Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali?

Wanabodi,

Hii ni sehemu ya pili, au muendelezo wa ile Makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla, ambazo zinachapishwa kwenye Gazeti la Raia Mwema la kila siku za Jumatatu.

Makala hii ni swali, la Jee Bunge linajipendekeza kwa serikali?, na sio statement, kuwa Pascal Mayalla, amesema Bunge Linajipendekeza kwa Serikali!.

Nimeuliza swali hili kwa mujibu wa haki zilizotolewa kwenye Katiba yetu za uhuru wa kujieleza, na kutoa maoni, Freedom of Expression, ila maoni hayo yasiingilie na kukiuka uhuru wa mtu mwingine.

Jee Bunge Linajipendekeza Kwa Serikali-2

Leo naendelea na sehemu ya pili ya makala hii ambayo ni swali, ikiuliza Jee Bunge letu linajipendekeza kwa serikali?. Katika sehemu ya kwanza wiki iliyopita, nilisema wazi kuwa hili ni swali, na jibu lake, sitalitoa mimi, ili nisije nikaitwa katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, na kuambiwa nimelidhalilisha Bunge. Ninachofanya hapa ni kukuwekea tuu tukio lilitokea, kisha wewe msomaji ndio ufikie uamuzi kama Bunge letu, linajipendekeza au laa, na wajuvi wa hoja hii wawe huru kupangua hoja kwa hoja, kama ni kweli linajipendekeza, au halijipendekezi!.

Na kwa vile mhusika mkuu wa huku kujipendekeza kwa Bunge kunakozungumziwa hapa ni Mhe. Spika, then naamini mjadala huu utafungwa kwa taarifa rasmi kutoka kwake au kutoka Bungeni kuwa Bunge halijipendekezi.

Baada ya kutoa hoja hizo, namalizia kwa kusisitiza kuwa

Haya ni maoni yangu binafsi yenye swali kuu la msingi kama jee bunge letu linajipendekeza kwa serikali, nikitaraji kupokea majibu, ama ni kweli linajipendekeza, au sii kweli, bunge letu halijipendekezi. Jibu la mwisho likiwa Bunge ni halijipendekezi, then Bunge letu na Wabunge wetu waendelee kuchapa kazi tuliowatuma kule Mjengoni, Bungeni Dodoma na kwenye majimbo yao. Lakini jibu likiwa Ndio Bunge linajipendekeza, then hapa tutahitaji mjadala wa kina, tufanyeje ili Bunge letu la Tanzania litimize wajibu wake ipasavyo ikiwemo kuisimamia serikali na sio kujipendekeza kwa serikali?.

Mungu Ibariki Tanzania
Wasalaam

Paskali
Asalaam Tanzania! bilashaka mmejibu kazi iendelee.

binafsi nimehuzunishwa sana na kauli ya SPIKA akiwa bungeni siku ya alhamisi tarehe 8/4/2021 yakuwa

"MKUBWA akishasema wengine inabidi tukae kimya"

Aliyasema hayo akirejea maoni yake kuhusu ujenzi wa bandari ya bagamoyo ambapo alisema rais alishauriwa vibaya.

Kiukweli kauli hii inaonesha udhaifu MKUBWA katika taasisi ambayo ilipaswa kuheshimika na kusikilizwa sana! Taasisi ambayo ni mhimili mkuu, taasisi ambayo inapaswa kuisimamia serikali, kutunga sheria na kutupa bajeti bora kwa maendeleo ya kweli kwa taifa letu.

Kistaarabu kauli ile (YA AIBU) ilipaswa kufutwa kwenye Hansard kwani inawafundisha wabunge ambayo wengine niwageni sio tuu kutoshauri kitu mkubwa (rais) akishakiongea! Bali kuwa waoga! bubu! na kutowasilisha matakwa ya wananchi waliowachagua!

Endapo kiongozi wako ananyamazishwa wewe uliye chini yake utasema nini?

Na huu ni uthibitisho mwingine yakuwa serikali ililiweka bunge mkononi na kuliamulia vyakusema, kwa bunge la namna hii tusitarajie maendeleo hili ni 'rubber stamp' ya nini serikali inataka.

Si ajabu sasa kuona wooote waliokosoa serikali waziwazi wametupwa pembeni kwenye uchaguzi wa aibu wa 2020. Sio ajabu kusema wabunge wa upinzani kupitia viti maalumu kuingia bungeni litakuwa ni agizo toka kwa MKUBWA kwenda kwa MDOGO.

Mhimili umegeuka sio mhimili tena,haustahimili kulibeba taifa na hauwezi. Udhaifu huu ni lazima tuuongee bila kukubali kuogopa vitisho na mateso yanayoweza kutekelezwa juu yetu! Tupaze sauti tulikatae.

BUNGE LA AIBU, AIBU, AIBU TUPU!
Hii iishie humu humu jf, ikitoka tuu nje, ikachapishwa na gezeti lolote, jiandae kuitwa Dodoma!.
Usije kusema hukujua, niulize mimi mwenzio, yalinikuta yepi?.
P
 
Na kwa vile mhusika mkuu wa huku kujipendekeza kwa Bunge kunakozungumziwa hapa ni Mhe. Spika, then naamini mjadala huu utafungwa kwa taarifa rasmi kutoka kwake au kutoka Bungeni kuwa Bunge halijipendekezi.

Baada ya kutoa hoja hizo, namalizia kwa kusisitiza kuwa

Haya ni maoni yangu binafsi yenye swali kuu la msingi kama jee bunge letu linajipendekeza kwa serikali, nikitaraji kupokea majibu, ama ni kweli linajipendekeza, au sii kweli, bunge letu halijipendekezi. Jibu la mwisho likiwa Bunge ni halijipendekezi, then Bunge letu na Wabunge wetu waendelee kuchapa kazi tuliowatuma kule Mjengoni, Bungeni Dodoma na kwenye majimbo yao. Lakini jibu likiwa Ndio Bunge linajipendekeza, then hapa tutahitaji mjadala wa kina, tufanyeje ili Bunge letu la Tanzania litimize wajibu wake ipasavyo ikiwemo kuisimamia serikali na sio kujipendekeza kwa serikali?.

Mungu Ibariki Tanzania
Wasalaam

Paskali
Hili jambo la deni la taifa, Spika alipaswa kulizungumzia Bungeni, na kule ndio kuisimamia serikali.

Hii maana yake sasa Bunge letu ndio linakwenda kuifanya ile kazi yake rasmi, tena ikibidi watunge kanuni, kabla serikali haijakopa, Bunge lielezwe, tunakopa fedha za nini, Bunge liridhie ndipo serikali ikope!.
P
 
Na kwa vile mhusika mkuu wa huku kujipendekeza kwa Bunge kunakozungumziwa hapa ni Mhe. Spika, then naamini mjadala huu utafungwa kwa taarifa rasmi kutoka kwake au kutoka Bungeni kuwa Bunge halijipendekezi.

Baada ya kutoa hoja hizo, namalizia kwa kusisitiza kuwa

Haya ni maoni yangu binafsi yenye swali kuu la msingi kama jee bunge letu linajipendekeza kwa serikali, nikitaraji kupokea majibu, ama ni kweli linajipendekeza, au sii kweli, bunge letu halijipendekezi. Jibu la mwisho likiwa Bunge ni halijipendekezi, then Bunge letu na Wabunge wetu waendelee kuchapa kazi tuliowatuma kule Mjengoni, Bungeni Dodoma na kwenye majimbo yao. Lakini jibu likiwa Ndio Bunge linajipendekeza, then hapa tutahitaji mjadala wa kina, tufanyeje ili Bunge letu la Tanzania litimize wajibu wake ipasavyo ikiwemo kuisimamia serikali na sio kujipendekeza kwa serikali?.

Mungu Ibariki Tanzania
Wasalaam

Paskali
Nakupa homework lakini hili Tatizo ni kubwa si kwa udogo huo wa batili au batilifu, hilo Bunge la kuisimamia serikali bado halipatikana Achana na spika ambaye yeye ni mtu mmoja tu
nimeipokea
p
 
Hoja za bandiko hili ni hoja za ukweli kabisa na zimetokana na udhaifu wa Mkuu wa mhimili.

Sasa imejitokeza fursa,
tusirudie makosa kuleta mtu tuu ili mradi ni mtu !, this time tunataka Spika Bora !.
P
 
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG).

Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge wamesikika hata wakishauri adhabu kali wapewe wahusika.

Bunge limehitimisha mjadala wa Ripoti husika. Nini kitafuata? Wahusika wa ufisadi na ubadhirifu huo mkubwa watafanywa nini na ni nani hasa mchukua hatua hizo?

Kiukweli, sisi walipa kodi wa nchi hii tungependa kuona hatua kali zinachukuliwa dhidi ya mafisadi na wabadhirifu waliotajwa au kuhusishwa na mambo hayo ndani ya Ripoti ya CAG.

Tunalipa kodi kwa maendeleo yetu. Kutumiwa isivyo kwa kodi na wale tuliowapa dhamana ya matumizi ya kimaendeleo ya kodi zetu kunaumiza sana. Tunatamani na kutaka hatua zichukuliwe. Wabunge wameona na kusema; wachukua hatua wafanye hivyo.
Mkuu Petro E. Mselewa, kwanza asante kwa bandiko hili Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?
Very objective, mimi msimamo wangu kuhusu Bunge letu, kwenye hoja ya bunge kuisimamia serikali, bado haujabadilika ni ule ule wa bunge lililopita Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?
Na hapa Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?
Japo Rais Samia ametoa maelekezo makali kwa maofisa masuhuli, hii ni kesi ya nyani kumpelekea ngedere!.
Kilichopaswa kufanywa on the first place ni kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG, alipaswa apishe kwanza, akiwa cleared ndipo arudishwe!.

Uko sahihi, tatizo watu wote walioko kwenye system wanajipendekeza chamani.
 
Back
Top Bottom