sekretarieti ya maadili ya umma inafanya kazi kwa manufaa ya nani hasa?

gwijimimi

JF-Expert Member
Sep 24, 2011
7,344
3,604
Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995.
inasema kifungu cha 18 (b) kinaeleza kuwa; Sekretarieti itapokea malalamiko na taarifa za ukiukwaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma kutoka kwa wananchi.

Kifungu cha 18 (c) Sekretarieti itachunguza tuhuma yoyote ya kuvunjwa kwa sheria ya maadili ya viongozi wa umma na viongozi wote wa umma wanaopaswa kuwajibika chini ya sheria hiyo.
pia sekretarieti katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa vipengele hivyo, itakuwa na mamlaka ya kupokea na kusikiliza malalamiko yote kuhusu kiongozi yeyote wa umma yawe kwa mdomo au kwa maandishi kutoka kwa si tu wabunge hao bali kwa mwananchi yeyote bila kuuliza majina na anwani za watu waliopeleka malalamiko hayo.

sasa ni wiki kadhaa sasa since wabunge na watu maarufu wamtuhumu mkuu wa mkoa wa dar es salaam bwana paul makonda kwa kua na mali nyingi ndani ya miaka miwili na utajiri unaotiliwa shaka

Suala la utajiri wa Makonda, liliibuliwa bungeni kwa mara ya kwanza Februari 6 na Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma akitaka mteule huyo wa Rais achunguzwe kwa kujilimbikizia mali.

kama nilimnukuu bwana Msukuma vyema ,alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tu wa wadhifa wake kama mkuu wa mkoa, Makonda amejilimbikizia mali likiwamo gari aina ya Lexus, lenye thamani ya Sh400 milioni.

Mbali na mali hizo Msukuma alisema Makonda anamiliki magari mengine ya kifahari aina ya V8, anajenga maghorofa jijini Mwanza na amekarabati ofisi yake kwa Sh400 milioni bila kutumia utaratibu wa sheria ya manunuzi.
hili la kukarabati ofice tunajua lazima kuna mhisani au mfadhili but sheria inasema Hata kama anachangiwa na wahisani, sheria inamtaka atangaze alivyopata pesa hizo na ni miezi imepita na hajajitokeza kufanya hayo Achunguzwe na Vyombo vya Dola.

moja:Makonda amenunua apartment pale Viva Towers kwa Sh600 milioni.
mbili:Makonda amempa mke wake gari aina ya Mercedes Benz lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani (Sh550 milioni) kama zawadi ya ‘Birthday’,”


here comes my surprise “Ana ma-V8 na Mwanza amejenga jengo la ghorofa…ni kina nani wanaotakiwa kujadiliwa na kufanyiwa uchunguzi? Na hawa mawaziri tulionao humu kwanini wamepigwa ganzi? Utawala bora, Mambo ya Ndani na Waziri wa Sheria…kwanini mmepigwa ganzi?”

last but not least how can makonda afford kwenda likizo Paris na Marekani na kukaa siku 21 hasa ikizingatiwa kuwa tiketi moja ni Dola za Kimarekani 14,000 huku yeye na mkewe jumla ikiwa ni dola za Kimarekani 28,000.??

hii tume ya maadili inadeal na watu gani hasa?for me each and everythng is clear wanasubiria go ahead from whom exactly?
kwani wao sio tume huru?
huu ukakasi wanaupata wap na kwanini?n mostly importantly kwa manufaa ya nani?

huyu ni just mkuu wa mkoa je ikiwa waziri je?mfano mzuri ni ile case ya january na muitaliano
what about kitwanga na scandal za billion37?
nadhan we need clear separation of power
nahtaj kujua hii sekretarieti ya maadili ya uma inafanya kazi kwa manufaa ya nani hasa
 
Kuwa bavicha ni janga la taifa.
Umeandika mwenyewe kuwa kifungu cha 18(b) kinasema "sekretarieti itapokea malalamiko..."
Hivi umejiuliza nani kapeleka malalamiko na hayajashughulikiwa?
Au ulitaka wafanye kazi kwa kelele za bungeni? Wabunge baadhi yao wanaotuhumiwa kutumia ngada?

Au ulitaka wachukue hatua kwakuwa wewe umelalamika humu jf?

Ungejiuliza kwanza kwanini bunge au mbunge asipeleke rasmi malalamiko? Au wangeunda tume ya bunge kumchunguza kama wanaamini kile walichokisema.

Lakini naamini ile ilikuwa mbinu ya kumzuia asiwataje wengine
 
Back
Top Bottom