Sehemu za speech ya ferguson zilizonigusa

The Listener

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
993
Reaction score
217
Ferguson kaagwa jana na mashabiki lukuki wa Man utd huku vijana wake wakimpa zawadi ya ushindi wa mabao 2 - 1. Mara baada ya mechi alitoa speech yenye huzuni lakini yenye kutia matumaini. Sehemu za speech hiyo ni;

1. Ninayo furaha kubwa kufanya kazi na wachezaji wakubwa na maarufu duniani

2. Nashukuru kwa kunipa support ya kutosha na mnachotakiwa kufanya ni kumpa support manager ajaye

Alipohojiwa baada ya sherehe atakumbuka nini katika maisha yake ya soka man utd alijibu' Nitakumbuka na kuyamiss sana magoli ya dakika za mwisho' (Akanikumbusha yale magoli ya UEFA final 1999 dhidi ya The Bavarians)

The legend - the great manager of all time pumzika kazi hii ambayo wengi wamekuwa wakitimuliwa kwa kutopata matokeo mazuri
 
Haijawahi kutokea Kocha kama huyu aliyeweka rekodi ya kusajili wachezaji mpaka Kocha mwenzake wa kumrithi!

Wengine wote watabakia kupokelewa kama wafalme na kutimuliwa kama paka mla kitoweo. Mkuu nimesikia wakati sisi tulipokuwa tunasheherekea jana nyumba ya jirani kimenuka?
 

Ni kweli na kama ulivyosema ni katika ile orodha ya wanaopokelewa kama wafalme na kutimuliwa kinyemela!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…