Sekretarieti ya ajira mnajua mnachofanya kweli au mnafanya kwa mazoea?

Foul

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
787
1,147
Wakuu salaam, naomba niende moja kwa moja kwenye madam tajwa hapo juu

Sekretariet ya utumishi ya umma inachekesha na kuhuzunisha wakati mwingine

Eti leo, mie nimepitia kwenye a/c yangu ya kuomba AJIRA kuona Kama nimeitwa kwenye nafasi yeyote Kat ya nilizowahi kuomba lakini status imeandikwa NOT SHORTLISTED, Birth certificate not certified by Advocate/ Megstrate,

Maajabu Ni kuwa sina Cheti ambacho sija certify na nimeshafanya interview zaidi ya Mara 4 kwa vyeti hivyo hivyo

Hata juzi tar 14 January nilikuwa Dodoma kwa jukumu hilo Hilo

Basi nilidhan Ni tatizo langu mwenyewe, lakini kuna rafiki yangu naye tumeangalia kwake naye kaambiwa hivyo hivyo Japo yeye kaambiwa Ni Cheti Cha kidato Cha 4

Nimewapigia rafiki zangu Kama 4, mmoja tu ndo kaitwa na hao watu wamepewa sababu ambazo hawajajua kupewa huko nyuma na vyeti vyote vimehakikiwa.

Labda niwaulize hao watumishi wa hii idara muhimu, hivi mnakaa MNAFANYA tu rondom probability ya kuita walioomba na wengine kuwapa sababu yeyote lengo likiwa Ni kupunguza mzigo wa makaratasi ya kusahihisha au mnasoma kweli mnajiridhisha?

Kama tatizo Ni Hilo, so mtoe mitihani online na system iwe inasahihisha yenyewe? Kwanza mtawapunguzia vijana kero za kuomba nauli au wengine tunaotumia vimtaji vyeti vya ujasiriamali uliodumaa kuja kufanya mtihani wa dk 40 vitu alivyosoma kwa miaka 6.

Nimewahi kuuona ukurasa wao humu, sikumbuki Kama Ni rasmi au la! Kama Ni rasmi yeyote awatag hapa tadadhal au mods wawalete hapa, Najua namba zeo kule hawapokei na wanatoa simu kwenye holder ili wawe busy kila tukipiga na hakuna namna yeyote rasimi ya kuwafikia.

Sasa mie nimefanya interview Kama 5 kwa vyeti hivyo hivyo, Leo mmetoa wapi hiyo comment?
 
Pole sana mkuu, kama upo Dar, nenda ofisini kwao pale kivukoni wakakutatulie hiyo shida
 
No, written
Pole sana mwana SUASO.. Hizo walizokupiga panga ndio ziko nyingi zaidi.. post 100 mmeitwa 600+ tukiweka factor ya changamoto za maisha mngeenda watu 500. Kumbuka post 100 kwenye Oral watahitajika 300.. hapa usingokosa kupenya mkuu hata mpango wa kanzidata ungekuhusu😂
 
Pole sana mkuu, kama upo Dar, nenda ofisini kwao pale kivukoni wakakutatulie hiyo shida
Asante mkuu kwa ushauri, nipo mbali sana na hilo jiji linaloitwa Dar au Dodoma
 
Pole sana mwana SUASO.. Hizo walizokupiga panga ndio ziko nyingi zaidi.. post 100 mmeitwa 600+ tukiweka factor ya changamoto za maisha mngeenda watu 500. Kumbuka post 100 kwenye Oral watahitajika 300.. hapa usingokosa kupenya mkuu hata mpango wa kanzidata ungekuhusu
Asante mwanasuaso mwenzangu, kwa experience yangu, Kama wameita 600+ pekee, basi hawataenda zaidi ya 400
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom