Seif Sharif Hamad Kesi utoto unamsumbua, akikua ataacha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Seif Sharif Hamad Kesi utoto unamsumbua, akikua ataacha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Jun 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]

  Na Umar Mukhtar, Zanzibar
  [​IMG]


  MWANDISHI anayejitambulisha kwa jina la Dotto Kesi akili zangu zinanambia huenda anaandamwa na hali ya utoto pengine akikua na kupata makamo anaweza kuacha na wala hatafanya kama afanyavyo sasa akiniwinda, kuniandama na kunifuatilia na kunikosoa kwa njia za kunikatisha tamaa.

  Kwa mara ya kwanza aliniandikia ujumbe mkali sana wa baruapepe wenye sura ya kejeli huku akilalamika kwanini nimetumwa kumsakama na kuandika juu ya Seif Sharif Hamad kutokana na makala zangu zinazoelezea jinsi yeye na baadhi ya wenzake alivyoshiriki kumsaliti Rais wa Awamu ya Pili Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi.

  Moja katika makala hizo za nyuma nilisema Seif anasumbuliwa kisiasa na mzimu wa Jumbe hivyo ni heri aende mapema Mjimwema kumwangukia akimtaka msamaha kabla mzee huyo hajatawafu kwa sababu ni mwalimu wake mkuu wa siasa na pengine kama si Jumbe siasa za Zanzibar zisingemfahamu Seif.

  Wakati ule Seif akiwa bado hajaomba kufunguliwa milango na kuingia ikulu ya Zanzibar ili kukutana na Rais Dk. Amani Abeid Karume niliwahi kumrai na kumshauri kwa kaundika makala huku nikimtaka akubali kumtambua kuwa huyo ndiye Rais halali wa Zanzibar. Chelewa chelewa atakuta mwana si wake na ngoja ngoja yaumiza matumbo.

  Zaidi nikamwambia Maalim Seif kwamba katika mtazamo wangu hafifu namuona Dk. Karume kwa kiasi kikubwa ana tofauti na wenzake waliomtangulia, siasa yake ni ya kati na hivyo anaweza kuwa tayari kufanya chochote kwa ajili ya Zanzibar na watu wake.

  Alipokwenda wala hakuonyesha uungwana wa kusema hata Mukhtar siku moja kama aliwahi kushauri, hilo nimelipuuza, lakini ndiyo mambo akipata yeye tumepata sote. Kesi naye akakaa kimya kama jambo halikuwa.

  Katika hoja yangu juu usaliti kwa Jumbe na wala sikumbakisha Seif na baadhi ya wenzake nikiwataja kwa majina jinsi walivyoshiriki kwa lengo la kumdidimiza Jumbe hadi akaondolewa bila heshima madarakani na hilo wala sitaacha kulisema na hakuna wa kuninyamzisha.

  Katika baadhi ya wa makala zangu nyingine niliwahi pia kusema kwamba tegemeo la Seif katika njama za kumtosa Jumbe alifikiri angeweza kupata njia rahisi ya yeye kuingia Ikulu lakini kwa wakati ule akaula wa chuya.

  Baada ya kumtambua Dk. Karume kiko wapi, si huyo leo anakaa pale Bosnia, Maisra Suleiman kama Makamu wa Kwanza wa Rais, akiitazama bahari na kupata upepo mwanana badala ya ule wa mtoni kwenye zile nyumba za Tanesco.

  Najiandaa kuandika makala nikiielezea safari ya Seif katika siasa kutoka kuwa Msaidizi wa Jumbe, Waziri wa Elimu, Waziri Kiongozi, mtuhumiwa gerezani akisota miaka mitatu, akijiunga na Upinzani hadi kupigiwa sluti na majeshi kama bosi kubwa.

  Ghafla zikamiminika baruapepe kutoka kwa Kesi kwamba nimejipanga kummaliza Seif, namchukia kwa sababu yeye ana asili ya Kiarabu, nataja sana katika makala zangu habari na harakati za vyama vya Hizbu, ASP, ZPPP na Umma Party akidai hivyo mimi ni mfu na kaburu mbaguzi wa kutupwa.

  Kadri ya akili zangu zinavyoweza kufanya kazi kwa haraka,umakini na usahihi wakati fulani nikamtumia ujumbe kwamba mimi sitaki Zanzibar iwapo Serikali ya kitaifa, nataka wazanzibari wapigane na kuuana huku akiniita ati miye ni mhafidhina.

  Wakati fulani nikataka kuteleza kwa kutuma ujumbe nikimwambia kama ni Dotto wa kiume basi huenda akawa anajihusisha na mambo ya kishoga na hivyo hakuwa mtu mkamilifu wa akili za kawaida zenye ustaarabu.

  Siku moja nikwamwambia ikiwa huwezi kujenga hoja na anaanza kukimbilia matusi kisa tu asitajwe Seif gazetini sitamjibu na kwamba kama afanyavyo Seif katika majukwaa ya CUF akielezea maovu ya SMZ na viongozi wake basi pia huenda wako baadhi ya watu tunaomjua nje ndani na tunaweza kumwelezea yale asioyajua Kesi na utoto wake.

  Kuhusu uandikaji wa baadhi ya waandishi hapa Zanzibar baadhi yao kwao ni halali kuandika mema na mabaya ya vingozi wa Serikali lakini ni haramu na msiba kwao kuandika yale ya viongozi wa Upinzani hasa akiwamo Seif, hili kwangu halimo akilini na sitakuwa mjinga kutii utumwa huo wa mawazo.

  Wiki ya juzi niliandika kuhusu maisha ya Rais Kanali Muammar Gaddaf wa Libya,uongozi wake na maendeleo ya wananchi wa Libya. Mtazamo wangu kama alivyo yeye anavyomfagilia Seif na kumpembejea hata kwa sifa asizonazo na mimi vivyo hivyo akiguswa Gaddaf naweza jibu lolote kwa nguvu ya hoja na si kuropokwa kama afanyavyo Kesi dhidi yangu akinisulubu kwa misumari ya chuki.

  Katika mitiririko wa makala hiyo nikasema na kutoa mfano kwamba kutokana na viongozi wa Afrika kukosa msimamo ndiyo maana wakati fulani Mwalimu Nyerere Julius akaupa mgongo Umoja wa Afrika na kushughulikia zaidi harakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika chini ya nchi tano zilizokuwa mstari wa mbele.

  Chini ya hoja yangu hiyo nikaeleza kisa mashuhuri ambacho hicho ndicho kilichonipa fikara na kusema huenda kijana huyo Kesi ni utoto unaomamsumbua.

  Nikasema kuwa Rais Kwame Nkrumah kiongozi aliyekuwa akihimiza sana Umoja wa Afrika nchi yake ilitumika kupitisha silaha zilizokuwa zikipiganisha vita nchini Bukina Faso hivyo Mwalimu Nyerere katika kikao kimoja chsa OAU aliwahi kumlaamu kinagaubaga Dk. Nkrumah kwa usaliti huo.

  Nimesema Kesi ni mtoto asiyejua kitu zaidi ya kumpenda sana Seif na CUF na kwamba anafikiri hii ni hadithi ya kutunga, naamini wakati huo alikuwa pengine hajazaliwa, hajapata elimu na wala hajui afanyalo.

  Hapa Zanzibar kiongozi wa ASP aliyekuwa akishiriki sana vikao vingi vya PAFMECA na mjuzi aliyekuwa akiijua OAU ni marehemu Jamal Ramadhan Nasib, laiti anghelikuwa hai yeye anaufahamu vizuri mkasa huu.

  Isitoshe wala sikuandika kwamba kulikuwa na vita ndani ya Ghana, yawezekana huyo Kesi wakati akisoma alikuwa na uraibu kichwani mwake na akawa anazisoma herefu kinyume mbele kutokana na haraka za utoto alionao.

  Nani asiyejua ushujaa wa Mwalimu Nyerere anapotaka kumwambia mtu jambo analolikusudia, Dotto aambiwe, afundishwe kwamba hata huyo sahibu yake Seif ni Mwalimu Nyerere ndiye aliyemwambia na kumpasha bayana ndani ya kikao cha NEC ya CCM kuwa “Ni heri na bora zaidi utupinge ukiwa nje kuliko ukibaki ndani ya Serikali ya CCM.”

  Nyerere alimpenda sana Seif lakini alipotaka kumpasulia jipu hakumuonea aibu alimbinya na kumwachia machungu ambayo hakuyatarajia.
  Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanakielezea kisa hicho cha Dk. Nkrumah ni mithili ya dua baya ya Mwalimu Nyerere dhidi yake na hakikupita kipindi kikubwa akapiduliwa madarakani akiwa nje ya nchi yake.

  Tofauti ya Noriega na Ortega, Nicaragua na Panama ni vitu vya kawaida katika kukosena kujichanganya na wala sikusema Gaddaf alikuwa mtawala mwema sana ila nimekemea umwamba wa Amerika na jinsi Gaddaf alivyo bora kuliko marais wengine

  Afrika. umarjahzar@hotmail.com
   
Loading...