The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,111
- 115,905
Wataalam wa jukwaa hili
hebu kila mtu amwage utaalamu wa kutengeneza
sekela chicken humu.....tupate mlo saafi....
hebu kila mtu amwage utaalamu wa kutengeneza
sekela chicken humu.....tupate mlo saafi....
chicken "SEKELA", sina uhakika hili jina sekela lina asili ya wapi katika ulimwengu wa mapishi kama ilivyo chicken tikka n.k..kwa ufupi ni kuku wa kuchoma (grill, bbq sijui vinafanana!).
Mahitaji
Kuku alietolewa ngozi,(vipande, au mzima) kulingana na upendavyo .
Kitungu thoumu na tangawizi3 vijiko ,
Limau au ndimu,
Chumvi kiasi
Binzari 2 vijiko,
Masala ya Tanduri au Garam 2 vijiko
Pilipili mbichi iliyosagwa au black pepper 1kijiko
Ukwaju au vinegar 1/2 kikombe,
Soy sauc 3 vijiko.
Asali au sukari vijiko 3 au kadri unavyopenda radha ya utamu.
Rangi ya chakula(food color) kias (red yavutia zaidi, japo me hupendelea kipapripapri ama kijani) , Ongeza maji kidogo kama mchanganyiko utakuwa mzito sana, baada ya hapo una mloweka kuku wako(vipande, ama aliepasuliwa tu kati) kwenye mchanganyiko kisha una mwacha kwenye friji kwa muda wa masaa mawili. Hapo sekela anakuwa tayari kwa kuchomwa.