Selasini avunjika mkono.

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,266
4,716
Yule mwanasiasa machachari anayegombea ubunge wa jimbo la rombo kwa tkt ya chadema amevunjika mkono (mara 3) na sasa anapata huduma pale kcmc
 
Mbona habari yako hii haieleweki, amepata ajali au imekuwaje? hadi akavunjika mkono?

Siku nyingine ukileta habari hapa nilizima ijitosheleze...

MODS, Mpeni nusu Saa awasilishe habari yake hii vizuri, hakishindwa ifutilieni mbali.
 
mganyizi,hili ni jamvi,unaleta mada watu wanadadavua,kama ikijitosheleza watu watajadiri nini?. Anyway amepata ajari kwenye kampeni. Nitakupa full story usiku wa leo.
 
MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Rombo, mkoani Kilimanjaro, Joseph Selasini, amepata ajali ya gari na kuvunjika mkono wake wa kulia mara tatu. Ajali hiyo ilitokea juzi saa 11:30 jioni, wakati mgombea huyo akitoka kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho kwenye kijiji cha Katangara, kata ya Katangara- Mrere, wilayani Rombo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika wodi namba 12, kwenye Hospitali ya Rufaa ya KCMC alikolazwa, Selasini, alisema ajali hiyo
ilitokea umbali wa mita 100, kutoka eneo alilokuwa akifanyia mkutano.
Alisema gari alilokuwa akiendesha, alikuwa ameambatana na viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya, Gabriel
Selengia, na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Wilaya (BAWACHA), Justina Mkenda, ambao wote hawakuumia.
Alisema alikuwa akiendesha gari aina Toyota Land Cruser yenye namba za usajili T 884 ABH; halikuwa na tatizo lolote na amekuwa akilitumia katika mikutano yake.
Kwa mujibu wa maelezo yake, alisema endapo asingechukua uamuzi wa kuligongesha gari hilo ukutani, angeweza kusababisha vifo vya waendesha pikipiki zaidi ya sita.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko, na Katibu wa CHADEMA Mkoa, Basil Lema, walithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari, mgombea huyo wa ubunge amevunjika mkono wake wa kulia mara tatu, ambapo pia mfupa unaounganisha vidole
viwili vya mkono huo umepata hitilafu.

TANZANIA DAIMA
 
MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Rombo, mkoani Kilimanjaro, Joseph Selasini, amepata ajali ya gari na kuvunjika mkono wake wa kulia mara tatu. Ajali hiyo ilitokea juzi saa 11:30 jioni, wakati mgombea huyo akitoka kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho kwenye kijiji cha Katangara, kata ya Katangara- Mrere, wilayani Rombo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika wodi namba 12, kwenye Hospitali ya Rufaa ya KCMC alikolazwa, Selasini, alisema ajali hiyo
ilitokea umbali wa mita 100, kutoka eneo alilokuwa akifanyia mkutano.
Alisema gari alilokuwa akiendesha, alikuwa ameambatana na viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya, Gabriel
Selengia, na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Wilaya (BAWACHA), Justina Mkenda, ambao wote hawakuumia.
Alisema alikuwa akiendesha gari aina Toyota Land Cruser yenye namba za usajili T 884 ABH; halikuwa na tatizo lolote na amekuwa akilitumia katika mikutano yake.
Kwa mujibu wa maelezo yake, alisema endapo asingechukua uamuzi wa kuligongesha gari hilo ukutani, angeweza kusababisha vifo vya waendesha pikipiki zaidi ya sita.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, na Katibu wa CHADEMA Mkoa, Basil Lema, walithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari, mgombea huyo wa ubunge amevunjika mkono wake wa kulia mara tatu, ambapo pia mfupa unaounganisha vidole
viwili vya mkono huo umepata hitilafu.

TANZANIA DAIMA

shy,asante kwa kuniokoa maana mganyizi alitaka nichukuliwe hatua kwa kudokeza habari za mgombea wa chadema kupata ajari.
 
Back
Top Bottom