Seka Sekondari - Wanavijiji waamua kujenga maabara tatu za masomo ya sayansi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940
SEKA SEKONDARI - WANAVIJIJI WAAMUA KUJENGA MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI

Seka Sekondari ni sekondari ya pili ya Kata ya Nyamrandirira yenye vijiji vitano.

Sekondari hii iliyojengwa Kijijini Seka, Musoma Vijijini, ilifunguliwa tarehe 5.7.2021.

Sekondari ina jumla ya wanafunzi 344 (Vidato vya I, II & III) na Walimu tisa (9), mmoja akiwa ni wa kujitolea.

Mapungufu makubwa na muhimu ni ukosefu wa:
*Maabara 3 za masomo ya sayansi ya Fizikia, Kemia na Baiolojia.
*Maktaba
*Choo kingine chenye matundu 7
*Jengo la Utawala

HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO

Leo, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, ameendesha HARAMBEE shuleni hapo kwa ajili ujenzi wa MAABARA 3 za masomo ya Sayansi.

MATOKEO YA HARAMBEE YA LEO:

*Wanavijiji wameamua kwamba Maabara hizo zikamilike ifikapo tarehe 30 Juni 2023.

*Wanavijiji watachangia nguvukazi na Tsh 15,000 kila kaya

*Vifaa vya ujenzi vilivyosalia kwenye ujenzi wa kutumia fedha za Serikali, vitumike mara moja, ikiwemo Saruji Mifuko 60.

*Viongozi mbalimbali wa Kata hiyo, wakiongozwa na Diwani wao, Mhe Mwl Nyeoje wamechangia Saruji Mifuko 12 na fedha taslimu Tsh 100,000

Michango ya Mbunge wa Jimbo:
*Saruji Mifuko 150
*Vitabu vya Maktaba box saba (7)
*Mahindi magunia manne (4) ya chakula cha wanafunzi

OMBI MAALUM LA UONGOZI WA SHULE:
Seka Sekondari isaidiwe kupata, computer, printer na photocopying machine - Wanakijiji na Mbunge wao wa Jimbo, watachanga kwa pamoja na kuvinunua ifikapo 30.4.2023

MICHANGO YA AWALI YA UJENZI WA SEKA SEKONDARI
Sekondari hii ilianza kujengwa kwa nguvu za WANAVIJIJI, MBUNGE WA JIMBO, WAZALIWA WA KATA YA NYAMRANDIRIRA na baadae SERIKALI imetoa michango mikubwa.

Michango hiyo ni kama ifuatavyo:

WANAVIJIJI
*Nguvukazi - kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji
*Kijiji cha Seka kilijenga na kuezeka vyumba 3 vya madarasa na kununua samani za ofisi za walimu
*Kijiji cha Kasoma kilijenga na kuezeka vyumba 2 vya madarasa
*Vijiji vya Mikuyu & Kaboni vilijenga na kuezeka maboma 2 ya madarasa
*Kijiji cha Chumwi kilichangia ujenzi wa boma moja la darasa na ujenzi wa choo cha walimu
*Wazazi wanachangia malipo ya posho za walimu wa kujitolea.

SERIKALI imechangia, kwa nyakati tofauti, Tsh MILIONI 25 + 80 + 60. Vifaa vya Maabara na Tsh 891,436,- kila mwezi (uendeshaji) kuanzia Oktoba 2022.

Wanavijiji wa Kata ya Nyamrandirira na Viongozi wao mbalimbali wanatoa shukrani za kipekee kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa, wa ujenzi wa Sekondari yao, unaotolewa wa Serikali anayoingoza - AHSANTE SANA!

MBUNGE WA JIMBO
Michango yake ya awali, kwa nyakati tofauti, ni:
*Saruji Mifuko 200
*Mabati 120

Mfuko wa Jimbo umechangia:
*Saruji Mifuko 330
*Mabati 137
*Nondo 17

WAZALIWA WA KATA YA NYAMRANDIRIRA
Wazaliwa wa Kata hii wamechangia jumla ya Tsh 2,840,000,-

HALMASHAURI yetu hadi sasa mchango wake ni Saruji Mifuko 30 tu!

MGODI WA SEKA
Mchango wa Mgodi huu (MMG) wa dhahabu ni mdogo na hauridhishi!

PICHA za hapa zinaonesha matukio mbalimbali ya HARAMBEE iliyopigwa leo Seka Sekondari ya Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 2.2.2023
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-02-02 at 22.21.09.jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-02 at 22.21.09.jpeg
    108.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-02-02 at 22.21.23.jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-02 at 22.21.23.jpeg
    113.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-02-02 at 22.21.14.jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-02 at 22.21.14.jpeg
    97.8 KB · Views: 2
Pongezi nyingi kwa wananchi, haya mambo ndo yanafanya serikali kupunguza juhudi za uwekezaji kwenye elimu
 
Back
Top Bottom