Malunkwi
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 339
- 79
Kwa wale waliofanya written interview ya Nationa Audit Office Sept 2011 waliambiwa kuwa Sekretariet iliamua kuita watu wengi ili iwaweke kwenye Database wale watakaofanya vizuri na litakapotokea hitaji la Auditors & Accountants(Wakaguzi/Wahasibu) serikalini bac watakua wakiitwa wale waliowekwa kwenye database hivyo hakutakua na haja ya kutangaza tena nafasi hizo hadi waliopo ktk Database watakapokwisha. Hivi karibuni watu wamekua wakiitwa kwenda kuchukua barua za Ajira na kwenda kuripoti kazini NAO na baadhi ya Wizara(ushahidi ninao). Sasa wasiwasi wangu ni kwamba kwanini wanaita watu kimyakimya? Na je tutaamini vipi kua hao wanaoitwa walifaulu ktk mchakato mzima wa usaili wkt Sekretarieti haikutoa orodha yao?
Upo uwezekano mkubwa wa kuingizana kwenye ajira za serikali pasipo hata kufuata taratibu hivyo sina imani na Sekretarieti ya Ajira, kwani watoto wa wakulima wataendelea kuchoma nauli zao kutoka mikoani kuja Dar es salaam kufanya usaili ambao nafasi zake tayari watoto wa walio ktk system washaanza kula mishahara.