Jamii Opportunities
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 4,438
- 1,387
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 08 – 15 Februari, 2019 kuwa majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo na kupangiwa kituo cha kazi ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo Barabara ya Kivukoni, Jengo la Utumishi, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazijachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.View attachment Tangazo kuitwa Kazini.pdf
Sent using Jamii Forums mobile app