Selection vyuo vikuu: Fomu ya kujiunga, taarifa za vyuo na kozi

Selection vyuo vikuu: Fomu ya kujiunga, taarifa za vyuo na kozi

Afu MoCU wameachia selection ila wameweka faculty moja tu sheria
 
anayejua udom wanatoa lini adimision ltter anjuze plz naihitaj kwa ajili ya kuombea ruhusa kazin haraka iwezekanavyo.
 
jaman anaejua chochote kuhusu chuo kikuu cha saut MWANZA rafiki yangu amechaguliwa hapo anahitaji kujua zaidi kuhusu hicho chuo k.v hostels,mazingira, nk
 
Kwa wale waliochaguliwa chuo cha mwenge wanipim kuhusu room nje ya chuo 0715407588
 
Hostel zipo kibao tuu karibu na chuo kuanzia laki6 mpaka milioni kwa mwaka.Ajiandae Kuishi kana mwanafunzi wa sekondari chuo kina sheria balaa,msisitize sana atunze risiti mpaka mwaka atakapomaliza chuo vingenevyo atajuta,malipo alipie katika matawi yaliyoainishwa na chuo asimpe mtu pesa mkononi au akalipia kwenye matawi mengine yatamkuta yakumkuta.
Walimu wengi ni Wakenya wakuda wakuda hivii,Chakula Mwanza bei simple mnoo kama akiamua kupika au kula kwenye migahawa.Usafiri kwenda town ni ni wa uhakika,chuo kipo nje kidogo ya mji.Totozi za kumwaga awe makini boom linaweza kuisha kwa siku moja,kama hana ndugu au jamaa afikie nyegezi corner kuna guest za bei nafuu wakati akifatilia usajili na hostel.
Ushauri wangu akae mitaa ya nyamalango au kwa Masha,atafute mtu watakayeendana tabia waishi pamoja na wajipikie.Kama hela zake ni za kuunga unga aende Kuishi hostel moja ya wanaume watupu inaitwa Darfur,bei haizidi laki3, msosi ulikuwa unauzwa buku na mikopo ipoo,chumba mnaishi mtu4.
Kwenye masomo kuna magroup ya kudiscuss haya ndo yatakukomboa,atafute group la watu makini na wapenda shule,akifata magroup ya wauza sura utapata supp mpaka utaacha shule mwenyewe.
Tengeneza ghetto au chumba vizuri ili upate wageni wa kutosha,kuwa msafi,fanya mambo yako.Biashara pia zinaenda kama unatokea dar usije mikono mitupu njoo na sandals,jezi,jeans za bei poa,saa unaweka kwenye kibegi na madaftari ukikuta kikundi cha watu unawaonyesha bidhaaa tuu hii ni kama hauna aibu.Masomo mema.
 
Back
Top Bottom