Home tutor Dar
Senior Member
- Feb 23, 2025
- 122
- 148
Zanzibar imeandika ukurasa mpya wa kihistoria katika sekta ya utalii baada ya kufanikiwa kuvunja rekodi ya uingiaji wa watalii kabla ya kufika mwisho wa mwaka 2025. Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ndugu Arif Abbas amesema, hadi kufikia mwisho wa mwezi Oktoba 2024, visiwa hivyo tayari vimepokea watalii 743,605, idadi ambayo imezidi rekodi zote za miaka iliyopita katika historia ya utalii Zanzibar.
Ukuaji huu wa kasi ya juu unatokea licha ya changamoto kubwa za kimataifa zilizotikisa sekta ya utalii, ikiwemo janga la UVIKO-19 na vita vya Urusi na Ukraine vilivyopunguza uhamaji wa watalii duniani. Hata hivyo, Zanzibar imeendelea kuwa mfano wa uthabiti na mafanikio kwa sababu ya hatua thabiti zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kuboresha miundombinu, na kuongeza thamani ya bidhaa za utalii.
Kupitia sera rafiki za Serikali, maboresho ya viwanja vya ndege, barabara, bandari, huduma za wageni na mazingira wezeshi kwa wawekezaji, Zanzibar imeongeza ushindani wake katika soko la kimataifa. Aidha, upanuzi wa bidhaa za utalii umechochea ongezeko hili, zikiwemo; Utalii wa Michezo (Sports Tourism), Utalii wa Maadili – Halal Tourism, Utalii wa Afya (Medical Tourism), Utalii wa Mikutano pamoja na ule wa Makongamano na Matukio maarufu kama MICE Tourism. Aidha, Utalii Endelevu (Sustainable Tourism) unaoendana na dhana ya “Tourism for All”, kuhakikisha utalii wenye manufaa kwa jamii, uhifadhi wa mazingira na ushirikishwaji wa wote.
Kupitia mikakati hii, Zanzibar imejijengea sifa kama moja ya maeneo bora zaidi kwa utalii barani Afrika na duniani kulikopelekea kushinda tunzo sita kutoka majukwaa tofauti ya kimataifa kama vile Worlds Travel Awards, Payne Awards,Trip Advisor, Travel and Leisure Indias Best Awards na Travelers Choise Awards.
Uvunjaji huu wa rekodi kabla ya kumalizika kwa mwaka sio tu ishara ya ukuaji wa sekta ya utalii bali ni uthibitisho kuwa Zanzibar inaendelea kupaa kwa kasi, na inajiimarisha kama kitovu kipya cha utalii wa kimataifa.
-
#ZBCUpdates