Sekretariat ya ajira ni kikwazo kwa watanzania sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sekretariat ya ajira ni kikwazo kwa watanzania sasa

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Najijua, Oct 30, 2012.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [h=5]SEKRETARIAT YA AJIRA;

  Ndugu zangu napata shaka sana utendaji wa namna wa sekretariat ya ajira. Kuna wadau wameenda kufanya usaili nua kukutana na vikwazo vingi ambavyo vinatoa mashaka ya uafanisi wa chombo hicho.

  1. Mtihani wa usaili wanaopewa wa sailiwa huvuja mapema mfano jana wamepewa mtihani wa maandishi watasailiwa morogoro mtihani ni ulele uliofanyika Dar Es Salaam majuma machache nyuma na hakuna lilobadilika
  Hapa kukawa na wengine waliopata mtihani huo awali kwa wale waliosailiwa mapema na wengine walioenda wakiwa watupu hawajui hili wala lile. Je, kuna uafanisi na umakini hapa?

  2. Baada ya mtihani mchana wanaambiwa mtapigiwa simu kama utatakiwa kwa ajili ya hatua nyingie ya usaili na usipopata simu kwa siku hiyo jioni jihesabu kama umekosa.
  Maswali hapa ni je wana uwezo wa kusahisha mitihani ya watahiniwa zaidi ya 2,000 kwa masaa 4 mpaka 6 na kuweza wapigia simu watahiniwa?

  3. Kuwaita katika usaili watu kwa nafasi ambazo hawajaomba hili nalo linanipa shaka sana juu ya uchambuzi na weledi wa ndg zetu hawa wenye dhamana ya ajira hapa nchini katika idara za serikali.

  4. Kutoa muda mfupi sana wa taarifa ya kuitwa katika usaili, Kuchukua muda mrefu kuita watu katika usaili toka kuwasilisha maombi na tarehe ya mwisho kupita na kuchukua muda mrefu tena kuwaita watu kazini.

  Maswali hapa je wamejipanga sawa sawa kufanya kazi hii kwa ufanisi?
  Karibuni kwa mitazamo na michango mingine[/h]
   
 2. c

  chipalila1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hawa jamaa hata mm nnamashaka nao mambo yao slow mno cjui n kwa nn
   
Loading...