

  Anything short of that ni usanii. Na, anaposema "atahakikisha serikali inajiuzulu," amewaambia kwamba atafanya nini specifically? Ili asipofanya hilo uweze kumbana. Mbunge ana nguvu gani za kuhakikisha serikali inajiuzulu, ameahidi atatoa shilingi, au atamu impeach rais, au amewaambia atafanya nini huyu Selelii specifically? Ikifika Novemba anaweza kutoa spichi kali Bungeni ya kulaani serikali halafu akaoneka anapambana na ufisadi. Ahadi imetimizwa. Kwa nini hatujifunzi? Si kuna Mbunge wa Mwanza alisema safari hii bajeti haipiti. Ilipita? Wasanii.

  Tusichotwe chotwe kijumla jumla na ahadi fuzzy, za uongo. Ukitaka kumbana mtu kwa ahadi yake ni lazima ujue kwa uhakika kabisa 1 ) anataka nini kitokee specifically 2 ) ameahidi kisipotokea atafanya nini specifically.
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Umeshajiuliza kwa nini wabunge wote wa CCM huwa wanakazania Richomunduli tu na EPA wanakimbia kama mafuta ya moto? Nafikiri jibu utakuwa nalo sasa...... kumbuka kumbuka kumbuka, EPA kimyaaaa!!!!!!

  Rostam aliwakamatisha 5M. Ila hawakufahamu zinatoka wapi. Wamekuja kufahamu zilitoka wapi, Rostam lina sahihi zao wale wote waliochukua hizo hela na kuweka sahihi. Kwi kwiii kwiii, Mu-Iran yuyu ana akili! Kawashika wengi pabaya....
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,841
  Trophy Points: 280
  Bora waanze kulipuana wenyewe mapema kabla ya vikao vya mjengoni manake huwezi jua hiyo november watakuja na staili gani..........sio mara ya kwanza kwa wadanganyika kushikwa masikio ...ngoja tuone!!!!!
   
 17. Z

  Zyansiku Member

  #17
  Aug 10, 2009
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna memba mmoja wa JF ana msemo mmoja ambao nami nimetokea kuupenda ghafla kuwa UTAMU WA PILI PILI MUWASHO WAKE1! sijui huwa ana maana gani?
   
 18. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Lazima ianze kama inavyoendelea kwani kutakuwa na posibility tatu.

  1. Wanyamazishwe..waitwe na kimya kabisa wanyamazishwe.

  2. Waungwe mkono na sisiem wengine na mpasuko utokee..amabo utakuwa ni siginificant.

  3. AU hatimaye Wafukuzwe/ waondoke na kwnenda chadema au ...
   
 19. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tume ile ya bunge ya Richmond ndio ya kulaumiwa kwani kwa kauli ya Mwakyembe hawakuwasilisha yote kwa sababu ya kuilinda serikali. Sasa jiulize kuilinda serikali ipi je hii ambayo imeundiwa tume na Bunge ? na kama ni hivyo kwanini walitumia fedha za wapiga kura kuichunguza serikali ambayo wanailinda na hawako tayari kutoa uchunguzi, ni nani yuko juu ya sheria, kuyumba kwa serikali maana yake nini? kama ni Raisi tumeshaona watatu na si ajabu akijiuzulu huo ni uungwana.

  Tayari tunaona kuwa hata tume ilikuwa na ufisadi, kwani kama kweli wanatume walikuwa na uchungu wa kweli na wazalendo wasinge nunuliwa kwa kuficha info ambazo leo hii kila kitu kingekuwa hadharani na wahalifu wangekuwa jela au serikali ingekuwa mufilisi.

  Sasa maisha ya kulindana ndio yanatufikisha hapa, nani yupo tayari kumfunga paka kengele. Ukichora kutoka kwa Mohamed Gire mpaka Rostam unamkuta JK mara tatu. Sasa kweli mkulu ataachia.

  Moja JK alipitisha kununuliwa kwa mitambo ya Mohamed Gire bila ya utafiti yakinifu, wakikubaliana kiusanii kwamba ni dharura, huku akiwa na ripoti za usalama wa taifa kwamba kampuni ile ni fafa. Akiwa na karatasi za tenda mkononi akasema mpeni.

  Jk alibariki Richmond kuwa Dowans huku rafiki yake mweka hazina wa CCM akiwa mstari wa mbele kuona yanafanikiwa.

  Jk alikuwa anabariki akisaidiana na DR. Idrisa wanunue mitambo mibovu ambayo ilinunuliwa kisanii. unganisha mchoro.

  JK ndiye aliyemteua Dr. Idrisa kuwa mkurugenzi Tanesco, JK ndiye aliyemteua Rostam kuwa mweka hazina wa CCM, Jk ndiye aliyepitisha Tenda ya richmond, na JK ndiye alikubali mitambo iuzwe tena Tanesco kupitia kwa Dr. Idrisa.

  Kumbuka DR. Idrisa aliposhindwa kazi JK ndiye aliyekataa asijiuzulu baada ya yeye mwenyewe kuomba huku JK akijua kuwa pamoja na yote Dr. Idrisa ni mshiriki wa rushwa ya Radar.

  Sasa nani atamfunga paka kengele? zote ni ngonjera majibu wote wanayo wanatuchezea cheusi chekundu wajinga huliwa maisha yao mbele kwa mbele. hata Mobutu alikuwa na wapinzani vyama mia tano kwenye payroll yake, hivyo kelele hizi wanajipanga tu hakuna kitu hapa. Novemba itapita na tutasahau kama mengi yalivyosahaulika. Kwani kipi hatari kama sumu ya North Mara imeua, inaua na itaendelea kuua na mgodi unatema fedha huliwa USA na Canada, watoto , wake, waume na wanyama wakifa bila huruma and no body give a .......................................!!!!!!
   
 20. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135  Hawa jamaa na wengine wachache,ni wapiganaji kweli,na haya ni maoni ya baadhi ya watanzania ambayo yana ukweli ndani yake....Lakini katika kila roho ya binadamu kuna umimi....kwenda upinzani si jambo dogo.unaweza kufirisika ghafla...maana kule ni siasa tu hakuna pesa.CCM ni siasa na pesa,bila kujali km ni za kifisadi au laa...Km mtu anabisha akawaulize akina 'mzee wa kibaragashia' au mzee malando...

  jamaa wataendelea kuchonga,lakini wanaangalia na ugali wa familia......
   
Loading...